DC aongoza maandamano kumuunga mkono Kikwete

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

SERIKALI wilayani Kwimba imesema kwamba, itawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wanasiasa watakaotumia majukwa kuitukana, kufanya uchochezi na kuhatarisha amani.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kupinga maandamano ya uchochezi, hivi karibuni mjini Ngudu, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Christopher Kangoye alisema wanasiasa ‘uchwara' wasiifanye Kwimba uwanja wa kupangia vurugu na uchochezi.
Kangoye ambaye ni Mtemi wa jeshi la jadi la wilaya hiyo (Sungusungu) alisema hayo baada ya kupokea heshima na salamu za askari zaidi ya 2,000 wa jeshi hilo , waliodai kwamba wamechoshwa maandamaono na mikutano ya uchochezi ya wanasiasa.
"Tutawakamata wanasiasa wanaodai wanakuja kufanya mikutano kwa nia nzuri kisha wanatumia fursa hiyo kufanya uchochezi, kumtukana Rais na Serikali, Kwimba siyo uwanja wa kupangia uchochezi," alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Alieleza kwamba nchi yetu imejengwa kwa misingi imara ya demokrasia, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa ambao unapaswa kulindwa kwa nguvu yote na kila mmoja, hivyo kuruhusu kundi la watu waivuruge ni kuuza amani ya watanzania.
Alisema maelfu ya sungusungu hao, wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, Vitongoji, Vijiji, Kata na wilaya waliohudhuria kwenye mkutano huo wa kupinga siasa za uchochezi zinazoweza kuvunja amani ya nchi, ni ishara kwamba wana Kwimba wanataka amani siyo mambo ya Tunisa au Libya .
Sungusungu hao wakiongozwa na Mteni wa Tarafa ya Ibindo Shimbi Mogani, wakiimba nyimbo za kusisitiza amani kwa lugha ya kisukuma,walisema uchaguzi umekwisha wana Kwimba wanachapa kazi na kusomesha watoto kuondoa umaskini na ujinga, waachiwe amani waliyozoea.
Waliimba "Obebe Slaa nelechama lyako mle bayojase." Yaani wewe Dk.Slaa na chama chako ni wachonganishi na kuwaasa wananchi wasiwape nafasi ya kuchochea vurugu na pia kumtaka Mtemi wao (Kangoye) achukue hatua kama serikali wilayani mwake wanapotokea wachochezi.
Awali mkutanao huo ulitanguliwa na maombi ya sala kuiombea nchi iwe na amani na kuepuka vurugu kama za Misri, Tunisia na Libta, kabla ya jeshi hilo kutoa heshina na nasaha hizo.
Waliotoa maombi hayo ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Kwimba Sad Seif(BAKWATA) na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa wilayani humo, Mchungaji Samuel Makima (AICT Kwimba) ambao walisema kuwa uchaguzi ulisha isha viongozi wakapatikana hivyo wajibu wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.
wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.

Mgambo wakiimba wimbo maalum kwa kilugha wenye ujumbe wa kukomesha maandamo yanoyafanywa na Chama cha CHADEMA.
 
hahaaa!! wanafuraisha kweli yani pamoja na umaskini mkubwa walionao bado wanakubali kudanganya kiraisi na kibaraka wa ccm(mkuu wa wilaya) kweli kazi ya ukombozi ni ngumu sana but tutapambana mpaka pumzi ya mwisho.
 
Olele kwa nini asiandamane kulinda kitumbua alichopewa na mumewe bila kustahili? Hili ndilo tatizo la katiba la kumpa mtu mmoja mamlaka ya kuwahonga watu vyeo. Ndiyo maana wanajazwa fikra za kiroboti roboti kama mbwa aliyefungiwa uani ambaye haishi kubwaka ili kumwonyesha bwana wake anafanya kazi alizotarajiwa. Hebu tazama wanaoitwa Sungusungu, ni waana CCM waliovalishwa vikolija vya kijani kwa fedha iliyofisadiwa, kodi ambayo hata wana CHADEMA wameilipa.
Shame to such leaders and their party - CCM.
 
SERIKALI wilayani Kwimba imesema kwamba, itawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wanasiasa watakaotumia majukwa kuitukana, kufanya uchochezi na kuhatarisha amani.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kupinga maandamano ya uchochezi, hivi karibuni mjini Ngudu, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Christopher Kangoye alisema wanasiasa uchwara wasiifanye Kwimba uwanja wa kupangia vurugu na uchochezi.
Kangoye ambaye ni Mtemi wa jeshi la jadi la wilaya hiyo (Sungusungu) alisema hayo baada ya kupokea heshima na salamu za askari zaidi ya 2,000 wa jeshi hilo , waliodai kwamba wamechoshwa maandamaono na mikutano ya uchochezi ya wanasiasa.
Tutawakamata wanasiasa wanaodai wanakuja kufanya mikutano kwa nia nzuri kisha wanatumia fursa hiyo kufanya uchochezi, kumtukana Rais na Serikali, Kwimba siyo uwanja wa kupangia uchochezi, alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Alieleza kwamba nchi yetu imejengwa kwa misingi imara ya demokrasia, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa ambao unapaswa kulindwa kwa nguvu yote na kila mmoja, hivyo kuruhusu kundi la watu waivuruge ni kuuza amani ya watanzania.
Alisema maelfu ya sungusungu hao, wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, Vitongoji, Vijiji, Kata na wilaya waliohudhuria kwenye mkutano huo wa kupinga siasa za uchochezi zinazoweza kuvunja amani ya nchi, ni ishara kwamba wana Kwimba wanataka amani siyo mambo ya Tunisa au Libya .
Sungusungu hao wakiongozwa na Mteni wa Tarafa ya Ibindo Shimbi Mogani, wakiimba nyimbo za kusisitiza amani kwa lugha ya kisukuma,walisema uchaguzi umekwisha wana Kwimba wanachapa kazi na kusomesha watoto kuondoa umaskini na ujinga, waachiwe amani waliyozoea.
Waliimba Obebe Slaa nelechama lyako mle bayojase. Yaani wewe Dk.Slaa na chama chako ni wachonganishi na kuwaasa wananchi wasiwape nafasi ya kuchochea vurugu na pia kumtaka Mtemi wao (Kangoye) achukue hatua kama serikali wilayani mwake wanapotokea wachochezi.
Awali mkutanao huo ulitanguliwa na maombi ya sala kuiombea nchi iwe na amani na kuepuka vurugu kama za Misri, Tunisia na Libta, kabla ya jeshi hilo kutoa heshina na nasaha hizo.
Waliotoa maombi hayo ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Kwimba Sad Seif(BAKWATA) na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa wilayani humo, Mchungaji Samuel Makima (AICT Kwimba) ambao walisema kuwa uchaguzi ulisha isha viongozi wakapatikana hivyo wajibu wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.
wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.

Mgambo wakiimba wimbo maalum kwa kilugha wenye ujumbe wa kukomesha maandamo yanoyafanywa na Chama cha CHADEMA.

Ndiyo faida ya kuwa na wananchi maskini na wenye elimu duni. Ni rahisi sana kuwakusanya na kuwashirikisha katika jambo lolote lile ilimradi uandae ng'ombe mmoja na Tshirts. Huo ndiyo mtaji wa sisiem. Wilaya zote ambazo literacy ya wananchi ni kubwa, siyo rahisi kuwakusanya na kuwapotezea muda wao wakiwa mabarabarani kuunga mkono jambo linaloleta hata ukakasi kulisikia. Poleni wana Kwimba kwa kutumiwa na mafisadi.

Baada ya maandamano hayo uchwara, sitashangaa kusikia mkuu wa wilaya amepandishwa cheo na kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
 
viongozi wa aina hiyo ndio wanaofanya watu wetu waendelee kuwa wajinga wasiojuwa haki zao kisiasa.
 
Huyu Kangoye ndo yule aliyeshindwa kwenye ubunge Tarime? Kumbe ana hisa na anapalilia ulaji zaidi kwa kutumia uelewa mdogo wa hao sungu sungu!
 
Umaskini sio kukosa mali tu. Hata ukiwa na fikra potofu wewe ni maskini wa kutupwa
 
Kuna Matatizo mengi kweli Wilayani Kwimba, lakini tatizo aliloliona ni la kitaifa - kufunda Mikutano ya Chadema
 
Hao wote wanalinda kazi zao, hakuna jipya wanalotoka nalo zaidi ya kutapatapa!
 
Hivi kwa mtaji huu, nani mwanzilishi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe (umwagaji damu)?
Hivi ccm wanadhani sungusungu wote wanawaunga mkono wao?
Tafakari
 
Wasiokuwa na taarifa kama wewe ndio wanamuunga mkono JK.

Haukatazwi kufikiri hivyo. Sote tulikuwepo mwaka 2005, 2010 hadi leo. Nje ya JF, JK bado anakubalika sana tu. Kuna wanaonufaika sana na yeye kuwa Rais wa Tz.
 
Back
Top Bottom