DC asifu mwenzake aliyecharaza walimu

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,926
31,169
• Asema alichokifanya ni sawa na kauli ya Pinda







MKUU wa Wilaya ya Maswa, Kapteni mstaafu, James Yamungu, amempongeza aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnali, aliyefukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete baada ya kuwachapa walimu viboko na kumwita kuwa ni shujaa.

Akizungumza jana wakati akifungua mkutano mkuu wa tatu wa Chama cha Akiba na Mikopo cha Nyalikungu SACCOS, alisema licha ya Mnali kufukuzwa kazi na Rais Kikwete, anabaki kuwa shujaa ambaye alikuwa akiwatetea Watanzania kuhusu suala la elimu.

Alisema baada ya rais kutangaza uamuzi wa kumfukuza kazi, wazazi katika Wilaya ya Bukoba Vijijini, walimwona shujaa aliyekuwa na uchungu na taifa katika sekta ya elimu.

“Ndugu zangu pamoja na rais kumfukuza kazi Mnali, wazazi katika Wilaya ya Bukoba Vijijini, pamoja na umma wa Watanzania, wanamuunga mkono na kumwona kama shujaa ambaye ana uchungu na taifa letu, hasa katika sekta ya elimu,” alisema DC huyo.

Yamungu ambaye pia ni Katibu wa Wakuu wa Wilaya Tanzania Bara, alisema kitendo alichokifanya Mnali ni sawa na kauli aliyoitoa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa ziarani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, baada ya kukerwa na vitendo vya baadhi ya watu wanaowaua walemavu wa ngozi (albino) na kutaka nao wauawe bila kujali sheria.

Alisema klabu ya wakuu wa wilaya Tanzania Bara, inasikitika kumpoteza mtu muhimu, kwani alikuwa mchapakazi mzuri na mambo aliyoyafanya wilayani Geita, akiwa mkuu wa wilaya ni mfano wa kuigwa, kwani alihamasisha wananchi kujenga shule nyingi za sekondari na alifanikiwa.

“Mnali mambo aliyoyafanya wilayani Geita akiwa mkuu wa wilaya ni mfano wa kuigwa, kwani alihamasisha wananchi kujenga shule nyingi za sekondari na kwa kweli nasema kwa moyo wangu wa dhati, tumempoteza mtu muhimu sana,” alisisitiza.

Alisema ni vizuri kwa wanachama wa chama hicho kuiga mfano huo wa kutetea mambo yaliyo na manufaa kwao kwa ajili ya kuendeleza SACCOS hiyo na hatimaye kuwa benki kwa lengo la kuwainua kiuchumi.

Mnali, aliamrisha kuchapwa viboko kwa walimu wa shule za msingi za wilaya yake ya Bukoba Vijijini, kwa kile alichodai kukithiri kwa utoro, uvivu na kusababisha wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba.

Kutokana na kosa hilo, Rais Kikwete aliamua kumvua madaraka, kwa madai kuwa alikiuka kanuni za utumishi wa umma na kulidhalilisha taifa.

Awali akisoma taarifa ya chama hicho katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana, Mwenyekiti wa Nyalikungu SACCOS, Sospeter Jafari, alisema jumla ya wanachama 348 wamekopeshwa sh 172,176,707 na zilizorejeshwa ni sh 98,476,930.
Source:Tanzania Daima.
 
Back
Top Bottom