Dah, kweli tunatofautiana.......

Na mpenzi wako unaweza ukaongea chochote.
Baada ya dakika 3 za maongezi muhimu zinazofata mara nyingi ni pumba.
Pumba nazo muhimu kwenye mahusiano. Zinanogesha.
 
Kama ni demu wangu haina shida, mi nachonga naye tu hata masaa 24 ili mradi tunayoongea hayana ubaya wowote. Mi napenda mpira na demu wangu alikuwa hapendi kabisa lakini tukichanganya story anaanza kupenda. Unaweza kuongea na mwanaume mwenzio bado mkaongea pumba vilevile. Labda kama unayeongea naye sio demu wako au siyo mtu wa karibu unaweza ukajiuliza kidogo. Kuna vitu vingi vya kuongea na kama mwanaume bado unaweza kumwambia demu wako kuwa nguo flani ilimpendeza. Mbona ukitongoza unasifia hadi hereni bwana, itakuwa kumwambia demu wako vitu kama hivyo. Nadhani hakuna tatizo, ukiweza kuongea muda mrefu au muda mfupi, cha muhimu ni kuwa wote mnakuwa na furaha na mnaridhika. Kuna demu anaweza kuwa anapenda muongee sana, we ukijifanya hutaki kuongea sana, watakuja wanaoendana naye halafu, freeesh. Maisha ndo haya tunayoishi, so kama haumkeri mtu mwingine au jamii kwa ujumla, fanya tu unachojisikia.
 
Kweli wanaume tunatofautiana, unakuta eti Mwanaume anampigia simu demu anapiga naye story kwa masaa manne hadi sita. Story zinazopigwa ni kuhusu Birthday, mahusiano, nguo za rangi gani zinavutia, sherehe gani unapendelea na kuhusu familia zenu mara Baba yangu ni mkali mara mama yangu hapendi kutazama Tv!!!
Au mimi ndiyo nina matatizo kwa sababu siwezi kuongea na demu kwenye simu zaidi ya nusu saa unless tunongelea mambo yanayoeleweka, mara nyingi huwa naona bora kumpigia msela mwenzangu na tukazungumza hata kwa masaa mawili bila kuboreka kwa sababu ni mengi ya kuongelea na wakati huo huo kujifunza, kwa mfano:

1. Siasa 2. wanawake 3. Manchester United 4. Wanawake 5. Chelsea 6. Wanawake 7. Kompyuta na elektroniki 8. Wanawake 9. Arsenal 10. Wanawake
11. Biashara 12. Wanawake 13. Bundersliga 14. Wanawake 15. Muziki 16. Wanawake
17. Magari 18. Wanawake............... 19. Masomo …………… na bado tukaahirisha mazungumzo kwa sababu ya muda au majukumu mengine.

Inaweza kutokea mtu unashindwa kulala eti kisa jirani yako anapiga stori na "rafiki yake" (mwanamke) tangu usiku mpaka asubuhi, ukimwambia amtongoze huyo demu basi kieleweke, anadai dini haimruhusu kutenda dhambi. Baada ya muda demu anapata Bwana, unaona njemba inanyong'nyea eti ita-miss mtu wa kupiga naye story. My foot!!!!!!

Kwenye hili suala kuna mtu lazima ana matatizo, aidha mimi au mtu wa aina hii….




Mkuu kwenye Blue hapo, huitaji kuwa na ulemavu ndo ujue watu tuko tofauti. Unavyoona wewe siyo kawaida au sawa kwa mwingine ni kawaida au sawa. Ndo ubinadamu huo unaotufanya tuweze kuishi katika jamii. Wote wangekuwa wanawaza au na tabia kama wewe sidhani kungekuwa na kukoseana au kuoneana kinyongo maana unavyofikili ndivyo mwingine naye angekuwa anawaza hivyo. Wakubali watu wa namna hiyo katika jamii uweze kuishi na kupata changamoto kutokana na kutofautiana.
 
Back
Top Bottom