Dawa ya kuondoa msongamano Dar...

jiulize hili
asubuhi kuna foleni tegeta-mwenge-posta,kimara-ubungo-posta,gongolamboto-posta,mnyamala-kino-posta utafix vipi hii kwa kufix kariakoo??hawa wote wanaenda kariakoo???
na jioni kuna foleni posta-mwenge-tegeta,posta-ubungo-kimara,posta-mbagala na hii utafix kwa kufix kariakoo???

Nimesema Posta na Kariakoo
Posta nayo kama ulikuwa hujui iko kwenye Tarafa ya Kariakoo
so wengine tukisema Kariakoo ni tarafa nzima
au CBD yoote....iwe fixed
CBD ni Central business District kuanzia posta mpaka fire mpaka kamata
 
Nimesema Posta na Kariakoo
Posta nayo kama ulikuwa hujui iko kwenye Tarafa ya Kariakoo
so wengine tukisema Kariakoo ni tarafa nzima
au CBD yoote....iwe fixed
CBD ni Central business District kuanzia posta mpaka fire mpaka kamata


hii inaweza kusaidia kidogo.
 
The boss wazo lako sio baya sana ila mimi ninachoona tatizo la foleni ni tatizo la mipango miji ambalo kama utalitazama vizuri basi utaweza kubaini kuwepo kwa mgawanyo mbovu uliopo katika mgawanyo wa huduma za kijamii zilizopo jijini Dsm.Dsm kama ilivyo ina manispaa tatu(3)yaani Ilala,Temeke & Kinondoni na katika Manispaa hizi kiukubwa kwa eneo ni Temeke ikifuatiwa na Kinondoni na mwisho ni Ilala ndio ndogo kieneo kuliko zote.Cha ajabu huduma zote za kibiashara,maofisi ya Serikali,Hospitali kubwa,Soko kubwa la Kariakoo,Wizara nyingi kama si zote,ikulu,Airport, maduka yote makubwa,mahoteli yote makubwa,mahukumbi makubwa yote na nyinginezo nyingi zipo katika Manispaa ya ilala.Kuwepo kwa huduma hizi tu katika eneo moja tena dogo kieneo ukilinganisha na manispaa nyingine hilo ni tatizo kubwa.Nini kifanyike,kwanza ni kuhamisha huduma zote muhimu kubwa katika manispaa ya ilala na kwenda katika manispaa nyingine za kinondoni na temeke,huduma kama vile kuwepo kwa shopping malls kubwa zenye kuchukua maeneo makubwa mf.century city iliyopo cape town,kuwepo kwa masoko ya kariakoo mengine katika manispaa hizi mbili,baadhi ya ofisi za Serikali kubwa zinatakiwa kuhamishwa hapo mjini(uchambuzi ufanyike zipi zihamishwe na zipi zibaki) etc
Pia kuanzishwe huduma ya kutoza kodi kwa magari yanayoingia mjini,hii itapunguza baadhi ya magari kuingia mjini na bila kusahau watu wahimizwe kutumia public transport kama dbrt itakapoanza.huo ni mtizamo wangu
Mtizamo wako ni Mzuri sana lakini ni vigumu kutekelezeka Kama ilivyokuwa vigumu kuhamia Dodoma kumbuka siku ikitokea Muujiza Wakahamia Dodoma basi ujue kila kitu kitawezekana hapa Tz kwani hakuna Jambo gumu hapa Tz Kama kihamia Dodoma .
 
Suruhisho la msongamano Dsm ni kuhamia Dodoma tu wala si vinginevyo
 
Hili siyo suluhisho 100%, kwa sababu miundo mbinu ya barabara iliyopo Keko,Tandika,Pugu etc bado ni finyu kuweza ku-accomodate pilika za biashara ulizotaja,suluhisho la uhakika ni uwepo wa barabara za kisasa na serikali kufungua maeneo ya biashara mchanganyiko(siyo aina moja kama unavyoshauri) kwenye njia kuu zinazoingia Dar kutokea mikoani,ili wajipatie huduma zote muhimu huko huko pembezoni,

Suluhisho pekee ni kuhamia Dodomo tu.
 
sio dar tu mfano miji inayokua kwa kasi kama Arusha na Mwanza,ingekua ndio mifano ya kurekebisha miundo-mbinu ili ikidhi muongezeko wa watu na shughuli mbalimbali kwa kupanua miji sehemu mbalimbali...
sasa nenda uone hii miji inavojengwa ni kichefuchefu yani unajiuliza hivi ndo "wataalamu" kweli hawa?wanafanya kazi gani mana haiitaji degree ya uhandisi wala mipango miji kuona huo ujinga unaofanywa ktk miji hii

mitaro ni kero kubwa sana yani barabara ndogo kuliko mitaro iliyo pembeni yake tena wazi,mji wa Mwanza ni kichekesho!
wakati ni mji ambao tungekuwa tumeupanga ipasavo ni kitovu kizuri sana sana kwa east afrika na maziwa makuu kiuchumi na kijamii

ila kwa serikali hii ya sasa tusahau!!labda kije kizazi kipya kabisa:wave:
 
Kuhusu emission standards, ni kweli Tanzania hakuna utaratibu wa maana, zaidi wa ule wa kuongeza VAT na ushuru kwa magari yenye umri zaidi ya miaka 10.

Nasikia kuanzia mwezi huu umri umekuwa miaka 8?

Sababu itakuwa ni hiyo hiyo aka kupunguza emission?

Halafu ni nani alidesign hii kitu?
 
Back
Top Bottom