Darasa la saba waliopata maksi 60 nao kubebwa kwenda sekondari - Agizo la Kikwete

Swali: kama wa kwanza kapata 30%, nadhani 24% pays a lot!
Ikitokea hivyo basi ujue kuna kasoro kwenye utunzi wa mitihani au watahiniwa hawakuelewa kabisa walichokuwa wanafundishwa kwa miaka saba!,ambayo kimsingi itakuwa janga la kitaifa!
 
sasa umeona umuhimu wa jamiiforums eh!?
Nina wasiwasi usije ukawa wale wanaotokwa na mapovu kwa kuipiga vita huku wakiwa hawafanyi utafiti wowote

Wewe nshomile wacha matusi, sasa mambo ya povu yanatoka wapi! Kuipiga vita kunatoka wapi tena? Noija kujumangana, oli muziba si?
 
kwetu ni kawaida tu hata huyu yuko 'A' level.
S0298/0025
F
MWANAASHA JAKAYA KIKWETE
27
IV
CIV-D HIST-F GEO-D KISW-D ENGL-C LIT ENG-D BIO-C B/MATH-F COMM-F

na hata hiyo C ya Biology ni shule kuvujisha Practical. Like father, like daughter
 
Natetemeka, napata kigugumizi, na kuogopa sana! Tusubiri ule mtihani wa ziada (supplementary) utaofanywa mwezi wa pili baada ya Waalimu watakapolalama kwa kupelekewa ziro.
Je umewahi kusikia watahiniwa waliofaulu kupewa mitihani wa pili wa Taifa kwa nyakati mfululizo ili kupima KKK?
Matokeo yake zaidi ya 5,000 hawakuumudu. Sijui wale waliokuwa wamefeli walikuwa na hali gani.
 
Bila kuwekeza ipasanyo katika Hisabati tusitegemee mabadiliko yoyote ya maana kwa vijana wetu. Pia tunahitaji kuwa na Mkakati wa Kitaifa kwa kila somo kuanzia Msingi mpaka Sekondari.
 
Kwa kweli mimi ni mwalimu na kubwa ni kuwa wanafunzi wa sasa ni waoga hata kuongea kidogo anachojua ni vigumu. Ila la msingi mfumo wa elimu ni mbovu wote kwa sababu zinazojulikana kubwa likiwa ni siasa chafu kwa elimu yetu hii. Tusipo weka tume huru ya elimu, du itakuwa madudu heri ya mwaka huu. Subirini ya mwakani kwani walimu wamechoka na wapo tayari kwa ufumbuzi. Kodi za watanzania zinatumika ndivyo sivyo katika hili. Wazazi wenyewe hawajui nini maana ya elimu sembuse matokeo hayo mabovu? Moto wanaujua walimu na wasomi wengine.
 
unazani mshahara wa mwalimu graduate 437000. na diploma 335000, hii ni utani na watoto wataendelea kufeli mpaka kikwete. arudi mezani na walimu na kuwajari kama na wenyewe ni wafanyakazi
 
Jamani hawa watoto wanayasubiri kwa hamu sana. Naomba kama inajulikana kiuhakika basi ndio isemwe
 
Hizi ndizo athari za kuwa na Rais anayepuuzia kila jambo. Wapeleke hata waliopata 20/250 kwani lengo lao si kujaza mikondo tu?
 
Waache waje sec.wote watoondoka na ''0''.WEalimu msiogopeshwe,msiangaike na wajinga la sivyo JK aje afundishe aone ugumu wa kufundisha tena mwanafunzi ambae hakushinda!!!!!!.Ongeza mshahara nma marupurupu mazuri utaona matokeo yake.Wazazi/Walezi chukua hatua kama JK ameshindwa.2015 NI M4C.
 
Hili ni pigo kwa Taifa ya serikali tawala ya Jakaya Mrisho Kikwete!

Hili halikubaliki hata kidogo!

Ndiyo faida (MATUNDA) ya serikali legelege ya ccm! Kilichopandwa ndicho kitakachovunwa!

Sasa wewe unatoa ushauri gani? Au hali hii imekufurahisha sana.
 
Ni kweli performance ya vijijini ni poor kwa sababu karibu muda wote wanafunzi wanatumikishwa na walimu. Ajira ya watoto bila malipo.
 
Back
Top Bottom