HKigwangalla
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 717
- 971
- Thread starter
- #21
Hii ni hoja pana, nitaandaa mada inayohusiana na hili swali lako la kutoa mawazo yangu.Mheshimiwa, ukiwa miongoni mwa wachache waliomo kwenye vyombo ambavyo vinaweza kuleta mabadiliko tunayofikiria kama watu waliomo wakitaka, upi mchango wako katika kuboresha huduma za afya ndani ya nchi yetu leo. Tumekuwa wapiga hadithi sana...tungependa kusikia vitendo zaidi ya maneno.
Ila kwa haraka haraka tu ni kwamba tunahitaji kuongeza bajeti ya afya, kuongeza idadi ya wafanyakazi, kwa maana ya kuajiri wanaohitimu kwa kasi kubwa zaidi, maana leo hii wanahitimu mf madaktari 700 kwa mwaka lakini wanaoajiriwa na serikali ni chini ya 100, sasa tunapiga hatua mbele ama tuko pale pale? Pia tunahitaji kufanya jitihada za kuboresha mazingira ya kazini, mahospitalini kwa kuhakikisha vifaa na madawa yanapatikana muda wote hadi ngazi ya zahanati... tunahitaji ku-accelerate MMAM ... kumbuka ilani ya uchaguzi ya CCM ilitaka tuwe tumejenga vituo vya afya 11,000 kufikia 2015 lakini leo hii tumeongeza vituo 78 tu kufikia 2010/11 making a total of health center to around 6500, je tutafika?
Tupunguze utegemezi wa bajeti yetu kwa wafadhili...leo hii mchango wa JMT kwenye bajeti ya afya ni les than 40%, zaidi ya asilimia 65 ni wafadhili....hii inakwenda upside down na general budget ya serikali ambapo tunatoa zaidi ya 68% na wafadhili ni hiyo 32/35% inayobaki...