BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,041
Mkuu Steve Dii unachosema ni kweli kabisa, lakini kungekuwa na utaratibu wa kuhakikisha viwango vya emissions level vinafuatwa nchini basi nina hakika baadhi ya magari nchini yasingeruhusiwa kuwepo barabarani na hivyo kupunguza msongamano huo wa magari japo kwa asilimia ndogo.
BAK, wazo la kuondoa magari kwasababu ya umri wake tu hata mimi sitoafikiana nalo. Siafikiani na wazo hilo maana roadworthy haitegemei umri wa gari; ni matunzo ya gari zaidi ndiyo huwa kigezo. Unaweza kuwa na gari la miaka minne lakini likawa linatoa moshi kuliko tairi la kuchoma kwenye maandamano! Lakini pia unawezakuwa na gari la miaka 12 ambalo limetunzwa na carbon emission yake ikawa chini sana. Hii inapelekea kukukumbushia moja ya jambo kwa wenzetu jinsi vile baadhi ya magari yaliyo 'antique' yanavyokuwa aghali kuliko mengi mapya.
Last edited by a moderator: