CUF sasa wawapigia magoti CHADEMA

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wapinzani wamsihi Mbowe

Kambi ya upinzani isiyo rasmi bungeni imemuandikia barua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuomba wachaguliwe kuunda Baraza la Mwaziri Kivuli kwenye Bunge ili waweze kushirikiana kwa dhati kama kambi ya upinzani.

Katika barua ya kambi hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Hamad Rashid na katibu wake David Kafulila kwenda kwa Mwenyekiti wa Chadema wamesema wanaomba ushirikiano huo uanze kwenye Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza Februari mwaka huu.

Kambi hiyo ilimsihi Mbowe kuunda kambi ya upinzani imara ikishirikisha vyama vyote vya upinzani ili kuimarisha nguvu ya upinzani bungeni na kuibana serikali ya CCM kwa pamoja.

Vyama vilivyotoa ombi hilo ni CUF chenye wabunge 33, NCCR Mageuzi chenye wabunge wanne, TLP mbunge mmoja na UDP mbunge mmoja wakati Chadema kikiwa na wabunge 47.

Chadema ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani kimeunda kambi ya upinzani peke yake huku mwenyekiti wake akichaguliwa kuwa kiongozi wa kambi hiyo na nafasi nyingine za mawaziri kivuli zikijazwa na wabunge wa chama hicho pekee…..


Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili.

 
CDM wasithubutu kabisa kabisa kufanya kosa kama hilo...please CDM! Hivi hamfahamu kama CUF inafadhiliwa na RA -- ambaye ni hasimu mkubwa CDM?

Puuzeni ninalowaambia mtakuja juta. Hili suala la Dowans ndilo RA anataka kuanza nalo Bungeni kwa kuitumia CUF. Watch out!!!!
 
Jamani hebu CDM wasikilizeni hao na mkiona kuna dalili ya usaliti au mkigundua wametumwa na green guard muwakatilie mbali
 
Kuna haja ya kuchangamana nao bse lengo ni kujenga nchi sio kubomoa
 
Imekuwaje tena? Huyo Hamadi Rashidi alikuwa anawakandia sana CDM na hasa Mbowe. Mnakumbuka ule mdahalo wa ITV?

Mie pia nina wasi wasi kwamba hawa CUF wanataka kuwafanyia CDM kitu mbaya.
 
Jamani, waacheni waje. Kama Hamadi Rashidi au Kafulila wakienda kinyume cha azma ya upinzani si Mbowe anaweza kuwatimua kutoka kwenye Bara Kivuli?

Hamadi Rashidi (mkuu wa kambi wa upinzani bunge lililopita) alisha mtimua John Cheyo wakati wa kikao cha bajeti mwaka jana pale Mbunge huyo wa UDP alipotoa kauli ya kuiunga mkono bajeti kwa asilimia 100!
 
Hakuna haja hata ya kuwasikiliza. CUF ni ndumilakuwili. Hivyo CHADEMA tafadhalini msiwasikilize hao.

AMANDLA.
 
Mbwe usithubutu kufikilia kitu kama hicho . Naamini watumwa na ccm kuwamaliza . be very carefuly
 
CDM inachotaka ni ukombozi wa wananchi na si ukombozi wa vyama, kama CUF watakuwa wameona makosa yao na kuyajutia wanaweza kukaribishwa wakienda kinyume wanafukuzwa kama alivyofukuzwa Cheyo.
 
CDM inachotaka ni ukombozi wa wananchi na si ukombozi wa vyama, kama CUF watakuwa wameona makosa yao na kuyajutia wanaweza kukaribishwa wakienda kinyume wanafukuzwa kama alivyofukuzwa Cheyo.

Sio mbaya kama wakishirikishwa wakaweka watu wawili kutoka CUF kwa kuwa wamewaandikia barua kuwaomba basi CDM wawafikirie
 
Mimi naona bora wawakubalie ili wawe na nguvu kumbukeni Caf wapo 33 Cdm 44 hapo namba hizo zikiwa pamoja kwa CCM ni mwiba wa samki mkiwabwaga imekula kwenu watakuwa na CCM
 
CDM msiwe wabinafsi....mi nashauri muunganishe nguvu kwa kila anayetaka mapinduzi ya kuikomboa nchi yetu dhidi ya utawala dhalimu wa mafisadi.
Kuungana na vyama vingine haina maana ndo watawaharibia ...maana lazima kutakua na miongozo na maadili ya kufanya kazi katika huo muungano....Lingine ni kwamba sisi wananchi tupo makini sana kwa sasa na twajua ni nani wa ukweli na ni nani wa uongo.
Msiwaogope kamwe wachukueni kwenye muungano ili mladi wafuate kanuni za huo muungano.
 
o
<font size="3">CDM wasithubutu kabisa kabisa kufanya kosa kama hilo...please CDM! Hivi hamfahamu kama CUF inafadhiliwa na RA -- ambaye ni hasimu mkubwa CDM?

Puuzeni ninalowaambia mtakuja juta. Hili suala la Dowans ndilo RA anataka kuanza nalo Bungeni kwa kuitumia CUF. Watch out!!!!</font>
Umenifurahisha sana hilo la RA kuifadhili CUF, ofcourse ni unfounded allegation! Lakini la CDM kufadhiliwa na Kada wa CCM Sabodo mbona unalifumbia macho? Acha unafiki!
 
KAFU mbona wanakua kama ma...laya ...kule zanzibar wameshirikiana na sisiem wakaunda serikali ya mapinduzi ... huku bara wanataka waungane na CDM waunde serikali kivuli ya upinzani.... sasa wachague bwana mmoja tu...sisiem au CDM .... kama wanataka kuungana na CDM waipe talaka sisiem
 
Back
Top Bottom