Uchumi wa Bluu ni dhana pana

Feb 13, 2017
5
8
Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Hassan Mwinyi alipoibeba ajenda ya uchumi wa buluu kwenye kampeni zake za mwaka 2020 kule visiwani na baada ya kukaa madarakani, wengi hatukumelewa.

Tukimshangaa kuona kakomalia shughuli moja tu, nayo ni uvuvi na kidogo kilimo cha mwani


Dhana ya Uchumi wa Buluu, kwa wengi ilikuwa mpya, hivyo hata wale ambao shughuli zao zinahusiana na bahari hawakuelewa kuwa ni sehemu ya uchumi huo.

Dr Mwinyi aliuangalia kwa mapana ambayo wengi hatukuyahusisha na uchumi huo pamoja na baadhi yao tuliyafahamu.

Hivyo basi, ilikuwa katika kuitafakari dhana hii nikakutana na Mtaalamu wa Uchumi wa Buluu, Betty Massanja ambaye anaielezea kwa lugha nyepesi kabisa akitumia mifano halisi.

Betty, anaielezea dhana hiyo kwa tafisiri yake binafsi, lakini BILA KUUPOTOSHA UKWELI, UHALISIA NA MUKTADHA, akisema, Uchumi wa Buluu ni dhana inayoakisi ama;

Shughuli au huduma za uzalishaji zitekelezwazo ndani ya vyanzo maji vya asili.

Mathalani, uvuvi, upakiaji au upakuaji wa shehena ndani ya vyombo vya usafirishaji kwa njia za maji kama vile boti, mitumbwi au meli.

Hili ni kundi la kwanza ambamo pia unazikita shughuli za extractives, kwa maana ya gesi, mafuta na madini, nazo pia hufanyika baharini na ni sehemu ya uchumi huo.

Kundi la pili analielezea kuwa ni zile shughuli zifanywazo nje ya vyanzo asilia vya maji kama vile shughuli za usafiri, usafirishaji na usafirishwaji wa ama bidhaa au watu baada au kabla ya kuingia ndani ya maji yatokanayo na vyanzo asilia vya maji kama vile kwenye bwawa kubwa, mto, maziwa SIYO YA KUNYWA, bali (LAKES) au mito.

Katika kundi hili pia kuna usafishaji bidhaa za ama uvuvi au kilimo - maji, ikiwa ni mojawapo wa mtandao na mnyororo wa uongezaji thamani wa bidhaa zipatikanazo ndani ya vyanzo maji asilia toaji.

Kundi hili la pili ndilo lenye shughuli nyingi zaidi katika mnyororo wa Uchumi huu ikiwemo pia uundaji wa boti na mashua za uvuvi au utalii wa ndani ya maji, meli za usafirishaji, uvuvi au utalii wa viwango vya juu.

Kuna usafishaji wa vyombo mbalimbali vitumikavyo katika uzalishaji wa ndani au nje ya maji.

Upo pia uuzaji wa nishati za kuendeshea vyombo au vifaa mbalimbali za uzalishaji ndani au nje ya vyanzo asilia vya maji kwa ajili ya Uchumi wa Buluu.

Uratibu na utunzaji kumbukumbu wa bidhaa, ukarabati wa vifaa mbalimbali vihusikavyo na Sekta ya Uchumi wa Buluu na ujenzi wa hoteli kwenye fukwe kwa ajili ya utalii wa fukweni na ndani ya maji

Hoteli hizo zinatoa fursa pia kwenye sekta ya huduma ndani ya hoteli za kitalii fukweni, mfano upishi, usafi na utembezaji watalii fukweni, na pasipo kusahau kuna shughuli za uzamiaji ndani ya vyanzo maji asilia.


Uchambuzi huu wa mtaalamu huyu ni machache tu kati ya mengi yahusuyo dhana nzima ya Uchumi wa Buluu.
 
Back
Top Bottom