Danish PhD student on Nyerere and "Vijiji vya Ujamaa"

Nimekulia kwenye mfumo wa Kicapitalist kila kitu kipo basi nikapelekwa kijijini kujua nyumbani kwetu kwa asili wewe si utani hiyo style ya kumpa mtoto uji kwa kumziba pua ilikuwa inanikera zingatia nilikuwa mtoto basi natamani kuwachapa makofi ndugu zangu hao.Wakainza hizo kazi zao za kumnywesha uji huyo ndugu yangu mchanga basi pua inabanwa mpaka mwingine anakuja kuminya miguu basi mtoto anafurukuta kama anaitaka kupoteza uhai.Na kweli hawajui tu kama binafsi najua walikuwa wanampa chakula ambacho ni kitu muhimu kwa maisha yake lakini kwa kumziba mdomo da ilikuwa inanifanya mwili wangi kusisimka n kujisikia vibaya.Kwa kuwa uko nilikotoka nimezaliwa na kukuta chupa ya maziwa nyonyo ndio jibu la kumkuza mtoto na ukilia unapewa nyonyo ya mkono [jig] unaangaika nayo kweye kitanda chako unajikuta umelala.

Hivyo utekelezaji wa shughuli nzima ya vijiji vya ujamaa ulikuwa ni muhimu lakini usimamizi wake ndio kama hivyo wajomba na mashangazi zangu wanavyowanyeshwa uji watoto wao,
Hilo la mtoto sikujuwa na mimi hadi nilipotoka nje ya nchi.

Nakumbuka kuna dada mwingereza ambaye alikuja for volunteering kwenye moja ya shule nilizosoma, so wakati anamalizia, nilimwalika nyumbani.

Na sister wangu alikuwepo kipindi hicho kutembelea akiwa na mtoto wake mdogo.(a year old or so)

Hapo pa kunyweshwa uji palimshangaza sana mgeni, alikuwa so unconmfortable hadi nikajuwa, lakini nikawa najisemea tu hii ni culture yetu na siwezi kushangazwa na jambo lolote la yeye kushangazwa kuhusu cultures zetu.

Ukweli baada ya kusafiri zaidi nimeona kuwa kuna njia nyingi tu za kufanya hivyo.Na hata nilisafiri na kukutana naye uingereza, kwa mbali nilikumbuka na kujisemea kweli ilikuwa aibu!

Na pia mtoto kumlazimishia hivyo na kumbana puwa, tunaona ni kawaida lakini hilo pia linamwathiri sana mtoto kwenye makuzi yake,mtoto kwa lazima anakuwa impacted psychologicaly, na mambo kama hayo huwa eventualy yana shape personality ya individuals na behaviors kwa ujumla.

@Asha Dii, when the need for water arrives (thirstiness), the cow will drink it!lol
 
Bado kuna nyingine inatoka gazetini nadhani Ijumaa hii, kuna mwandishi/mwanasafu kakasirika sana - ikiipuliwa jikoni itawekwa hapa!

Mnakasirika na nini? Afu inakaaje mtu aandike vitu vya maana akiwa amekasirika? Ndio maana mambo yenu mengine yataishia kwenye mitandao tu.
 
Nimeona kwenye blog yako. Inaonekana mna-mind wasomi kufuatilia Nkwame na sio Nyerere. Mnaanza kuleta wivu na hasira.

poa ila huyo mwandishi anayotoea makala ijumaa anampinga nyerere kwa mengi tu, ameshaandika makala nyingi tu kupinga sera zake hasa za elimu (kumbuka hapa suala sio kupinga au kutupinga vijiji vya ujamaa, suala ni methodolojia za utafiti na hitimisho kuhusu rejea zinazohusu dola ya nyerere enzi za azimio la arusha).
 
Tuko kwenye side show sasa. Suala la hapa tumeshahitimisha. By the way kwanini Kenya wanamisingi mizuri ya uchumi bila kuwa na longolongo za Ujamaa?
 
Hilo la mtoto sikujuwa na mimi hadi nilipotoka nje ya nchi.

Nakumbuka kuna dada mwingereza ambaye alikuja for volunteering kwenye moja ya shule nilizosoma, so wakati anamalizia, nilimwalika nyumbani.

Na sister wangu alikuwepo kipindi hicho kutembelea akiwa na mtoto wake mdogo.(a year old or so)

Hapo pa kunyweshwa uji palimshangaza sana mgeni, alikuwa so unconmfortable hadi nikajuwa, lakini nikawa najisemea tu hii ni culture yetu na siwezi kushangazwa na jambo lolote la yeye kushangazwa kuhusu cultures zetu.

Ukweli baada ya kusafiri zaidi nimeona kuwa kuna njia nyingi tu za kufanya hivyo.Na hata nilisafiri na kukutana naye uingereza, kwa mbali nilikumbuka na kujisemea kweli ilikuwa aibu!

Na pia mtoto kumlazimishia hivyo na kumbana puwa, tunaona ni kawaida lakini hilo pia linamwathiri sana mtoto kwenye makuzi yake,mtoto kwa lazima anakuwa impacted psychologicaly, na mambo kama hayo huwa eventualy yana shape personality ya individuals na behaviors kwa ujumla.

@Asha Dii, when the need for water arrives (thirstiness), the cow will drink it!lol
Unajua mkuu wangu yale makuzi sii ya Kibepari wala kijamaa bali ni Umaskini. Mtoto anabanwa pua kunywa Uji kwa sababu mtu aliyebanwa pua akilishwa hawezi kujitapisha, ni sayansi ya mwafrika ambayo ilifanya kazi japokuwa itatafsirika kama abuse. Mtoto alilazimishwa kunywa uji kwa sababu pia ndio chakula pekee wazazi waliweza ku afford na provide maana maziwa deal kubwa sana..na mtoto asipoupenda uji kazi mpya ya kumnywesha kwa nguvu inakuja tofauti na wewe uliyekulia Ulaya unaweza kutafuta ni kitu gani mwanao anakipenda kula au kunywa.

Ni katika makuzi hayo sisi tulozaliwa vijijini hatuna kuchagua chakula, wala hizo allergies hatukukua nazo.. nasi tunawashangaa watoto wa frigi open wanapougua kwa kunywa Uji wa karanga au hata vumbi. Tumekuzwa ktk mazingira ambayo yalitujenga Ungangari, mwili wetu umeweza kuvumilia magumu kama kunywesha uji wakati pua zimezibwa. Ndivyo Vijiji vya Ujamaa wakati sisi tulilazimishwa hawa wenzetu wanaanzisha makazi mapya kwa kupima ramani na kugawa ardhi utaona watu wanahamia wenyewe.. Sisi tulianzisha Dodoma miaka 30 ilitopita lakini hadi leo inasemekana yalikuwa makosa makubwa..
 
Tuko kwenye side show sasa. Suala la hapa tumeshahitimisha. By the way kwanini Kenya wanamisingi mizuri ya uchumi bila kuwa na longolongo za Ujamaa?

misingi ipi hiyo? hebu iorodheshe kwanza!kisha itolee maelezo.
 
Nimeona sehemu hapo juu, mwalimu said "in my report to the 1973 TANU conference I was able to say that 2,2028,164 people were living in village.two years later,in june 1975 I reported to the next TANU conference that approximately 9,100,0 00 people living together in 7,684 villages" na shivji amesema this is a tremendous achievement.
Lakini shivji hapo mwanzo kaandika "villagisation was a means of accelerating development and facilitating provision of health,education,water and other social services..
Swali ni, hilo lengo la services lilifanikiwa kwa kiasi gani? Au watu huko walitaabika zaidi..
Mwalimu alijisifu kwenye kiwango/idadi ya watu waliofanikiwa kuhama kwenda kwenye hivyo vijiji,lakini sioni mafanikio katika services yakitajwa na mwalimu katika andiko la prof.shivji..
 
Dear colleagues, i hardly comment in these blogs but with this topic i feel obliged to do so. I feel so pity for this Danish PhD student who tries to claim knowing much not only about Tanzania but Mwalimu with his vision and mission.

To be honest, no Tanzanian will claim to be so let alone the so called researchers from outside who will only stay for a limited number of time in the country, actually spending most of it travelling around. This is what we always feel and face for those who are in the diaspora especially studying at various Universities, so much claims about what is going in Africa and Tanzania in this case.

I sometimes wonder if we can have a policy through COSTECH that all research that is being done in Tanzania, its results should be communicated back or at least having the copies at the National library. It is only in this way that we come to learn what 'they' write about us. As for the Ujamaa policy, yes alot is written and said, unfortunately, there is a split, some are for and others against.

Imagine what would the western researchers write or at least those who took or take their studies in the western universities, being supervised by the western professors.

I concur to have the policy in place if it is not there.
 
Unajua mkuu wangu yale makuzi sii ya Kibepari wala kijamaa bali ni Umaskini. Mtoto anabanwa pua kunywa Uji kwa sababu mtu aliyebanwa pua akilishwa hawezi kujitapisha, ni sayansi ya mwafrika ambayo ilifanya kazi japokuwa itatafsirika kama abuse. Mtoto alilazimishwa kunywa uji kwa sababu pia ndio chakula pekee wazazi waliweza ku afford na provide maana maziwa deal kubwa sana..na mtoto asipoupenda uji kazi mpya ya kumnywesha kwa nguvu inakuja tofauti na wewe uliyekulia Ulaya unaweza kutafuta ni kitu gani mwanao anakipenda kula au kunywa.

Ni katika makuzi hayo sisi tulozaliwa vijijini hatuna kuchagua chakula, wala hizo allergies hatukukua nazo.. nasi tunawashangaa watoto wa frigi open wanapougua kwa kunywa Uji wa karanga au hata vumbi. Tumekuzwa ktk mazingira ambayo yalitujenga Ungangari, mwili wetu umeweza kuvumilia magumu kama kunywesha uji wakati pua zimezibwa. Ndivyo Vijiji vya Ujamaa wakati sisi tulilazimishwa hawa wenzetu wanaanzisha makazi mapya kwa kupima ramani na kugawa ardhi utaona watu wanahamia wenyewe.. Sisi tulianzisha Dodoma miaka 30 ilitopita lakini hadi leo inasemekana yalikuwa makosa makubwa..
Mkuu hivi kipi kinatakiwa kubadilika kwanza kati ya mazingira na watu?
 
Nimeona sehemu hapo juu, mwalimu said "in my report to the 1973 TANU conference I was able to say that 2,2028,164 people were living in village.two years later,in june 1975 I reported to the next TANU conference that approximately 9,100,0 00 people living together in 7,684 villages" na shivji amesema this is a tremendous achievement.
Lakini shivji hapo mwanzo kaandika "villagisation was a means of accelerating development and facilitating provision of health,education,water and other social services..
Swali ni, hilo lengo la services lilifanikiwa kwa kiasi gani? Au watu huko walitaabika zaidi..
Mwalimu alijisifu kwenye kiwango/idadi ya watu waliofanikiwa kuhama kwenda kwenye hivyo vijiji,lakini sioni mafanikio katika services yakitajwa na mwalimu katika andiko la prof.shivji..

LR,

Ukitakaa kupima mafanikio ya vijiji vya ujamaa, tumia namba. Watu waliohamishwa 9,100,000. Idadi ya vijiji 7684. Je kwenye kila kijiji kulikuwa na watu wangapi? 9,100,000/7684 = 1184.

Kila kijiji kilikuwa na watu 1184 ukijumlisha watoto na wasiojiweza. Niambie ni muda gani inachukua kwa watu 1184 kuanzisha makazi mapya, kuzalisha chakula cha kujitosheleza wenyewe, kujenga mashule, zahanati, kuwa na maji safi? Mwaka mmoja, miwili, mitatu, minne au mitano?
 
Aisee umesoma lakini hii kitu hapa chini?

Research in Economic History
Ec2339

Presents:

Philip Osafo-Kwaako
Harvard University

" Long-run Effects of Villagization in Tanzania"

Monday, November 14th, 2011
4:00-5:00PM
Littauer M-17
Abstract: Developmental villages (vijiji vya maendeleo) were introduced in mainland Tanzania over the period 1974-1982 as part of a large-scale resettlement program. This paper investigates the long-run impacts of these villages, examining whether variation in intensity of the government's villagization program explains within-region variation in social capital outcomes today. An earlier body of social science research largely criticized Tanzania'svillagization program as a failed example of large-scale state planning with adverse consequences for peasants. Combining historic data on Tanzania from the 1970s and recent national household surveys, I first document that developmental villages led to an increase in primary school completion rates. Today, districts which experienced a high share of developmental villages have greater availability of public goods and report higher rates of participation in community activities. I also report instrumental variable estimates based on a drought which facilitated the resettlement of peasants in these villages.
 
Naisoma. Lakini kitu ambacho mwandishi anakosea ni kuwa imetokea re-configuration na voluntary mass migration. Hivyo anachozungumza sasa ni vitu vingine.
 
aisee hebu weka haya maneno kwa kiingereza nimtumie, nitakutafutia na pepa yake pia;

ps. kuna hii kitu imetoka jikoni, imetulia sana: Justinian F. Rweyemamu – A Wealth of Knowledge

Companero,

Niletea pepa yake nijaribu kuisoma kwanza.

Mjadala huu umeanza kwa sababu mwandishi hakufikiri kuwa watanzania wamefanyia kazi. Na kosa analofanya mwandishi wa kazi hii nyingine ni kutotoa credits kwa watanzania kuweza kuli-invent maisha yao.

Inaonekana Mmaasai akihamishiwa Morogoro na kujengewa shule. Basi maendeleo kayapata. Lakini kupoteza kwa ardhi na kuharibikiwa kwa fabric ya maish yake sio tatizo.
 
Mkuu hivi kipi kinatakiwa kubadilika kwanza kati ya mazingira na watu?
Bila shaka WATU ndio watakao badilisha MAZINGIRA myatakayo. Maana MAZINGIRA ndio huttokana na dira ya Taifa na hivyo watu ndio waliobeba uzito mkubwa. Lakini hata siku moja huwezi kuibadilisha character ya binadamu isipokuwa tunaweza badilisha attitude zetu kupitia imani na uzalendo ulojengwa. Tuseme, vita yetu ya umaskini haitawezekana ikiwa wananchi wenyewe hawatakuwa tayari kubalisha tabia zao.. Sasa hizi tabia zitaweza tu kubadilika ikiwa kuna mafundisho yaliyolenga kupambana na umaskini na watu hao wataweza TAYARI kuyabadilisha Mazingira ili kuondokana na Umaskini..

Lakini pia hatuwezi tengeneza msahafu wa mafundisho iwe katiba yetu bila kuzingatia katiba hiyo inawalenga WATU gani, nini vipaji vyao, imani zao, utamaduni wao na kadhalika na katika hivyo vitu ni vipi vitaenziwa na vipi vitachukuliwa kama utamaduni mbaya dhidi ya malengo yetu.

Hivi sasa tupo ktk mchakato wa katiba mpya na tutafanya makosa makubwa sana ikiwa hatutazingatia kwanza WATU na MAZINGIRA kwa maana kwamba 1. WATU - Sisi ni Taifa lenye makabila zaidi ya 120, wenye imani ya dini tofauti hivyo ni katiba gani itakayowawezesha hawa watu kukaa zizi moja bila sheria zetu kuwadhalilisha baadhi yao na wakaishi kwa utulivu na amani. Kazi hii aliiweza sana mwalimu alipoweka Azimio la Arusha kuondoa makundi baina yetu lakini haikutosha kubadilisha Mazingira ktk kupambana na Umaskini..

There is no easy solution ktk Mazingira maana unapambana na tamaduni na mila za watu, wenzetu Ulaya waliweza kupambana na mageuzi ya WATU kwa miaka 200 kuweza kuunda taifa moja la Uingereza, Marekani, Ujarumani, France na kadhalika japokuwa baina yao wote wana asili tofauti. Kumbuka Hata Paul yule wa wakati wa Yesu asili yake alikuwa Mturuki lakini he identified himself as a Italian and a Jew, sisi ndio kwanza tunatafuta kusema hata Nyerere hakuwa Mtanzania.. Leo Marekani hata Mchina anajiita I am American, mtu mweusi vile vile wengine ukiwaambia una asili ya Afrika wanakutemea mate!. We failed kubadilisha watu kama tulivyo fail ktk viwanda na mashirika na sasa hivi tunakoelekea ndio kubaya zaidi maana western countries wameanza kuzijua tofauti zetu, mapungufu yetu na wanafanya kila mbinu kutugawa ktk makundi.

Tazama waarabu leo hii baada ya Western kujua kumbe wana makundi ya Sunni na Shia, sasa wanawalisha sumu yao wenyewe wanamalizana wakati hakuna sababu kabisa ya msingi. Ghadaffi, Saadam, Mubarak both were easily taken out kwa sababu wao ni Sunni na hawana umoja kama wa Shia ambao Assad wa Syria anaupata. So if you can change WATU to hate each other lazima watabalisha Mazingira from peaceful to warzone. Iraq, Libya, Misri will never be the same..Ni jukumu letu kufahamu hasara za kupoteza UMOJA wetu kitaifa kwa sababu tu ya tofauti za Kimtazamo.
 
Companero,

Niletea pepa yake nijaribu kuisoma kwanza.

Mjadala huu umeanza kwa sababu mwandishi hakufikiri kuwa watanzania wamefanyia kazi. Na kosa analofanya mwandishi wa kazi hii nyingine ni kutotoa credits kwa watanzania kuweza kuli-invent maisha yao.

Inaonekana Mmaasai akihamishiwa Morogoro na kujengewa shule. Basi maendeleo kayapata. Lakini kupoteza kwa ardhi na kuharibikiwa kwa fabric ya maish yake sio tatizo.

nina ppt yake tu, mpaka leo hujanipa email yako, usiwe na hofu wala mashaka mimi sio tiss kama nduguyo jasusi
 
Back
Top Bottom