Hakukatishi tamaa, its time to show your man hood! Ni muda wa kujenga heshima ya kiume kutumia koo lako na mistari kama ulivyo anza badala ya kuamini katika vitu!Mtoto amekiri kesha kuelewa, go on with season 2, naisubiri bana!!Mh, sasa mbona unanikatisha tamaa tena jamani!
Hahahahaaa season 2 yaja mkuu, ngoja kwanza nifanye kazi nipunguze work log kidogo hapa kwa meza yangu then nitaendelea kushuka mistari wala usijaliHakukatishi tamaa, its time to show your man hood! Ni muda wa kujenga heshima ya kiume kutumia koo lako na mistari kama ulivyo anza badala ya kuamini katika vitu!Mtoto amekiri kesha kuelewa, go on with season 2, naisubiri bana!!
Hahahahaaa season 2 yaja mkuu, ngoja kwanza nifanye kazi nipunguze work log kidogo hapa kwa meza yangu then nitaendelea kushuka mistari wala usijali
Dear WEWE.S02E02
Mkutano aliohudhuria msichana siku hiyo ulichelewa sana kwisha na hivyo wakati anarejea ofisini kuchukua mizigo yake ya kawaida hakuwa anakumbuka tena kama kuna tukio lilitokea mchana ambalo kimsingi hakuwa amefika tamati yake. Alifika na kuchukua mkoba wake na kutoka ofisini kwani bosi wake alikuwa anamsubiri na alitaka kumpa lift ya kumrejesha nyumbani kwa siku hiyo kwani muda ulikuwa umekwenda sana.
Kesho yake asubuhi wakati anaingia ofisini alipita kama kawaida kwa yule sekretari rafiki yake ambapo walipiga stori mbili tatu na ndipo yule sekretari akamuuliza sababu ya kumuulizia yule kijana aliyekuja jana kwani hawakuwa wamekutana tena jana yake baada ya kwenda mkutanoni. Ndipo alipokumbuka habari ya ile bahasha ndogo iliyoonekana kuwa na barua ndani lakini hakuwa ameisoma. Bila kujibu kitu aliondoka na kwenda ofisini kwake ambapo alitafuta karibu kila sehemu lakini hakuweza kuiona mahali popote. Kasha lake la kuwekea takataka tayari lilishatolewa na kijana wa usafi na karatasi zote zilishatupwa na hata wakati anaingia ofisini alikutana na gari la kukusanya takataka likiwa linatoka maeneo ya ofisini kwao na hivyo alijua fika kwamba kwa namna yoyote ile ilikuwa imeshapotea na hakukuwa na namna yoyote ya kuipata.
Msichana alibaki na maswali mengi kichwani ambayo sasa yalianza kumfanya apate hofu
Mh msichana aliendelea kuwaza kwa muda lakini baadae alisahau tukio lile na maisha yakaendelea kana kwamba hakukuwa na kitu chochote kilichotokea.
- Ni nani aliyekuwa ametuma mzigi ule usiokuwa wa kawaida kwake?
- Kile ki ua chekundu kilikuwa na maana gani, maana kilikuwa kimoja tu tena kwasababu kilikuwa kimefunikwa kwenye mfuko kilishaanza kunywea.
- Nini kilikuwa kimeandikwa kwenye karatasi zilizokuwa ndani ya bahasha ile ndogo?
Je nini kitaendelea kwa jamaa atakapoona kimya? na nini hatima ya sakata zima?
Endelea kuwa nami..........
Dear WEWE.S02E03
Majira ya saa saba kasorobo mlango uligongwa wa hapo nyumbani kwa rafiki yangu, kwakuwa yeye alikuwa jikoni akiandaa chakula aliniomba nimfungulie huyo anayegonga. Nilitoka na kwenda mlangoni harakaharaka kwani kwa wakati huo nilikuwa naagalia zile Bongo movi zetu kwenye chaneli moja ya dstv nafikiri. Ile nafungua mlango tu nusura nipoteze fahamu, ulikuwa ni wewe ukiwa umesimama mlangoni.....................
Dah! Ilikuwaje baada ya hapo..........Tutaendelea tena kesho
Ua jekundu la hibiscus, biskuti pakiti 2 ndogo!!Hapa patakuwa na ujumbe uliofichika, nasubiri maana ya pakiti hizo mbili za biskuti, ua jekundu kwa mapenzi si jambo geni!!!
M'Jr umenikumbusha enzi zile nikiwa skuli Caigo, kuna mdada mmoja (Preta), nilimpenda sana aliniaga ya kuwa anaenda sokoni, nikamwomba akaniletee zawadi ile ambayo yeye angeona inanifaa!! Mkuu nililetewa NYANYA moja iliyoiva pyuuu, aliileta kwa mbwembwe nyingi sana!!!Mpaka leo hii nikimkumbuka huyu Preta wangu, hakika namwona mpya! Maana ya ya ile nyanya hajanambia mpaka leo, ila anasema siku si nyingi atanambia!!
Hahahaa hiyo nimeipenda, niruhusu niitumie kwenye sehemu mojawapo ya simulizi mkuu
Dear Wewe,
Yapata wiki ya tatu sasa nakuona ukiwa unatokea upande wa kaskazini wa pale ninapokuona kila siku asubuhi. Najua huenda hunijui lakini mie nakufahamu vyema kwani katika kipindi cha wiki tatu hizi nimefanya homework ya haja kiasi cha kujua mpaka nyumba uliyohamia. Labda nikukumbushe tu kama utanikumbuka, mi ni yule kijana niliyekusalimia siku ile ulipodondosha pochi yako baada ya kusukumwa na yule muuza matunda aliyekuwa na toroli pale kituoni, ingawa wakati najiandaa kuanzisha mazungumzo likatokea lile gari jeusi lenye namba za stk na ukapanda na kuondoka huku mi nikizuiliwa kuingia ingawa gari lilikuwa tupu.
Natumaini sasa umeweza kunikumbuka japo kidogo, najua utakuwa unajiuliza maneno meengi haya ninayoandika yana lengo gani, ntajaribu kupunguza maneno ili isiwe kama tuko kwenye mkutano wa siasa kule katani kwetu maana wale wanasiasa hupiga maneno mengi na dakika tano za mwisho ndipo husema lengo lao kubwa la kuwa kwenye mkutano ule. Basi mi nitaenda moja kwa moja kwenye dhumuni kuu ya waraka huu.
Baada ya kukuona siku ya kwanza na nakumbuka tulipanda wote daladala kuelekea mjini, moyo wangu ulihisi kupata ganzi. Sio kwakuwa we u mrembo sana, bali ni hali isiyoweza kuelezeka ya nguvu kali ya uvutano toka kwako ingawa nina shaka kama nguvu hii itakuja kuwa inatoka kwa pande zote mbili. Hata hivyo kwa kipindi chote hiki nimejaribu kufanya homework yangu ili kuweza kukufahamu nikisaidiwa na FBI ya kichwa changu, na LPD ya miguu yangu, CIA ya macho yangu na KGB ya masikio yangu. Pia nikapata msaada mkubwa wa Reuters na CNN ya karatasi na kalamu zangu ili kufanikisha mchakato mzima huu. Mchakato huu umefanikisha kujua mahali unapoishi, pale unapofanyia kazi, siku gani unazokwenda kazini na siku za mapumziko na hata kumjua yule rafiki yako ambaye nimekuja kugundua kuwa ni secretary wa pale kazini kwenu (yule mwenye maneno meeengi kama radio iliyowekwa betri mpya)
Jambo lililonopa moyo na mshawasha wa kuendelea na mpango wangu ni kutoona hata siku moja binadamu wa jinsia ya kiume akiingia ama kutoka pale nyumbani kwako. Hii ni kwa msaada wa CCTV kali za yule mama wa gengeni pale pembeni yenu, fundi viatu wa pale mwembeni pamoja yule dogo mjukuu wa mama mwenye nyumba wako ambao either nimelazimika kuwa mteja wa bidhaa zao au kulazimika kufadhili baadhi ya mahitaji yao ili kufanikisha kazi yao ya kuku-cctv na mimi kupata habari zote bila chenga.
Sasa hili ndilo langu ninalotaka kulileta kwako...........................................
Dont miss episode 2
Story umeifanya ndefu wakati ni fupi na pia sijapenda lugha ulizotumia, CCTV, FBI, CNN, CIA, LPD n.k na pia ulipomwambia rafiki yake anaongea kama radio iliyowekwa btri, sasa huyo ni rafiki hujawaona NDUGU si utaandika vitabu na kuwatungia movie kwa kuwa descibe????????