DAWASA na ubambikiaji wa bili za maji

bugzbunny

JF-Expert Member
Mar 9, 2013
838
748
Katika siku za karibuni mashirika yanayojiendesha yamekuwa katika mikakati ya kuhakikisha yanazalisha pesa kwa namna yoyote Ile ili mradi wapate kujiongezea stahiki na mambo mengine, sasa katika harakati hizi ni DAWASA.

DAWASA imekuwa ikilalamikiwa na wateja wengi sana kuhusu bili za maji kupanda ghaflaghafla wakati matumizi ya mteja hayajabadilika Sana. Utakuta mtu kwa wastani bili yake ni shillingi elfu 10 kwa mwezi. Ghafla analetewa bili ya sh 60,000 yani mara sita ya matumizi yake ya kawaida.

Hii imeleta malalamiko mengi sana. Na ukimywa wa serikali inaonesha pengine imewatuma. Au kwa vile waliambiwa wajipandishie mishahara? Yani wasomaji mita wanarusha units makusudi kabisa.

Hili suala linaitaji mjadala mpana na solution. Ikiwezekana tuwe na mfumo Kama wa luku maana imezidi na ninajua ni wengi Sana wahanga wa hili suala.

Wamefikia sehemu mpaka wanazibambikia bili taasisi za serikali pia. Hili lisiposemwa itakuwa sio haki kwa Watanzania.
 
DAWASA wana madeni hatari. Ripoti yao ya 2019/20 walikua na 50% ya Unaccounted For Water (Maji ambayo wamechukua kutoka kwenye chanzo ila hayakauzwa labda yamevuja ktk leakage yameibwa etc).

Hii inaonesha miundombinu yao ipo vibaya saaana. Kuanzia kwenye miundombinu hadi Wafanyakazi.

Nadhani hii kitu ya bili kuja tofauti wanaijua sana sema ndio mbinu yao ya kucover madeni na waweze jilipa mamilion ya mishahara.
 
Wenye shillingi chimbeni makaro ya maji mvune maji ya mvua mpunguze adha hii.
 
Wana matatizo sana hawa ....
Screenshot_20210312-222146_Instagram.jpg
 
DAWASA wanawaibia sana wananchi, unakuta mtu bill yake average per month haizidi 12,000 sasa tokea Jan 2021,unakuta wanaleta bill hadi 50,000 yaani mara 4 hadi 5 zaidi, huu ni uwizi wa wazi na Mh. Waziri wa Maji yuko, na lazima hili tumwambie.. Huu ni uwizi, hasa Tabata Segerea, Bima, bill zinakuja mara 4 hadi 5 zaidi kwa mwezi, wakati maji wakati mwingine hakuna 10 days..
 
Aisee now i see the light... kila mwezi nalipa 30K na nakaa mwenyewe nyumbani na weekdayz nipo kazini!! Mpka nikajiuliza labda kuna mtu ana kiwanda halaf bomba kaconnect kwangu
 
Ila Tanga uwasa wako wazi nilipenda wanavyojali wateja. Wakija kukata maji Kama haupo hawakati Hadi wakusikilize.
 
Katika siku za karibuni mashirika yanayojiendesha yamekuwa katika mikakati ya kuhakikisha yanazalisha pesa kwa namna yoyote Ile ili mradi wapate kujiongezea stahiki na mambo mengine, sasa katika harakati hizi ni DAWASA.

DAWASA imekuwa ikilalamikiwa na wateja wengi sana kuhusu bili za maji kupanda ghaflaghafla wakati matumizi ya mteja hayajabadilika Sana. Utakuta mtu kwa wastani bili yake ni shillingi elfu 10 kwa mwezi. Ghafla analetewa bili ya sh 60,000 yani mara sita ya matumizi yake ya kawaida.

Hii imeleta malalamiko mengi sana. Na ukimywa wa serikali inaonesha pengine imewatuma. Au kwa vile waliambiwa wajipandishie mishahara? Yani wasomaji mita wanarusha units makusudi kabisa.

Hili suala linaitaji mjadala mpana na solution. Ikiwezekana tuwe na mfumo Kama wa luku maana imezidi na ninajua ni wengi Sana wahanga wa hili suala.

Wamefikia sehemu mpaka wanazibambikia bili taasisi za serikali pia. Hili lisiposemwa itakuwa sio haki kwa Watanzania.

Hii kitu moja ni watanzania wachache wanaojua kusoma mita za maji na pia huwa hatuna muda wa kuchunguza matumizi ya maji au umeme kwa kila mwezi kwa watanzania tulio wengi ndio maana wanafanya huu mchezo na pia hii itakuwa ni agizo tokea kwa uongozi wa @DAWASA kwani ukiwapelekea unit ulizotumia kwenye mfumo wa picha wanakubadilishia wala sio wakali wanakuambia tu ni shida ya msomaji.
Chengine kinawaponza ni kufikia malengo kwa lazima na kutoa gawio kwa serekali.

Mwisho hakikisha unasoma kila mara mita ya maji ili kujua ipo sawa au umezidishiwa bili zako
 
Jifunzeni kusoma Meter zenu, sio mnalalamika. Ukihisi bill ni kubwa kuliko matumizi yako, kagua Meter yako kujua kama inafanya kazi vizuri.
 
Hilo ni kwl kabisa mkuu,,,mimi anatumia unit 1 au 2 kwa mwezi,,

Lakini naletewa bili ya units 8.

Pumbavu zao kabisa Hawa.
 
Hilo ni kwl kabisa mkuu,,,mimi anatumia unit 1 au 2 kwa mwezi,,

Lakini naletewa bili ya units 8.

Pumbavu zao kabisa Hawa.
Tatizo mita zao zimefungwa kwa namna ambayo maji yakipita kidogo mita inakimbia kiasi ambacho kwa siku unajikuta mita ikisoma mamia ya lita kinyume na uhalisia. Kwa ufupi wanatuibia kupitia mita zao walizoongeza speed.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Nina tank ya 3000 lts..

Nikijaza hilo sihangaiki na kufunguwa bomba.

Na huwa silimalizi kwa mwezi mzima.

Ajabu wananipa 8 units kwa mwezi.
 
Kwani wakija wanasogeza mita yako kiujanja? Hawawezi kukuibia kama utaisona mita yako kila wakati! Mimi Kila wakileta bili ninalinganisha na mahesabu yangu naona sawa.

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom