DC aongoza maandamano kumuunga mkono Kikwete

Well done wana kwimba na DC wenu mmeonyesha njia na wengine watafuata kwa kuepuka kuwa mbuzi wa kafara kwa manufaa ya wachache wa CHADEMA walioshindwa kupata uongozi wa njia za demokrasia kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki

Liwepo jukwaa la mizaha na vituko!
 
No. Ungemwambia wajinga/wapumbavu kama yeye ndo wataendelea kumuunga mkono jk.

Unatukana mamilioni ya Watanzania pamoja na baadhi ya ndugu zako. Sio mbaya. Ukweli una tabia ya kuchukiwa, kubezwa......
 
[/COLOR][/SIZE]

unachokisema ni kweli kabisa, mfano hapo kwenye RED ni watu kama Rostam Aziz & co, na makuwadi wao kama wewe.

Uzuri wako wewe kwa siku za karibuni unanishambulia mimi badala ya hoja ninazotoa. Ukweli haubadilishwi hata kwa kuupaka rangi.
 
masikini weeeeeeee umasikini wao ndio unatumiwa kuwadanganya wana kwimba wachache.........
 
Enzi za kuupinga ukoloni na hata wakati wa harakati za kupinga ubaguzi Afrika Kusini kulikuwa na vibaraka katika kila nyanja ya maisha ambao walikuwa wanalipwa kutafuta habari na wakati mwingine kuwauwa waliokuwa wanapigania uhuru/haki, waliandaa matamasha na mikutano ya hadhara kama hii na wakaiita mikutano iliyoandaliwa na wananchi kuunga mkono serikali iliyopo (ili wale wanaodai haki waonekane ni wahuni wachache tu ndo wanaopiga kelele) hata sasa tumeona maandamano ya namna hii kule Tunisia, Misri, Libya, Yemen, n.k. lakini mwisho wa yote ile sauti halali ya wanyonge ilisikika na mwangwi wake ni mkuu, hakuna awezaye kuuzuia hata kama ana majeshi yenye nguvu kiasi gani
 
tunapoelekea si kuzuri hao sungusungu sijui wanajua nini kuhusu haki za kibinadamu na uhuru wa kuongea! Kama polisi tulionao wanatumika na CCM kuua waandamanaji basi tutarajie machafuko soon maana hao sungusungu watapewa sh 50 ya gongo halafu kitakachobaki ni fujo tu! tuwaulize Kenya watuambiwa vyanzo vya mchafuko yao ni nini siku zote?
 
SERIKALI wilayani Kwimba imesema kwamba, itawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wanasiasa watakaotumia majukwa kuitukana, kufanya uchochezi na kuhatarisha amani.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kupinga maandamano ya uchochezi, hivi karibuni mjini Ngudu, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Christopher Kangoye alisema wanasiasa ‘uchwara' wasiifanye Kwimba uwanja wa kupangia vurugu na uchochezi.
Kangoye ambaye ni Mtemi wa jeshi la jadi la wilaya hiyo (Sungusungu) alisema hayo baada ya kupokea heshima na salamu za askari zaidi ya 2,000 wa jeshi hilo , waliodai kwamba wamechoshwa maandamaono na mikutano ya uchochezi ya wanasiasa.
"Tutawakamata wanasiasa wanaodai wanakuja kufanya mikutano kwa nia nzuri kisha wanatumia fursa hiyo kufanya uchochezi, kumtukana Rais na Serikali, Kwimba siyo uwanja wa kupangia uchochezi," alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Alieleza kwamba nchi yetu imejengwa kwa misingi imara ya demokrasia, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa ambao unapaswa kulindwa kwa nguvu yote na kila mmoja, hivyo kuruhusu kundi la watu waivuruge ni kuuza amani ya watanzania.
Alisema maelfu ya sungusungu hao, wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, Vitongoji, Vijiji, Kata na wilaya waliohudhuria kwenye mkutano huo wa kupinga siasa za uchochezi zinazoweza kuvunja amani ya nchi, ni ishara kwamba wana Kwimba wanataka amani siyo mambo ya Tunisa au Libya .
Sungusungu hao wakiongozwa na Mteni wa Tarafa ya Ibindo Shimbi Mogani, wakiimba nyimbo za kusisitiza amani kwa lugha ya kisukuma,walisema uchaguzi umekwisha wana Kwimba wanachapa kazi na kusomesha watoto kuondoa umaskini na ujinga, waachiwe amani waliyozoea.
Waliimba "Obebe Slaa nelechama lyako mle bayojase." Yaani wewe Dk.Slaa na chama chako ni wachonganishi na kuwaasa wananchi wasiwape nafasi ya kuchochea vurugu na pia kumtaka Mtemi wao (Kangoye) achukue hatua kama serikali wilayani mwake wanapotokea wachochezi.
Awali mkutanao huo ulitanguliwa na maombi ya sala kuiombea nchi iwe na amani na kuepuka vurugu kama za Misri, Tunisia na Libta, kabla ya jeshi hilo kutoa heshina na nasaha hizo.
Waliotoa maombi hayo ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Kwimba Sad Seif(BAKWATA) na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa wilayani humo, Mchungaji Samuel Makima (AICT Kwimba) ambao walisema kuwa uchaguzi ulisha isha viongozi wakapatikana hivyo wajibu wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.
wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.

Mgambo wakiimba wimbo maalum kwa kilugha wenye ujumbe wa kukomesha maandamo yanoyafanywa na Chama cha CHADEMA.

Maandamano yenyewe yako wapi hapo? Mbona tunaona sungusungu ambao wamelazimishwa kuvaa kiyangayanga na kisimbasimba, au kulikuwa na pambano la wapenzi wa timu za watani wa jadi wa eneo hilo na huyo "mkuu wa wilaya" alikuwa mgeni rasmi.
 
Baadhi ya viongozi wa serikali walikuwa wanapinga maandamano kuwa yanawapotezea wananchi muda wa kufanya kazi na kujiingizia kipato chao. Sasa iweje tena kiongozi wa serikali wilayani afanye kilekile ambacho mabosi wake wanakandya?

Huyo DC hana lolote zaidi ya kujipendekeza huku akijua kuwa mwezi Mei viongozi wa mikoa na wilaya watateuliwa (Kwa mujibu wa Mh. Pinda). Na hao Sungusungu wataendelea kuchezewa akili zao wakati wenzao wakijineemesha kwa ufisadi kwenye miradi ya wakulima.
 
hahaaa!! wanafuraisha kweli yani pamoja na umaskini mkubwa walionao bado wanakubali kudanganya kiraisi na kibaraka wa ccm(mkuu wa wilaya) kweli kazi ya ukombozi ni ngumu sana but tutapambana mpaka pumzi ya mwisho.

Mkuu wa wilaya kapata ajira kwa kupigiwa simu na katibu mkuu Luhanjo!=kazi isiyohitaji elimu. Wanamgambo vijana wenye mateso makubwa kwa kukosa elimu leo wamedanganywa na pilau na tisheti ili wapige picha na kutoa tamko. Mungu saidia Afrika na makaburu weusi ambao ni wabaya kuliko wale wa Afrika ya kusini maana hawa wanaua huku wanacheka
 
Sungusungu anajipa mamlaka yasiyokuwa yake. Kazi kweli kweli...huyu DC kukagua kundi la sungusungu amejiona amekuwa raisi.
 
Huyu mkuu wa wilaya kwimba, Kangoye 2005 aligombea jimbo la Tarime na chacha akamgalagaza , kikwe akaona ampe ulaji. Kweli ipo kazi.
 
SERIKALI wilayani Kwimba imesema kwamba, itawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wanasiasa watakaotumia majukwa kuitukana, kufanya uchochezi na kuhatarisha amani.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kupinga maandamano ya uchochezi, hivi karibuni mjini Ngudu, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Christopher Kangoye alisema wanasiasa ‘uchwara’ wasiifanye Kwimba uwanja wa kupangia vurugu na uchochezi.
Kangoye ambaye ni Mtemi wa jeshi la jadi la wilaya hiyo (Sungusungu) alisema hayo baada ya kupokea heshima na salamu za askari zaidi ya 2,000 wa jeshi hilo , waliodai kwamba wamechoshwa maandamaono na mikutano ya uchochezi ya wanasiasa.
“Tutawakamata wanasiasa wanaodai wanakuja kufanya mikutano kwa nia nzuri kisha wanatumia fursa hiyo kufanya uchochezi, kumtukana Rais na Serikali, Kwimba siyo uwanja wa kupangia uchochezi,” alisema Mkuu huyo wa wilaya.

Alieleza kwamba nchi yetu imejengwa kwa misingi imara ya demokrasia, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa ambao unapaswa kulindwa kwa nguvu yote na kila mmoja, hivyo kuruhusu kundi la watu waivuruge ni kuuza amani ya watanzania.
Alisema maelfu ya sungusungu hao, wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, Vitongoji, Vijiji, Kata na wilaya waliohudhuria kwenye mkutano huo wa kupinga siasa za uchochezi zinazoweza kuvunja amani ya nchi, ni ishara kwamba wana Kwimba wanataka amani siyo mambo ya Tunisa au Libya .
Sungusungu hao wakiongozwa na Mteni wa Tarafa ya Ibindo Shimbi Mogani, wakiimba nyimbo za kusisitiza amani kwa lugha ya kisukuma,walisema uchaguzi umekwisha wana Kwimba wanachapa kazi na kusomesha watoto kuondoa umaskini na ujinga, waachiwe amani waliyozoea.
Waliimba “Obebe Slaa nelechama lyako mle bayojase.” Yaani wewe Dk.Slaa na chama chako ni wachonganishi na kuwaasa wananchi wasiwape nafasi ya kuchochea vurugu na pia kumtaka Mtemi wao (Kangoye) achukue hatua kama serikali wilayani mwake wanapotokea wachochezi.
Awali mkutanao huo ulitanguliwa na maombi ya sala kuiombea nchi iwe na amani na kuepuka vurugu kama za Misri, Tunisia na Libta, kabla ya jeshi hilo kutoa heshina na nasaha hizo.
Waliotoa maombi hayo ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Kwimba Sad Seif(BAKWATA) na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa wilayani humo, Mchungaji Samuel Makima (AICT Kwimba) ambao walisema kuwa uchaguzi ulisha isha viongozi wakapatikana hivyo wajibu wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.
wa kila mmoja ni kutii mamlaka ya serikali.

Mgambo wakiimba wimbo maalum kwa kilugha wenye ujumbe wa kukomesha maandamo yanoyafanywa na Chama cha CHADEMA.

Usipotoshe watu hapo hakuna maandamano kuna kikundi chawanaccm wachache ushaidi umeweka mwenyewe
 
Maskini ndugu zangu wasukuma,sijui wataamka lini.Uduni wa fikra,elimu na kujitambua?....,mwenzao anapalilia unga wake.Haya bwana....
 
Umaskini sio kukosa mali tu. Hata ukiwa na fikra potofu wewe ni maskini wa kutupwa
Mimi naona hawa CCM sasa wanachanganyikiwa! Tangu lini hao sungusungu wana madaraka ya kukamata wanasiasa? Wao wakifanya hivyo polisi watafanya kazi gani?Kama kila chama makada wake wasiporidhika wakipewa jukumu la kukamata wapinzani wao patatosha hapa kwetu?
Kwa taarifa yenu Dr Slaa atakuja huko muda si mrefu na atahutubu kama kawa halafu jaribuni kumkamata muone moto wake!
 
hahaaa!! wanafuraisha kweli yani pamoja na umaskini mkubwa walionao bado wanakubali kudanganya kiraisi na kibaraka wa ccm(mkuu wa wilaya) kweli kazi ya ukombozi ni ngumu sana but tutapambana mpaka pumzi ya mwisho.
Mambo ni kupata fulana za njano at zero cost, at the expense ya kupofushwa daima, kweli inasikitisha
 
Back
Top Bottom