Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

ACHA KUPOTEZA MUDA KUWATISHA WATU, fanyeni toba iliyo ya kweli mtasamehewa.

Haya, assume unatubu kwa mchungaji au padre alafu yeye ametoka kufanya dhambi kama yako na hajatubu?
Nimeandika wazi kabisa,

Nenda mtafute mtumishi wa Mungu wa Kweli aliyeokoka mwenye BUSARA ya Mungu.

Mbona mada Iko wazi, mnatafuta pa kujifichia?

Yesu alikwisha Sema, yaliyofanyika sirini, yatawekwa yote wazi, na pia imeandikwa, azifichaye dhambi hatafanikiwa.

Mungu ameelekeza, dhambi tajwa ni LAZIMA uhusishe Mtumishi wa Mungu wa Kweli aliyeokoka.

Na Kwa kuwa hujalazimishwa, ni hiari Yako kuamua.

Amen
 
Salaam shalom.

INTRODUCTON.

Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).

Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:


1. ZINAA NA UASHERATI.

UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.

UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.

Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.

Kuzini na mke wa mtu, faini ya juu ni kulipa Mahari aliyotoa muoaji Ili akusamehe, kushirikisha mtumishi ni kutumia BUSARA ya Mungu Ili muibiwa mke aridhie kukusamehe kutomlipa, au akupunguzie faini.

(Mithali 6:20-35,) UZINZI hufunga NAFSI, Amri ya Mungu usizini (Kumbukumbu la torati 5:1-21)

2. USHOGA.

Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko. ( Mwanzo 38:9-10) Mungu alimwua Onani Kwa kumwaga shahawa nje ya uke makusudi Ili asizae na mke aliyepewa.

3. USAGAJI.

Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. mwanzo 38:9-10, Onani aliuwawa Kwa dhambi hiyo, ( kumbukumbu la torati 5:1-21) Amri za Mungu Usiue.

4. PUNYETO/ KUJICHUA.

Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!! (Mwanzo 38:1-25) Mungu alimwua Onani Kwa kumwaga shahawa nje ya uke Ili asizae na mke wa marehemu kaka yake.
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.

5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.

Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. ( Mwanzo 38:9-10, (Mithali 6:20-35)Amen.

6. ORAL SEX.

Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.

(1 Wakorintho 6:9-11), (Ufunuo wa Yohana 21:8) (Mzo 38:9-10) Mungu alimwua Onani Kwa kutenda Tendo la NDOA kinyume.

7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.

Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.

(Kumbukumbu la torati 5:1-21) Usiue ni Amri ya Mungu.

Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.

9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.

(Mwanzo 38-9-10) Mungu alimwua Onani Kwa kutenda kinyume na Utaratibu wa Tendo la NDOA na taratibu za UZAZI alizoweka Mungu.


Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

10. MAUAJI.

Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi. ( Acts 9:3-6) Sauli alikuwa mwuaji, Yesu alimwelekeza aende Kwa mtumishi.

(Kumbukumbu la torati 5:1-21) Mungu ameamrisha " Usiue".

11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.

Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.

(Mithali 6:20-35) kifungo Cha NAFSI sababu Ibada ya sanamu ni UZINZI kiroho mbele za Mungu, ( UFUNUO 21:8, (1 korinthians 6:9-11) watendao uchawi na Ibada ya sanamu watatupwa Jehanum.

Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.

Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen

HITIMISHO.

Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.

NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.

ANGALIZO: Sadaka tutoazo Si Kwa ajili ya kununua Muujiza, au kununua Msamaha wa Mungu, Yesu msalabani alikwisha maliza yote Kwa Damu yake msalabani. Sadaka tunatoa kama shukrani tu na kuonyesha Upendo Kwa Yale Mungu alikwisha tutendea.

Mungu awabariki.

Source: Nabii Justine Ibrahim, U-Tube., Promover Tv channel U-Tube.

Ikiwa hujampokea Yesu kuwa BWANA na Mwokozi wako, fuatisha Sala hii,

EE YESU, NINAKIRI KWAKO KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU,ULIANDIKE KATIKA KITABU CHA UZIMA, NINAOMBA UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI, NIWEZESHE NIISHI MAISHA MATAKATIFU.

Ameen
Acha kudanganya watu. Kujua biblia na kuichambua haikufanyi ujitungie vitu ambavyo havipo huku ukirecall mistali ya biblia..
Labda utufafanulie, kwani biblia moja ina Agano la kale na Agano jipya?? Vitabu si vingejipanga tu bila kuvi categories agano la kale na agano jipya??
 
Pole sana, umenisikia nikifundisha watu kufanya uchafu?
Ndio,

Unapingana na mada, kwamba kwako,

Mtu akizini, au ameua mtu, au ni mchawi,

Wakijifungia na kutubu binafsi, unasema inatosha.
 
Ndio,

Unapingana na mada, kwamba kwako,

Mtu alizini, au ameua mtu, au ni mchawi,

Wakijifungia na kutubu binafsi, unasema inatosha.
Kwa hiyo mtu akipingana na hiyo imani yako potofu ndiyo anakuwa mzinzi?
 
Acha kudanganya watu. Kujua biblia na kuichambua haikufanyi ujitungie vitu ambavyo havipo huku ukirecall mistali ya biblia..
Labda utufafanulie, kwani biblia moja ina Agano la kale na Agano jipya?? Vitabu si vingejipanga tu bila kuvi categories agano la kale na agano jipya??
Kipi kimetungwa hapo?

Huamini zilizotajwa hapo ni DHAMBI?
 
Kwa hiyo mtu akipingana na hiyo imani yako potofu ndiyo anakuwa mzinzi?
Yaeza kuwa,

Narudia tena, dhambi hapo juu, bila kumshirikisha Mtumishi wa Mungu wa Kweli Aliyeokoka,

Sahau Mbingu.

Njia ya Mbinguni, ni nyembamba sana, ila njia ya Kuzimu ni Pana, na waendao huko hujifariji, pombe kidogo Haina shd, wengine ukiwauliza why mnavaa marozali, au why mnapigia magoti sanamu, unajibiwa ni Ishara tu, wengine ni Wachungaji na wanazini na waumini na wanatubishana gizani na kesho wanarudi kuzini.


Mimi nakuambia, moto unawahusu wote wataopuuza ujumbe wa Mungu.

Amen
 
Huyu Mungu anayehitaji kubembelezwa ni out of character na superior-being, hio ni moja mbili yaani ameteua watu ili wawe wawakilishi wake ? (delegation) ili iweje ?

Hio ni process tu ya kibinadamu ya baadhi ya watu kujifariji kwamba wao ni wateule kuliko wengine...

Anyway whatever tickles your fancy..., to each their own....
 
Yaeza kuwa,

Narudia tena, dhambi hapo juu, bila kumshirikisha Mtumishi wa Mungu wa Kweli Aliyeokoka,

Sahani Mbingu.

Njia ya Mbinguni, ni nyembamba sana, ila njia ya Kuzimu ni Pana, na waendao huko hujifariji, pombe kidogo, Haina shd, wengine ujiwauliza why mnavaa narozali, au why mnapigia magoti sanamu, unajibiwa ni Ishara tu, wengine ni Wachungaji na wanazini na waumini na wanatubishana gizani na kesho wanarudi kuzini.


Mimi nakuambia, moto unawahusu wote wataopuuza ujumbe wa Mungu.

Amen
Narudia tena, Yesu Kristo pekee ndiye mpatanishi kati mwanadamu na Mungu, tena ndiye anayetuombea kwa Baba. Acheni utapeli wa kuwafanya watu watoe sadaka ya ukombozi, huo ni wizi.
 
Narudia tena, Yesu Kristo pekee ndiye mpatanishi kati mwanadamu na Mungu, tena ndiye anayetuombea kwa Baba. Acheni utapeli wa kuwafanya watu watoe sadaka ya ukombozi, huo ni wizi.
Mimi nimemaliza.
 
Yeah!......Kuna dhambi ambazo muhusika mwenyekwe ni vigumu kuomba na kusikilizwa maana maagano aliyonayo hayaruhusu hayo, mfano uchawi/ushirikina, uuaji hapo lazima mtumishi amuongoze muhusika sala ya toba na kumtakasa kwa damu ya Kristo.
hiyo damu ya kristo munaitoa wapi kama sio kudanganyana
 
Narudia tena, Yesu Kristo pekee ndiye mpatanishi kati mwanadamu na Mungu, tena ndiye anayetuombea kwa Baba. Acheni utapeli wa kuwafanya watu watoe sadaka ya ukombozi, huo ni wizi.
Majizi kama yalivyo majizi mengine
 
  • Thanks
Reactions: len
Ni dhambi nakubali kabisa. Ila hizo complication za kutafuta mtu aliye okoka kwelikweli umweleze shida yako unatudanganya na unawakwamisha watu wengine ambao wanatamani kumrudia Mungu wao
Huo ndio UKWELI,

Hakuna nayemkwamisha sababu sijajitungia hayo, ni Mungu mwenyewe ndo anaelekeza hivyo.

Dhambi tajwa hapo juu Zina maagano na mikataba ya kipepo, zingine zinahusisha NDOA BATILI kati ya mtenda dhambi na Pepo, hivyo mfungwa hawezi jifungua pingu mwenyewe,

Kama una mashaka na viongozi ulionao, nenda sehemu ingine, upate msaada.
 
Huyo mtumishi unamuelezea dhambi ulizofanya au inakuwaje?
Ndio, unamshirikisha, ndomana ni LAZIMA awe ameokoka, mwaminifu,muadilifu, mtunza Siri.

Ikiwa Hana sifa hizo, usimshirikishe, tafuta mwenye sifa husika, usifungwe na mipaka ya dini.


Ubarikiwe
 
Kama kweli mbingu ipo,, basi tutafika tukiwa tumechoka mnoo..
Halafu naomba unitajie ni kifungu gani wameclassify ipi ni dhambi kubwa na ipi ndogo maana mimi najua kwa Mungu dhambi zote ni sawa isipokua kumkufuru roho mtakatifu
 
Kama kweli mbingu ipo,, basi tutafika tukiwa tumechoka mnoo..
Halafu naomba unitajie ni kifungu gani wameclassify ipi ni dhambi kubwa na ipi ndogo maana mimi najua kwa Mungu dhambi zote ni sawa isipokua kumkufuru roho mtakatifu
Mbingu ipo na ndimo Mungu anamokaa.
Kuhusu dhambi, hakuna dhambi, zote zilichukuliwa na Yesu,
Dhambi ya kumkufuru roho ni mtu kutokuamini ya kwamba Mungu alimtoa mwanaye kama ondoleo la dhambi ili kila aaminie asife bali aishi
 
Kama kweli mbingu ipo,, basi tutafika tukiwa tumechoka mnoo..
Halafu naomba unitajie ni kifungu gani wameclassify ipi ni dhambi kubwa na ipi ndogo maana mimi najua kwa Mungu dhambi zote ni sawa isipokua kumkufuru roho mtakatifu
Dhambi zote ni sawa,

Bt zipo dhambi zilizotajwa hapo juu, utaratibu wa kutubu pekeako ni ngumu.

Mfano, umezini na mume wa mtu, halafu umebaini kuwa huyo ni DHAMBI, niambie utatubu pekeako na mzinzi mwenzio chumbani na mkakubaliana kuacha bila kumwomba radhi muibiwa mume au mke?
 
Dhambi zote ni sawa,

Bt zipo dhambi zilizotajwa hapo juu, utaratibu wa kutubu pekeako ni ngumu.

Mfano, umezini na mume wa mtu, halafu umebaini kuwa huyo ni DHAMBI, niambie utatubu pekeako na mzinzi mwenzio chumbani na mkakubaliana kuacha bila kumwomba radhi muibiwa mume au mke?
Umwombe radhi muibiwa Tena… you can’t be serious 🧐
 
Back
Top Bottom