CUF na Operesheni "Zinduka"

celebrating-cuf.jpg
Celebrating CUF, Celebrating Liberal Values.
 
Ukweli unabaki pale pale kuwa Lipumba aje na kujibu kwanini hawana mbunge hata mmoja?? Je ni kwanini ameshindwa kuongoza Chama hicho na mikakati Imara?? Je ni kwanini ameshindwa au kupunguza idadi ya Madiwani toka mwaka 200-2005, ukilinganisha kwa makini na minendo ya vyama hapa Tanzania utaona umarufu wa CUF umepungua sana


Kama ambavyo ukweli unabaki kuwa umeli ongopea jamvi
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/33226-ujumbe-kwa-salim-dimani-wa-cuf.html


Re: Ujumbe kwa salim dimani wa cuf

Quote:


Hivi CUF biharamulo ilisimika mgombea wake??




Iliunga mkono TLP na Opresheni ZInduka inakejeli "kulipua mabomu ya ufisadi", jambo ambalo ndio nguzo ya sasa ya Chadema na baadhi ya wana CCM, mkakati uliopata uungwaji mkono mkubwa wa umma. Sasa CUF kwa kuungana na TLP na NCCR Mageuzi katika chaguzi ndogo zilizopita wako sahihi? na je, wataing'oa CCM kuelekea 2010 ama ni mkakati wa 2020?
progress.gif
 
Afadhali Lwakatare kaona mbali,baadala ya kujipanga na constructive idea to win on the coming election wanaegemeana kwenye mabomu nadharia, CCM ikishinda kelele zinaanza kumbe hawajipangi sawasawa.

waende kwa wananchi kunadi sera siyo kulaumu for nothing ,wawaeleze wananchi mikakati yao kama watapewa dhamana na hasa kipaumbele katika kuiniua hali duni za watanzania.

kelele za chura hazimzui tembo kunywa maji.

thx.
 
kama Lipumba amekuwa PUMBA ajiuze kwa wauza komoni, maana amekosa cha kusema. tena yeye ni fisadi mbaya zaidi anapandikiza chuki kwa watoto wetu wakati anakula hela ya serikali na CCM pia. yawezekana CUF nayo ni CCM-C
ha ha ha komini hivi hadhi ya CUF kuwa CCM -B iliisha lini au humu jamvini munabatiza majina kutegemea nyakati
 
3th July 2009, 10:13 AM nikimjibi Calipso, nilisema hivi:


Quote:


[/B] Mkuu Halisi..
siku nyingi una maneno kama haya,na niliwahi kujibu matamshi yako,the way ulivo na maneno yako ni tofauti kabisa.. tatizo lako na mafisadi limalize mwenyewe,sijui niseme ni miongoni mwa watu wanaotumiliwa na ccm kukipakazia Cuf kama walivofanya nyuma,walivokuwa wakipakazia ni chama cha udini,cha warabu na mengineo sasa unaleta propaganda nyengine..sawa mkuu wasaidie hao ccm,lkn huna ushahidi na unaloongea.. lkn kaka yangu siko unapokwenda,rudi kwa Mola wako...[/I]




Siwezi na sijawahi kutumiwa na chama chochote cha siasa ikiwamo hiyo CCM. Nafahamu unajua hata CUF haijawahi kunitumia na hata pale nilipofanya kazi za CUF, CCM, Chedema, NCCR-Mageuzi, TLP, TADEA, nilifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya majukumu yangu ya kawaida. Hivyo ndivyo ilivyo JF. Hoja za msingi ni kwa CUF kusafisha hizo kelele kuhusiana na matatizo ya ndani ambayo si vyema yakatumika kukichafua. Najua maneno ya ufadhili yamekera lakini nimegusia nikijua mulio ndani mutaelewa na kusafisha hizo tuhuma ikiwa ni pamoja na zile za mpakani.

Kimsingi CUF ikijipanga inaweza lakini ijiepushe sana na watu wanaojifanya kuwa ni wema kwao, hasa wale wenye mikono michafu na umekiri mwenyewe kwa kusema, "tatizo lako na mafisadi limalize mwenyewe", pamoja na kufumba kwako, najua umelenga nini na hii inanitia faraja kwamba umenielewa. Bila kusema hatuwezi kujirekebisha na bila CUF yenye nguvu hakutakuwa na mageuzi ya kweli katika nchi hii. CCM imekuwa makini sana kupenyeza agenda za kuua nguvu za upinzani. Wametumia mbinu za kubeba ajenda ya ufisadi ya kina Dk SLaa na Hamad Rashid, wameibua hoja ya kujifanya Bunge la wabunge wengi wa CCM lina nguvu, yote ni kupoteza mwelekeo kabla ya 2010 na kuwanyang'anya hoja wapinzani. Huko Zanzibar nako wameibuka na kubeba hoja ya mafuta ambayo Maalim Seif amekuwa akiimba miaka yote, leo imekuwa hoja ya Karume na shemeji yake Mansoor na CUF wanashangilia. Lazima muamke.

Kama ulivyosema "mafisadi ni tatizo langu" ikiwa na maana ya kuwa halikuhusu, narudi tena kwenye hoja yangu ya pili kwamba CUF isipopima upepo unavyokwenda itaendelea kupoteza mwelekeo na labda iwekeze kuelekea 2015 ama 2020 na si 2010.

Kumbukeni niliyowahi kusema kuhusu "Operesheni ZInduka ya CUF" kuhusiana na jinsi watakavyoipeleka. Wameanza vyema na sasa tumeona Lipumba ameanza kumsafisha Lowassa kama ambavyo aliwahi kumtetea Rostam. Inawezekana isionekane hivyo lakini kwa kusema kwamba uamuzi wa Richmond ni wa Baraza la Mawaziri lote chini ya Kikwete ambaye naye aliridhi, ina maana sasa Lowassa alionewa> Hata kama ni kweli (jambo ambalo siamini) kisiasa si CUF wa kuliweka hilo. Wangejiepusha nalo. Itachukua muda (si 2010) kwa wananchi (wapiga kura) kuwaelewa CUF kwa kuibua suala la Richmond kwa staili yao. TAFAKARI





https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/11725-muafaka-ccm-na-cuf-pande-mbili-za-shilingi-15.html
 
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/33226-ujumbe-kwa-salim-dimani-wa-cuf.html



Re: Ujumbe kwa salim dimani wa cuf


Quote:​




Hivi CUF biharamulo ilisimika mgombea wake??




Iliunga mkono TLP na Opresheni ZInduka inakejeli "kulipua mabomu ya ufisadi", jambo ambalo ndio nguzo ya sasa ya Chadema na baadhi ya wana CCM, mkakati uliopata uungwaji mkono mkubwa wa umma. Sasa CUF kwa kuungana na TLP na NCCR Mageuzi katika chaguzi ndogo zilizopita wako sahihi? na je, wataing'oa CCM kuelekea 2010 ama ni mkakati wa 2020?

progress.gif

Hah ha ha ha ha

Nani alikwambia wapinzani wanatafuta kuing'oa ccm ? Hapo umenowa mkuu ,wapo pale kwa masilahi binafsi, kwa dhamila ile ile ,mlengo ulele,nia ile ile ,sababu zile zile,hamu ile ile na uwezo ule ule
 
Hah ha ha ha ha

Nani alikwambia wapinzani wanatafuta kuing'oa ccm ? Hapo umenowa mkuu ,wapo pale kwa masilahi binafsi, kwa dhamila ile ile ,mlengo ulele,nia ile ile ,sababu zile zile,hamu ile ile na uwezo ule ule
Tune ya TOT hiyo!!
MkamaP, CCM itang'olewa tuu, Subiri hawa wapinzani uchwara wanaoendekeza njaa watakapojidhihirisha kama tunavyoona sasa watakapo toswa na waTZ na kuwapa nafasi wale wenye nia thabiti ambao CCM haipumui kwa kuwahofia,hata wewe unawafahamu.
Wimbo huu wa Profesa ndio ubeti wake wa mwisho katika siasa, ni kama ule wimbo wa Mzee wa Kiraracha kule Biharamulo "Chagua TLP,ukishindwa basi ipe kura CCM ......."
 
Mkuu halisi..
Tatizo lako umeweka mbele maslahi yako,yaani unaongelea kile ambacho unaona kina maslahi na wewe,huzungumzii ukweli halisi ulivo,ndugu yangu ajenda ya RA ya kukifadhili cuf ni uongo mtupu na huna ushahidi na hilo,na ukitaka nikuthibitishie kama ni uongo unaouongea basi lete zile barua za Lwakatare tuzijadili,kuna kipengele kiko wazi ambacho wewe unakichukua,kinaonesha hasa kuwa hilo suala halipo,na ndo mana mpaka leo huwezi kutoa ushahidi,na ukizungumza kuhusu Jusa na RA kuwa ni marafiki ni kweli,lkn ni suala la mtu binafsi,mbona wewe una marafiki wakubwa tu wa ccm? mbona Salmin na Juma duni ndugu kabisa,mbona nasor khamis ni shemeji yake Amani na wengineo au hujui,sasa hilo ni suala la watu binafsi,mbona tulisikia kubeinea katembelewa na Kikwete spitali,mbona tuliskia kafadhiliwa na kikwete kwenda matibabu au tuseme yule kubainea ni ccm? sasa ndugu yangu Cuf ingekuwa inashirikiana na mafisadi wasingezungumzia ajenda za ufisadi na ujue Lipumba kaanza kuzungumza ufisadi kabla ya akina Dr slaa na zitto,na hivi sasa kwa kujiamini Lipumba ameanza kuweka wazi ufisadi unaofanywa mpaka na vyama pinzani kwa anajiamini yupo safi,na ukizungumza Kuhusu kumsafisha Lowasa,yaani nakushangaa sana ndugu yangu duh! yaani kusema na kikwete anahusika moja kwa moja na kwa kuficha ukweli wakaamua wamtoe kafara Lowasa peke yake lkn wote wanahusika,ishakuwa anamsafisha? duh! hebu fatilia uzuri.. sasa nakuuliza kwanini husemi kwamba chadema waje wajibu tuhuma,unang'ang'ania cuf tu? upo fair kweli? au ndo bado tupo kwenye mfumo wa chama kimoja?
 
Nimezinduka, CUF hawana mpango tena wa kushika dola ndo maana wameacha kupambana CCM na badala yake wanaelekeza mapambano kwa CHADEMA.
 
Nimezinduka, CUF hawana mpango tena wa kushika dola ndo maana wameacha kupambana CCM na badala yake wanaelekeza mapambano kwa CHADEMA.
Hawana kabisa mpango huo na pia sasa wamebaki na majungu yasio na maana yoyote ile
 
Nimezinduka, CUF hawana mpango tena wa kushika dola ndo maana wameacha kupambana CCM na badala yake wanaelekeza mapambano kwa CHADEMA.
Kweli na ndo mana,chadema waliwahi kumfata Mustapha wandwi wa cuf wakampa na pesa ili aingie chadema, kweli kabisa maneno yako,na ndo mana chadema wakabambwa live wakiongea na Lwakatare ktk hoteli moja kubwa,wakati huo Lwakatare bado ni naibu katibu mkuu wa cuf,kweli maneno yako,ndo mana chadema wakaenda kufunga matawi ya cuf kule bukoba. he! bado cuf wakae tu wanyamaze, kweli maneno yako,ndo mana cuf walikuwa wanawaachia baadhi ya majimbo chadema lkn walipotaka kusimamisha wao cuf,chadema wakawajibu UPEPO UMEBADILIKA. Duh! kumbe cuf imevumilia saana. sasa sijui nani yupo kwa ajili ya mwenzake,akili kichwani mwako....
 
Chadema bila ushirikiano na vyama vingine mjue mta-angukia pua katika uchaguzi ujao.

Washirikiane na vyama vipi? CUF au?
Siku zote ambapo CUF wamekuwa wakiungwa mkono na CHADEMA hawakufahamu kuwa ni chama cha mafisadi, leo baada ya kuona mwendo unashika kasi ndio wanafanya uvumbuzi wa Mzungu kuvumbua mlima Kilimanjaro!

Siku zote naamini ushirikiano wa vyama hauwezi kuleta tija. Kinachowezekana na kuvivunja na kujenga chama kimoja, vinginevyo, hao waliovianzisha walikuwa na malengo na misingi ambayo daima haiwezi kuvifanya vitengemae katika ushirikiano!
 
Washirikiane na vyama vipi? CUF au?
Siku zote ambapo CUF wamekuwa wakiungwa mkono na CHADEMA hawakufahamu kuwa ni chama cha mafisadi, leo baada ya kuona mwendo unashika kasi ndio wanafanya uvumbuzi wa Mzungu kuvumbua mlima Kilimanjaro!

Siku zote naamini ushirikiano wa vyama hauwezi kuleta tija. Kinachowezekana na kuvivunja na kujenga chama kimoja, vinginevyo, hao waliovianzisha walikuwa na malengo na misingi ambayo daima haiwezi kuvifanya vitengemae katika ushirikiano!
Mwaka 2000, Chaguzi zote za kule Zanzibar na kila wakati walikuwa karibu sana katika siasa za Tanzania lakini CUF walikuwa hawaoni haya na sasa baada ya CHADEMA kuchukua uhalisi wake
 
Sema wewe na pia itakuwa vizuri akaenda kufundisha uchumi kule Dodoma university maana kuna uhaba mkubwa sana wa Walimu
 
Kweli na ndo mana,chadema waliwahi kumfata Mustapha wandwi wa cuf wakampa na pesa ili aingie chadema, kweli kabisa maneno yako,na ndo mana chadema wakabambwa live wakiongea na Lwakatare ktk hoteli moja kubwa,wakati huo Lwakatare bado ni naibu katibu mkuu wa cuf,kweli maneno yako,ndo mana chadema wakaenda kufunga matawi ya cuf kule bukoba. he! bado cuf wakae tu wanyamaze, kweli maneno yako,ndo mana cuf walikuwa wanawaachia baadhi ya majimbo chadema lkn walipotaka kusimamisha wao cuf,chadema wakawajibu UPEPO UMEBADILIKA. Duh! kumbe cuf imevumilia saana. sasa sijui nani yupo kwa ajili ya mwenzake,akili kichwani mwako....

Acha kuleta maneno yamitaani -- ya akina wandwi nk yasiyokuwa na uthibitisho. Ukweli unabaki palepale -- CUF imepoteza dira kabisa -- viongozi wao badala ya kwenda Pemba kuwasaidia wenzao wanaonyanyaswa na ubabe wa CCM kujiandikisha kupiga kura -- wao wako mwanza kuisaidia CCM hiyo hiyo kujaribu kuibomoa Chadema -- mwiba wao mkuu kuhusu ufisadi.

Inanikumbusha Mbatia wa NCCR alivyokwenda Pemba kuisaidia CCM kuibomoa CUF na huku akiliacha jimbo la Mbunge wake Kigoma kusini kuchukuliwa na CCM kiilaini. yeye mbatia alifanikiwa angalau kuwapa viti CCM.
Kusema kweli hamueleweki kabisa -- ni kama vile wametumwa na CCM, au sana sana mafisadi -- kwani tunasikia Jussa na RA ni dam dam.
 
Baada ya Kusoma hizi quotations za wana-CUF kuhusu mafisadi, niliwasiliana na Mzee Edwin Mtei. Mzee Mtei amesema hajapata nafasi ya kusoma matamshi ya Prof. Lipumba, lakini akakiri kwamba anam-respect sana Lipumba as an economist.

Kuhusu ugavana wake wa Benki Kuu, alisema aliteuliwa Gavana mwaka 1966 akaanzisha sarafu mpya (currency) ya kitaifa na Benki Kuu yake. Amesema ali-hand over to Charles Nyirabu kama Gavana mwaka 1974. Charles Nyirabu alikuwa ni Deputy Governor wake na sio Bob Makani.

Baada ya BoT, Mtei alikuwa Secretary General wa East African Community mpaka ilipovunjika mwaka 1977 ambapo alirudi Dar es Salaam na kuteuliwa Waziri wa Fedha na Mipango. Mzee Mtei alijiuzulu uwaziri baada ya kutofautiana na bosi wake, Mwalimu Nyerere juu ya sera, hasa za uchumi na fedha. Ndipo alipoanza shughuli za kilimo mwanzo wa mwaka 1980.

Mzee Mtei ameeleza kwamba alichaguliwa na Magavana wa English Speaking African countries Oktoba 1982 kuwa Executive Director wa International Monetary Fund, na akahamia Washington D.C. mpaka Novemba 1986. Wakati jengo la BoT alilolisimamia likijengwa lilipoungua kwa moto mwaka 1984, alipigiwa simu akiwa huko Washington. Charles Nyirabu ndiye alikuwa Gavana, na Deputy wake alikuwa Bob Makani. Kama CUF au Lipumba wana ushahidi wa wizi au ufisadi kuhusu chanzo cha ule moto, waulekeze kwa waliokuwa na jukumu kuendesha BoT. Wajifunze pia historia ya BoT na waepuke uzushi.

Mzee Edwin Mtei alikuwa Muasisi wa Chadema mwaka 1992 na alikiongoza kama Mwenyekiti Taifa mpaka 1998 alipo-hand over to Bob Makani. Anasema sasa anafarijika sana kuona CHADEMA chini ya uongozi mpya wa vijana jasiri, wabunifu na wazalendo kinakuwa tishio kwa chama tawala.

Badala ya CUF kuunganisha nguvu na Chadema ili kuleta demokrasia ya kweli nchini, inaonekana viongozi wake wanabuni hadithi za ufisadi dhidi ya Mzee Mtei, ambaye by any stretch of the imagination, hahusiki. Kama kweli kuna mkono wa R.A. ktk kupika hizi hadithi za uongo basi Tz tunaelekea pabaya.

Mzee Mtei ameniambia kwamba anatafuta hayo magazeti yaliyomnukuu Lipumba na wana-CUF ili aone wamemkashifu kiasi gani. Amesema kwamba hana shida na fedha, eti aende kortini ku-sue misguided wana-Mageuzi kama hilo kundi la CUF. Endapo watamuomba Mzee Mtei msamaha hadharani hiyo itatosha.
 
Last edited:
Back
Top Bottom