KERO Dar: Hali ya Barabara ya Mbezi Juu Makonde kuelekea Baraza la Taifa la Mitihani ni masikitiko makubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hali ya barabara ya kuelekea Baraza la Mitihani kupitia Makonde, Mbezi Juu, Dar es Salaam inasikitisha sana na nashindwa kuelewa Serikali inawaza nini kiasi cha kushindwa kabisa kuirekebisha hii barabara na hata kuiwekea lami ukizingatia inaelekea kwenye moja ya Taasisi zake kubwa kabisa

photo_12_2024-01-23_13-00-21.jpg
photo_10_2024-01-23_13-00-21.jpg
photo_9_2024-01-23_13-00-21.jpg


Hali ya barabara hii sio adha tu kwa Watu au Wageni wanaoenda Baraza la Mitihani bali hata kwa sisi Watumiaji wa kila siku ambao ni wa tumiaji wa barabara hii mara kwa mara. Hapa imeharibika na bado inaendelea kuharibika na mara kwa mara hali huwa hivi hivi hadi wananchi tunajichanga na kuziba viraka kwa magunia ya mchanga. Serikali ione aibu kubwa sana kuwa na Taasisi kubwa kama hii lakini hii ndio njia ya kupita kwenda kwenye ofisi hizo

photo_5_2024-01-23_13-00-21.jpg
photo_6_2024-01-23_13-00-21.jpg
photo_7_2024-01-23_13-00-21.jpg


Kwa kweli inakuwa ni Mtihani kufika Baraza la Mitihani. Ikumbukwe barabara hii inaenda kuungana na barabara ya lami inayotoka Mbezi Shule hadi Mbezi Mwisho kwa kupitia Goba
 
Back
Top Bottom