DC wa arusha mjini kazomewa na kupigwa mawe.

Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini amepigwa mawe na kuzomewa na wananchi wa kata ya daraja II ni kwenye kampeni ya udiwani kata ya daraja II..

Crash funguka zaidi, ilikuwaje hadi wakamzomea na kumpopoa na mawe? Mazingira yalikuwaje?

Matokeo ya uchaguzi wa Daraja 2 yatatoa mwelekeo wa uchaguzi wa Ubunge Arusha mjini, iwapo utarudiwa.
 
Alikuwa anatimiza kile kilichoandikwa katika katiba ya shishiem kuwa yeye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa wilaya,hivyo akaenda kupiga kampeni. hawa jamaa wa ajabu sana ona sasa>>>>>>>>>>
 
mkuu wa wilaya alikuwa anatafuta nini kwenye kampeni? Au alikuwa anamkampenia nani? Hawa watu wa ajabu sana, wanasahau kabisa kwamba nafasi zao ni za kiserikali na si za kichama. Ningewepo katika hao, ningemkamata na kumchoma moto kabisa.

Mkuu lukolo,ni sawa kwa namna ungependa kuonesha hisia zako.kumbuka kuwa mkuu wa wilaya ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya.so kama alikuwa hapo kwa majukumu ya kiofisi kwa kuzingatia majukumu yake hakuna tatiko,tatizo huwa wanapoanza kuleta ukada ktk kushughulikia mambo,by the way mleta uzi hajasema mkuu wa wilaya alikuwa eneo hilo kimajukumu au kimatembezi kwa kwa lipi na kwanin wananchi wamemzomea.
 
Mkuu lukolo,ni sawa kwa namna ungependa kuonesha hisia zako.kumbuka kuwa mkuu wa wilaya ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya.so kama alikuwa hapo kwa majukumu ya kiofisi kwa kuzingatia majukumu yake hakuna tatiko,tatizo huwa wanapoanza kuleta ukada ktk kushughulikia mambo,by the way mleta uzi hajasema mkuu wa wilaya alikuwa eneo hilo kimajukumu au kimatembezi kwa kwa lipi na kwanin wananchi wamemzomea.
Kwa imani yangu wananchi hawawezi kukurupuka na kuanza kumzomea au kumrushia mawe mkuu wa wilaya kama hakuleta siasa kwenye mambo yao. Kama mkuu wa wilaya angefika eneo la tukio kwa nia ya kusimamia mambo ya usalama, kwa hakika hakuna mtu angekuwa na shida na yeye. Lazima alileta kauli zenye upendeleo.
 
Anaitwa nani huyo gamba? sihitaji kuuliza alikuwa anafanya nini huko kwani bado nakumbuka kauli ya liwalo na liwe kuhusu kazi za maDC na maRC.
 
Mimi ningekuwa mkuu wa Wilaya nisingekaa nipigie campain chama cha siasa. Kazi kwenda mbele siasa mwiko..
 
Nafkiri ni yule aliyekuwa kigoma mjini mtoto wa Gamba mashuhuri.
Jina ni John Mongela nafikiri
 
Hawa mafisadi yani yao ni ngumu sana majira tunayoelekea nawaambia!

Bado kitambo kidogo sana watajajuta na bila majibu!

Wao wana pesa Sisi tuna MUNGU aishiye na kumiliki sasa na hata enzi hizo!

Kudadeeekii! Kwani hajapepewa kitu kizito chenye ncha kali?? Hawa vijana wa hapo Ngalelo hawajafika hapo Daraja mbili tu!

Mkuu wa wilaya ni serikali. Anampigia nani kampeni?


Hawa mafisadi kuna mahala wanafikaga wananichefua roho kabisa natamani nikajitowe nao mhanga lakini basi tu!
 
mzimu wa barlow umemjia huyu.wengi wa viongozi wenye vyeo hupenda waabudiwe,waogopwe na hata kusujudiwa.Wote twala,twaenda haja chooni,twavaa.cheo ni dhamana.heshimu na hudumia wa kwa nidhamu paripo kujali hali binafsi ya mtu,sote sawa.acheni hizo,hamtoi juic au keki kule maliwatoni.mbona mnajisikia sana?
 
A-Town inaongoza kwa kukagua wajinga na wenye magamba. Nasikia hata kuhamishwa kwa wamachinga ilisababishwa na kumpinga Mkuu wa Mkoa pale Soko Kuu.

Wajiandae kukamatwa.
 
Nadhan umetuachia maswali mengi kuliko majibu. Embu fafanua zaidi. Ilikuaje? Alikwenda kufanya nini? Alitaka nini? Kwanini kapigwa? Kamati ya usalama ya mkoa ilikuwepo? Polisi je? Kama walikuwepo, walikuwa wanaangalia tu? Mabomu ya machozi yameisha huko Arusha? Vipi maji ya kuwasha? Hakukuwa na taarifa ya kiintelijensia? Vipi kuhusu polisi jamii? Hakukuwa na vitu vizito? Je vyenye ncha kali? Funguka mkuu Crashwise!

Vyenye ncha kali havikuepo ila vizito vilielekezwa kwa DC.
Taarifa za kiintelijensia walikua nazo Raia wanusalama hawakua nazom kiao kiligeuka.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom