kAMATI KUU YA CCM Imemshahuri Rais kukutana na vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni badala ya CDM kama walivyokuwa wamenuia! najiuliza mengi, hivi na hawa CUF na TLP nao wana hoja ya mapungufu katika Muswaada uliopitishwa Bungeni?! sidhani hivyo maana nahisi kama wawakilishi wa vyama hivyo ni kama wachumia tumbo maana matharani CUF baada ya kuingia kwenye muafaka kule Zanzibar wameendelea kuporomoka na kwa sasa mwenendo wao unatishia uhai wa chama chao! kwa sasa ni chama dhaifu mno! na huyo mrema naye ni aibu tupu! wanakwenda kuvuruga mazungumzo tu! Kumbe njaa ilikuwa inawasumbua! nasikitika sana kuona Prof. Lipumba ana bongo kweli lakini yupo sehemu isiyo sahihi! Hivi nyie CUF na TLP si mliunga mkono kwa kishindo na mpenzi wenu CCM?! Mnataka kwenda Ikulu kusema nini?!