Barabara ya Kerai, Mbezi Jogoo ni korofi miaka na mikaka. TARURA kwanini hamuiboreshi?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Barabara hii inayoanzia Mbezi Jogoo karibu na kituo cha daladala na kwenda kuungana na ya Mbezi Makonde ina umuhimu sana kwa sasa kwa sababu inapita maeneo yenye huduma za kijamii kama Zahanati ya Ndumbwi ambapo sasa imepanda hadhi hadi kutoa huduma ya kujifungua kwa wajawazito. Pia kuna shule ya msingi Ndumbwi.

Hii kutokana na asili yake kuwa ya mteremko kama unashuka kuelekea barabara kuu ya Bagamoyo, chanzo kikubwa cha uharibifu wa barabara hiyo ni maji ambayo hayakuwekewa njia maalum hiyo kupelekea kujitafutia njia zisizo rasmi hivyo kuharibu barabara hiyo kwa kiasi kikubwa. Naamini barabara hiyo ingejengwa kwa kiwango kinachokubalika na kuwa na mitaro inayojiweza, basi isingekuwa korofi sana.

Nailaumu TARURA kwa sababu naona kama kuna uzembe unafanyika kutokana na kuwepo kwa kampuni ya ujenzi ya Kerai ambayo imekuwa ikijitolea kurekebisha barabara hiyo pindi inapoharibika ili iwe rahisi kupitisha magari yake makubwa ya ujenzi. Pamoja na msaada huo, kampuni hiyo imekuwa ikifanyia matengenezo ya kawaida tu ambayo si suluhisho la kudumu, hivyo tatizo kubaki palepale.

Hata njia ya kuingia barabara hiyo kutoka barabara kuu ni korofi sana kutokana kuwa na mashimo yasiyotengenezwa. Ila upande wa pili Art gallery, TARURA waliweka lami hadi nyumbani kwa Balozi Mulamula siku chache tu baada ya kuteuliwa kuwa Waziri. Huu kwetu ulikuwa ni ubinafsi uliopitiliza.

Nisiandike mengi.

1.png
2.jpg
3.jpg
4.jpg
5.jpg
6.jpg
 
Back
Top Bottom