Danish PhD student on Nyerere and "Vijiji vya Ujamaa"

AshaDii,

Sasa hivi wapo watanzania wanaoshiriki katika kazi mbalimbali za kitaalamu katika nchi mbalimbali. Katika kushiriki kwao wanajifunza best practise. Hili kujifunza best practise hizi, tunaona wenzetu wanakosoa mambo yao ya zamani. Hivyo kila siku wanaboresha capabilities zao.

Kwa ujumla hakuna Achievement yoyote ya vijiji vya Ujamaa. Maendeleo katika vijiji vya Tanzania hayana tofauti au yapo nyuma kuliko nchi zingine ambazo hazikuwa na sera ya vijiji hivyo. Hapa chini ni maneno ya mwalimu kuhusu hivyo vijiji. Ukiangalia maneno aliyosema hayakutimia. Hivyo mafanikio yapo kwenye zoezi la kuhamisha watu. Lakini sio ujamaa wenyewe.

" Our agricultural organization would be predominantly that of cooperative living and working for the good of all. This means that most of our farming would be done by groups of people who live as a community and work as a community. They would live together in a village; they would farm together; market together, and undertake the provision of local services and small local requirements as a community Their community would be the traditional family group, or any other group of people living according to Ujamaa principles, large enough to take account of modern methods and the 20th century needs of man." [Nyerere, 1967]

Hivi umesikia hivi vinavyoitwa SACCOS kwenye vijiji; umesikia jinsi wana vijiji siku hizi wanavyoshirikishwa katika maamuzi ya vijiji vyao na jinsi wanavyoamua matumizi ya ardhi yao?
 
Hivi umesikia hivi vinavyoitwa SACCOS kwenye vijiji; umesikia jinsi wana vijiji siku hizi wanavyoshirikishwa katika maamuzi ya vijiji vyao na jinsi wanavyoamua matumizi ya ardhi yao?

Poor you,

Saccos ya kijiji ni paradox ya kijinga; wanachama wa saccos kwa kijj cha watu 2000 hawazidi watu 20...

Vijiji si sababu ya kuwepo kwa saccos
 
Zakumi heshima mbele! Naomba unisaidie hili,umesema akina Mwl Nyerere walipelekwa kwenye Vijiji vilivyofanikiwa tu kule China je kwa udhibitisho gani mkuu wangu au ndio zile literature za ma capitalist? Lakini pia kuna tatizo gani akina Mwl Nyerere kujifunza mafanikio ya ujamaa na kutumia mbinu hizo hizo hapa Tz? Zakumi,nina wasiwasi umesoma sana propaganda za ma capitalist na mtiririko wako naona kama wa huyo mwanafunzi wa PHD! Asante kwa changamoto unayoitoa hapa nazidi kujifunza kutoka kwenu!

Mtazamo,

WaChina walifanya strategy ya kutuvuta kwenye kambi yao bila sisi kujijua na walifanikiwa. Unaweza kunieleza sababu ya waChina kujenga reli ya Tazara?

Kuhusiana na mimi kutumia propaganda za capitalist, hakuna ubaya wowote hule. Ni upanuzi wa political spectrum. Kwa sababu kinachozunguzwa cha kunipinga mimi ni propaganda za kicommunism.

Mtanzania halisi hafungamani na siasa yoyote hile. Anatakiwa kusikiliza pande zote zile.
 
Ndio hapo ambapo weaknesses zake haziwezi kukosa.... Wakati hili la Ujamaa linakua Introduced Mwalimu aliliongelea kwenye hotuba zake for as much as sikuwepo ni evident (Toka hio declaration ya Arusha; the document also empasised on self-relience as a strategy of national development; the community became the focal point for socio-economic development in the country side na hivo ikitegemewa itagusa Tanzania nzima at Par). Take note in writings inasemekana hadi miaka ya early 1970 Ujamaa Village zili develop taratibu sana.... Ila baada ya hio Act ndio ilipelekea kukua kwa hizo villages hivo kwa upande fulani mafanikio....

Haya basi NDIO wananchi waliambiwa ila elimu on Ujamaa na self reliance ilikua sio ya kukidhi ama niseme kutosha. Kumbuka kua Mwalimu alikua ana delegate tu.... Being the man he was na nia yake ya Ujamaa siamini kua alikua anakua na details zote za hilo zoezi linavoenda. Nakumbuka niliwahi soma on matatizo ya Ujamaa kuna mahala ulitolewa mfano kua watu wa Tabora na Dodoma waliharibiwa makazi yao na kuachwa hawana pa kujihifadhi bali chini ya miti.... Tukubali kua pale tu ilipopitishwa kua "Act" ndio pale tayari "Ujamaa" ulienda na kua Implemented tofauti na the way it was intended.

Alafu bana huo mfano wa ng'ombe kumlazimisha kunywa maji sio kabisaaa.....lol. Sema kumlazimisha baby kunywa uji kwa kumkaba... anaona wamtesa kumbe as a Mother have good intentions at heart... lol
Kumbe lengo lilikuwa ni kuanzisha tu vijiji bila kutilia maanani eneo unaloanzisha kijiji?

Nilidhani waliangalia facts kama locations ie zenye uwezo wa irrigation pamoja na rutuba?

Kama umemsoma Skinner, kwenye behaviorism, utaelewa ni wapi tuliyumba.
 
Naona kuna festival. Nikizuka sehemu kama hizo mnaweza kunipiga mawe.

Mbona Mzee wa Utandawazi, Ubinafsishaji na Uwekezaji, Mkapa atakuwepo tena miongoni mwa wanamdahalo:

In the afternoon, we will have a conversation on ‘Hali ya Dunia ilivyo leo na Mustakabali wa Afrika' (The World Situation today and the Future of Africa). The chief participants in the conversation are: Mhe. Benjamin Mkapa (in his capacity as the Chairman of the South Centre), Professor Issa Shivji and Dr. Ng'wanza Kamata.
 
Watanzania ,napenda sana kuzungumza mambo ya Africa. Hakuna siku watasema The World Situation today and the Future of Tanzania.
 
Watanzania ,napenda sana kuzungumza mambo ya Africa. Hakuna siku watasema The World Situation today and the Future of Tanzania.

Una uhakika? Huo ni mkutano wa Wamajumui wa Afrika ndio maana inabidi iwe hivyo. Makongamano ya Tanzania tumeshayafanya mengi. Wewe beba tu maboksi unakosa mambo.
 
Una uhakika? Huo ni mkutano wa Wamajumui wa Afrika ndio maana inabidi iwe hivyo. Makongamano ya Tanzania tumeshayafanya mengi. Wewe beba tu maboksi unakosa mambo.

Kwikwikwi. Mabox matamu mkuu. Unawachia Obama anafanya vitu vyake. Na yeye anakuachia unafanya vyako. Pure division of labor kama Adama Smith alivyosema.

Bongo Prof akitoka lecture anawahi kwenye banda la kuku.
 
Kuna mdau kanitumia hii sasa sijui kama ni kweli au ni longolongo:

Ni ajabu. Kwa kweli, mimi kila maktaba niliyowahi kukumbana nayo nilikuta hazina kubwa ya vitu vinavyozungumzia Ujamaa/Nyerere/Tanzania - kwa kweli kuliko kiti kingine chochote ninachokijua Afrika. Mpaka virtual libraries. Hakuna jambo lililofanyiwa utafiti mkubwa barani Afrika kaa Ujamaa wa Tanzania. Kwa maandishi ya kibiashara labda Kenya inaweza kushinda, ama ya kishabiki Mandela anaweza kushinda, lakini kwa ya kianazuoni, kwa kweli hakuna. Hakuna.
 
  • Thanks
Reactions: DSN

Ulifanyiwa utafiti si kwa sababu kila mtu aliweza. Nyerere si kazi zake zilikuwa zinatoka kichwani bila kuwa na references.
 
Kipindi nipo college nilikuwa nashangaa vibabu vya miaka 70 kinakuja library ya chuo kuazima vitabu anaenda nanvyo home kusoma. Bongo library ya UDSM kama sio mwanachuo kwanza hutakiwi!

Nazungumzia swala zima la kuhamasisha watu wasome japo hivyo vichache vilivyopo pale.
 
.

Alafu bana huo mfano wa ng'ombe kumlazimisha kunywa maji sio kabisaaa.....lol. Sema kumlazimisha baby kunywa uji kwa kumkaba... anaona wamtesa kumbe as a Mother have good intentions at heart... lol

Nimekulia kwenye mfumo wa Kicapitalist kila kitu kipo basi nikapelekwa kijijini kujua nyumbani kwetu kwa asili wewe si utani hiyo style ya kumpa mtoto uji kwa kumziba pua ilikuwa inanikera zingatia nilikuwa mtoto basi natamani kuwachapa makofi ndugu zangu hao.Wakainza hizo kazi zao za kumnywesha uji huyo ndugu yangu mchanga basi pua inabanwa mpaka mwingine anakuja kuminya miguu basi mtoto anafurukuta kama anaitaka kupoteza uhai.Na kweli hawajui tu kama binafsi najua walikuwa wanampa chakula ambacho ni kitu muhimu kwa maisha yake lakini kwa kumziba mdomo da ilikuwa inanifanya mwili wangi kusisimka n kujisikia vibaya.Kwa kuwa uko nilikotoka nimezaliwa na kukuta chupa ya maziwa nyonyo ndio jibu la kumkuza mtoto na ukilia unapewa nyonyo ya mkono [jig] unaangaika nayo kweye kitanda chako unajikuta umelala.

Hivyo utekelezaji wa shughuli nzima ya vijiji vya ujamaa ulikuwa ni muhimu lakini usimamizi wake ndio kama hivyo wajomba na mashangazi zangu wanavyowanyeshwa uji watoto wao,
 
Nadhani suali tunalopaswa kujiuliza laymen style ni kama huu mtindo wa sasa wa kuchukua ardhi iliyokuwa inamilikiwa na Watanzania na kupewa raia wa nje eti ni mwekezaji ndio utakaotusaidia Watanzania kujikwamua kiuchumi.

Migogoro ya ardhi inayosikika hivi sasa Arumeru. Mbarali, na hivi karibuni itasikika tena Sumbawanga baada ya Agrisol kupewa ardhi ya bure, ni matunda ya uongozi wetu kutupilia mbali vision ya Julius Nyerere. Hata badala ya kusahihisha pale Nyerere alipokosea, tunajitahidi kufuta kila kitu alichosimamia, hata kama kilikuwa na maslahi kwa Watanzania wote.
kwa kiasi fulani huwa nikitafakari juu ya sera za Mwalimu Nyerere pia najisikia kuzichukia lakini huwa nakumbuka kitu kimoja juu ya dawa ya maralia, Chloroquine. Hii dawa ni chungu sana na inanywewa kwa tembe 4,4 then 2, lakini ilikuwa inatibu maralia!

Hivyo huwa najiridhisha kuwa Mwalimu aliona ukweli huo japo 'wagonjwa' (watz) tuliangalia tu kwenye uchung wa dawa badala ya kuangalia athari za ugonjwa wenyewe.

Jaribu kutafakari juu ya mchoro huu unaoelezea athari za ubepari alioukataa Mwalimu na hali halisi ilivyo. Badala ya kukaa na kutulia inabidi tufikiri kwa kina. Nafikiri hii inatoa mwanga wa jibu la hapo kwenye red.
capitalism.jpg

View attachment 50379

Lukindo,

Kwa hiyo nikiwa na ufumbuzi wa matatizo na uwezo, nina uhalali wa kulazimisha watu mawazo yangu? Ni afadhari Ujamaa ulidondoka yeye mwenyewe akiwa madarakani. Hii imeonyesha kuwa mawazo ya binadamu bado ni ya binadamu hata kama yana uzuri ndani yake.

Masikini wa Tanzania hata kama ana matatizo anayo haki ya kujiamulia mambo yake. Na ujamaa ulikuwa unawanyima hizo haki.
 
Back
Top Bottom