CUF yaiachia CHADEMA kata zote uchaguzi mdogo

Sasa wote si ukawa hakuna kinachopotea ..... swali je ulitaka cuf yenye pande mbili wagombea wake wawe loyal kwa nani??? Maalim au lipumba??? Sakaya kasema wanasimamisha kata zote hivo hawaitambui ukawa..... sasa ulitaka Cuf ya maalim na wenyewe waweke wagombea wao ama???
Sasa labda utoe suluhisho kuwa nini kifanyike sio kulaumu wakati hujui wanachopitia wenzako kwenye huo mgogoro
Hoja yangu hapa ni kuwa: kwa sababu CUF ina mgogoro, na maana ya Umoja ni nguvu, kwanini kata zingine wasipewe NLD na NCCR kwa sababu watakuwa na nguvu ya kushindana ndani ya UKAWA badala ya kata zote kupewa CHADEMA kwa kisingizio cha mgogoro wa CUF na kuviacha vyama vya NLD na NCCR kubaki wapiga debe. Hii ina maana kuwa UKAWA ni ya CHADEMA na CUF, na kwa sababu CUF ina mgogoro CHADEMA imenufaika na mgogoro wa CUF kwa kuachiwa kata zote na Maalim Seif.
Team Lipumba wamewashtukia CHADEMA
Sasa wote si ukawa hakuna kinachopotea ..... swali je ulitaka cuf yenye pande mbili wagombea wake wawe loyal kwa nani??? Maalim au lipumba??? Sakaya kasema wanasimamisha kata zote hivo hawaitambui ukawa..... sasa ulitaka Cuf ya maalim na wenyewe waweke wagombea wao ama???
Sasa labda utoe suluhisho kuwa nini kifanyike sio kulaumu wakati hujui wanachopitia wenzako kwenye huo mgogoro
 
Duh mbowe pekee ndo kamleta lowassa chadema?? Lipumba na slaa hawakuhusika kumkaribisha eeh?? Yaani slaa kamleta lipumba kampokea ila lawama ni MBOWE pekee ake.... duh mie nahisi una chuki binafsi na mbowe maana nachojua lowassa alikuja kwa baraka ya kamati kuu nzima slaa inclusive na pia vyama washirika so kma ungetaka kulaumu ulaumu wote kma UKAWA na slaa inclusive sio mbowe tu hyo lazma tutafsiri kma chuki binafsi
But mbona hakwenda cuf?ni mbowe alimpokea akamwita mtaji na sasa katajirika personally ila kisiasa sidhani.
 
"Vita vya panzi furaha ya kunguru". Asomae na afahamu!!
[HASHTAG]#UtuUzalendoUadilifu[/HASHTAG]
 
Nakubaliano na hoja yako na namsifu sana kwa kuimarisha upinzani na kukiweka chama tawala kilale na jicho moja wazi, ila kwa jinsi mauzauza anayofanya sasa nashawishika kusema Dr. Slaa ndiye aliyeimarisha upinzani, huwezi amini nilikuwa namsapoti mpaka alipobadili gia angani.
Unafiki wake ni kutokuwa na msimamo, akisema kitu kumbe hamaanishi. Aliujenga upinzani na Slaa ukawa imara ghafla akaja haribu kwa kupokea watu aliowaponda kuwa ni mafisadi na kuwaita ni wakombozi.
 
Huyo mketo anataka kutuambia kuwa Kuanzia sasa CUF itakuwa ni chama binti cha chadema?sheria za msajili zinaruhusu hilo?
 
Nyie ndo mnamharibia lipumba bila kujua mpka inaonekana kweli anatumika. Maana iweje ccm wamsifie mpinzani ?? Kma ya seif ni dhaifu si ndio mumsupport sasa amuangushe lipumba ili mbakie na mpinzani dhaifu SEIF mumshinde kirahisi 2020??
Yaani mlimpiga virungu mwaka huu pale mtongani eti leo hii kawa IMARA kwenu?? Really?? Kma angekuwa mpinzani wa kweli na anawanyima usingizi kweli mngekubali aendelee kuwa mwenyekiti ili aendelee kuwanyima usingizi zaidi???
SHAME ON YOU
siasa za upinzani ni za majitaka ambayo hata ukifanya kuyarudisha kwenye hali ya kawaida hauwezi , chadema wananufaika na mgogoro wa CUF kwa asilimia 100% CCM inanufaika na migogoro ya upinzani kwa asilimi 100% Kama ambavyo vyama hivi vya upinzani vinavyo omba CCM kuchafuke kwa hali na mali lakini wameshindwa kumbuka Lowassa alipo waambia nakuja na wakuu wa wilaya zaidi ya .... na wabunge zaidi ya.... mkaona sasa CCM inakufa moja kwa moja na chakushangaza Lowassa hakuja na hata mfuasi na aliokuja nao ni wale ambao mpaka leo wanajuta
 
CHAMA cha Wananchi CUF kimesema hakijasimamisha mgombea yoyote katika chaguzi za marudio zinazotarajiwa kufanyika Januari 22 mwakani katika kata 20.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo jioni Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF amesema hatua hiyo inatokana na mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho.

Mgogoro unaoendelea ndani ya CUF ni juu ya Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti 2015 lakini Juni 2016 akatangaza kutengua uamuzi wake na kuirejea nafasi hiyo huku uongozi wa CUF chini ya Maalim Seif ukipinga na hatimaye kumvua uanachama lakini ameendelea kutambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mketo amesema hapo awali CUF ilikutana na vyama washirika katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR – Mageuzi na National League For Democracy (NLD) ili kujadili namna vyama hivyo vitavyoshiriki katika uchaguzi ikiwemo kuachina kata.

“Sisi CUF tulikutana na vyama washirika wa ukawa katika kamati ndogo ya ufundi ya Ukawa ambapo tulikubaliana mambo kadhaa kuhusu kuachiana kata.

Wakati tukijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Ukawa katika uchaguzi wa marudio, ghafla akajitokeza Magdalena Sakaya (Mbunge wa Kaliua – CUF ambaye ni mfuasi wa Prof. Lipumba) na kutangaza kuwa CUF itasimamisha wagombea katika kata zote,” amesema Mketo.

Ameongeza kuwa, “Ieleweke kuwa hatujasimamisha wagombea sehemu yoyote na Sakaya na wenzake kutangaza kusimamisha wagombea katika kata zote ni utekelezaji wa kazi zao za kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi.”
Hapo ndio mjue ukawa nia yake ilikua kukiua chama cha cuf. sasa hivi cuf é finito.
 
Back
Top Bottom