Mkutano wa DCI wavunjika
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba hakutaka kuzungumzia suala hilo akisema: Hayo yote yameundiwa tume ngoja tuiachie ifanye kazi yake.
Awali, DCI Manumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari mkoani Iringa, ambao hata hivyo, ulivunjika baada ya kutokea kutoelewana baina yao.
Manumba alitaka kueleza ripoti ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, lakini waandishi hao walikataa kumsikiliza wakisema hawauamini uchunguzi huo kwa kuwa ulifanywa na polisi peke yao.
Kabla Manumba, hajaanza kuzungumza, Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Iringa (IPC), Frank Leonard alisema kutokana na msimamo wa waandishi wa habari wa mkoa huo hakutakuwa na uhusiano wa kikazi na polisi hadi pale tume zilizoundwa kuchunguza kifo hicho zitakapotoa taarifa sahihi juu ya mauaji hayo.
Msimamo wetu ni kusitisha uhusiano wa kikazi baina yetu na jeshi la polisi hususan Mkoa wa Iringa, tumekuja hapa kwa sababu DCI umetuita na kama unataka kutupa taarifa ya kifo cha ndugu yetu basi waambie hao maofisa wa jeshi wa Iringa watoke nje, alisema Leonard.
Akijibu madai hayo Manumba alisema: Nia yangu ni kutoa taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, ndiyo maana niliwasiliana na mwenzenu ili tuweze kuzungumza, Polisi Iringa wataendelea kuwepo na waandishi wa habari mtaendelea kuwepo, matukio kama haya yapo na yataendelea kuwepo.
Licha ya maelezo hayo, hakuna mwafaka uliofikiwa na mkutano huo ukavunjika.
Chanzo: Gazeti la Mwananci 6/9/2012.
Wanahabari na wananchi wote mnapaswa kuangalia ujumbe wenye maandishi mekundu kwa hadhari kwani yamkini DCI ameshatoa tahadhali ya kuendelea matukio kama yale yaliyomsibu ndugu Mwangosi popote na muda wowote ule. Kwa elimu yake, sidhani kama ulimi wake ulitereza kusema hiyo kama alisema hivyo.Kama alijua kuwa kuna tume juu ya kifo hicho yenye uwezo wa kutolea maelezo, yeye nani kampa kazi hiyo ya kuelezea chanzo cha kifo wakati si Daktari na si mwanatume? Atakayekaidi tahadhari ya muheshimiwa huyu, litakalomkuta asimlaumu mtu kwani hata Msajiri wa vyama vya siasa alishasema kuwa, zana za kazi za polisi ni silaha kama kalamu na komputa zilivyo kwa waandishi.