Desktop Icons zote zimepotea na siwezi ku-right-Click kwenye desktop Windows Xp

jacobae

Member
Oct 29, 2007
68
1
Kuna pc tatu zote zina windows xp, zimekumbwa na malware na wasi wasi kwani desktop icons zote hazionekani na wala siwezi kuright click kwenye desktop. Naomba msaada wa jinsi ya kurescue hii situation. Asanteni.
 
Umhh kuna watu bado wanatumia xp..

Subiri wataalamu watafika kukusaidia
 
duh, hiyo malware au virus nooma. never heard of it before, ngoja niwasubiri wataalamu wenzangu :biggrin:niskie hoja zao
 
shikilia bila kuachia hizi kex minya kwanza ctrl(usiachie) then minya alt(usiachie) then malizia delete hapo ikitokea task manager tafuta new task kisha andika explorer halafu minya enter
 
shikilia bila kuachia hizi kex minya kwanza ctrl(usiachie) then minya alt(usiachie) then malizia delete hapo ikitokea task manager tafuta new task kisha andika explorer halafu minya enter
toa maelezo mazuri..ukishaingia kwenye task manager nenda kwenye file juu pale then new ndo uandike io explorer then enter
 
desktop icon kupotea si virusi bwana ni feature ya windows mi kwa window 7 najua kuhide huwa tunafanyagaga hivi
-right click kwenye desktop
-click view
Utaona option ya kuhide au show desktop icon sjajua kwa xp kama ni same procedure

Na kama huwezi fanya right click try this solution
http://www.technize.com/cannot-right-click-desktop-or-in-windows-explorer

Naomba nieleweke, kwenye desktop huwezi fanya chochote kwa maana ya kuright click. Hilo swala la kuhide or view desktop icons nalifahamu lakini sio katika hii situation. Naendelea kusisisitza kuwa ni malware or virus naombeni msaada wa kuwatoa sasa.
 
Umeclick hio link au umesoma maelezo na kucoment
 
Kuna pc tatu zote zina windows xp, zimekumbwa na malware na wasi wasi kwani desktop icons zote hazionekani na wala siwezi kuright click kwenye desktop. Naomba msaada wa jinsi ya kurescue hii situation. Asanteni.
Ilinitokea kama wiki 2 zilizopita, inaonekana uliplug flash disk yenye files za system ya zamani zaidi, pia inaweza kuwa ni trojan, namna rahisi ni kuyaweka vizuri mafile yako na ufunge windows xp sp3 upya, tatizo lako litapotea, namna nyingine itakuchukuwa muda sana.
 
Kuna option ya kufanya System Restore (kurudisha kompyuta yako katika hali nzuri iliyokuwa nayo kabla hizo icons kupotea (reverse changes made in your computer)
Click Start >All programs>Accessories>System Tools>System Restore

Utaona screen inakuuliza Restore windows to an earlier point in time chagua Restore my computer to an earlier time halafu click Next, chagua "Restore point" tuseme kama siku mbili nyuma kabla desktop haijapotea then fuata maelekezo na Restart komputa yako.

Pia unaweza kufungua System restore kwa kutumia command prompt
Bonyeza Start > Run au Windows +R kwenye keyboard kutatokea box inayosema Run
kwenye box Run andika neno C:\windows\system32\restore\rstrui.exe halafu bonyeza Enter.
Fuata maelekezo kufanya System Restore

Ila kama ni malware itabidi pia ufanye scanning kwa kutumia antivirus yako. nakushauri u-start kompyuta yako kwenye safe mode na ufanye scanning kompyuta ikiwa kwenye safe mode ambapo ni rahisi antivirus kugundua malware au virus (ku start kompyuta kwenye Safe Mode itabidi ubonye Restart Computer, then wakati kompyuta inajaribu kuwaka na kabla login screen haijaonekana uwe unabonyeza CTRL +F8 kwa pamoja mara kibao mpaka itokee screen nyeusi itakuambia choose how to restart windows, chagua Restart in Safe mode. then fanya scanning

swali moja tu, je umefahamu ni malware gani ime-affect hizo komputa zako?
 
ndo hiyo uliotumia kuandikia hii theread au? kama vip nisichangie coz sina antvirus!
A%20S%20angel.gif
 
Back
Top Bottom