DCI Manumba astaafu, Kamishna Isaya Mungulu Mkurugenzi mpya wa Upelelezi

images
Z

out? in?
Isaya Mngulu amrithi DCI. Robert Manumba ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa Sheria..
kama ndio bac tumekwishaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa chama dume, na kama changoja naye akilamba uIGP tukivuka 2015 salama bila... bac mungu ashukuriwe sana, kwani maamuzi ya hawa ni ya kibabe sanaa yasiotumia hekima na busara.
 
Hilo tulilitegemea kwa kuzingatia kwamba ni mtumishi mtiifu wa magamba badala ya kuwatumikia watanzania wote.

Tume/kamati zote alizowahi kupewa kuziongoza juu ya mambo yenye utata matokeo yake yanatosha kumtambulisha yeye ni mtu wa namna gani.

Sasa tusubiri kibaraka mwingine wa magamba Andengenye akabidhiwe u IGP ili shughuli ikamilike.
Mkuu Mwita huyo mtu mie simjui na wala sijapata kumsikia! Hebu niambie issue yake yoyote ile labda naweza kumkumbuka kabla sijam-judge!
 
Tunampongeza na kumtakia utumishi mwema asimamie haki.

Simiyu usiwe mnafiki wa haki za watanzania...hebu jaribu kufungua box lako na kulichambua ....

Polisi wadai kumhoji ‘mtesaji' wa Ulimboka
na George Maziku

JESHI la Polisi nchini limedai kumhoji mtu anayedaiwa kuwa Afisa Usalama wa Ikulu, Ramadhan Ighondu, anayetuhumiwa kuwa mhusika mkuu katika tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Steven Ulimboka.
Akizungumza na Tanzania Daima jana ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi, Isaya Mngulu, alisema kuwa tayari polisi ilishamhoji Ighondu kwa tuhuma hizo........
......
Dk. Ulimboka alimtaja wazi wazi Ighondu kuwa ndiye alipanga na kuratibu njama za kutekwa kwake, na kusisitiza kauli yake hiyo kwa kula kiapo mbele ya wakili wake, Dk. Rugemezela Nshala, ambayo ilisomwa mbele ya waandishi wa habari.
Mngulu alisema kuwa jeshi la polisi lilishamuita na kumhoji Ighondu kuhusiana na tuhuma za utekaji na kutesa zilizotolewa dhidi yake na Dk. Ulimboka na kwamba hawakubaini ushahidi wa kutosha kuweza kumfungulia mashtaka mahakamani.
"Sisi tulishamhoji huyo Ramadhan Ighondu kuhusiana na tuhuma za Ulimboka dhidi yake, lakini hatukumfikisha mahakamani kwa sababu ushahidi haukujitosheleza.......


Aidha Mngulu alisema kuwa mbali ya kumhoji Ighondu, pia walimhoji wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, kuhusiana na suala hilohilo.
Hata hivyo, Kicheere alikanusha kuhojiwa na polisi kuhusiana na suala la Dk. Ulimboka, bali aliitwa polisi kuwasilisha tamko la kisheria (hati ya kiapo) la Dk. Ulimboka ambamo anathibitisha kuwa Ramadhan Ighondu ndiye aliyepanga na kuratibu njama zote za kutekwa na kuteswa kwake........
"Siyo kweli kwamba nimewahi kuhojiwa na polisi kuhusu suala la Dk. Ulimboka, hawajanihoji, ila niliitwa makao makuu ya polisi na nilipofika pale hawakunihoji chochote bali waliomba niwape ile hati ya kiapo ya Dk. Ulimboka ambayo niliisoma mbele ya waandishi wa habari, na pia niliwapatia cheti cha kisheria cha kuniidhinisha kuisoma hati hiyo kwa waandishi wa habari," alibainisha Kicheere na kuongeza: "Ila nimepata taarifa kwamba polisi wamepanga kuniita tena ili nikaandikishe maelezo, kwa hiyo nawasubiri waniite rasmi, lakini nasisitiza kuwa kwa sasa polisi hawajanihoji chochote kuhusu suala hilo," alisisitiza.
Hata hivyo, wakati polisi wakidai kumhoji Ighondu, hawajawahi kumuita wala kumhoji Dk. Ulimboka ambaye ndiye shahidi namba moja na mtu pekee anayewajua bila chembe ya shaka watekaji na watesi wake.

JE MPAKA HAPO BADO HUWEZI UNGANISHA DOTS?


 
Isaya Mngulu amrithi DCI. Robert Manumba ambaye amestaafu rasmi kwa mujibu wa Sheria..

Ndugu tofautisha kurithi nafasi na kukaimu nafasi,Kilichofanyika pale ni Isaya Mgulu kukaimu nafasi ya DCI Manumba aliyestaafu kwa mujibu wa sheria kama ilivyoelezwa,na wala Mgulu hajateuliwa kama DCI
Nafasi hii ni Presidential,ni mpaka Rais au Ikulu itamke lakini hili limefanyika ndani ya police mlemle,maana ya anakaimu tu,so far hata yeye Mgulu ameshastaafu toka mwaka jana,hapo alipo anatumika ki mkataba tu.
 
Historia itamhukumu............ ameacha viporo vya waliofanya uhalifu dhidi ya ulimboka, kibanda, mwangosi nk.
 
Ndugu tofautisha kurithi nafasi na kukaimu nafasi,Kilichofanyika pale ni Isaya Mgulu kukaimu nafasi ya DCI Manumba aliyestaafu kwa mujibu wa sheria kama ilivyoelezwa,na wala Mgulu hajateuliwa kama DCI
Nafasi hii ni Presidential,ni mpaka Rais au Ikulu itamke lakini hili limefanyika ndani ya police mlemle,maana ya anakaimu tu,so far hata yeye Mgulu ameshastaafu toka mwaka jana,hapo alipo anatumika ki mkataba tu.
Kama huyo Mngulu ameshastaafu na yuko kwa mkataba hawezi kupewa hiyo nafasi. Atachaguliwa mtu mwingine. Kiutaratibu mtu akistaafu huwa anaweza kupewa mkataba wa miaka miwili tu ikiisha ni lazima astaafu.
 
Mngulu will atakuwa DCI tu kwa traditional yao hao and he is a Nightmare bora hata Manumba .I know this guy .
 
Back
Top Bottom