Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Kweli inasikitisha. sasa hivi Wapemba wanayimwa kujiandikisha kupiga kura ili CCM wayachukue majimbo yao 2010 viongozi wao wako huku Bara wanatumikia agenda za RA dhidi ya maadui zake.
Profesa, tulikuamini sana, achana na hao akina Jussa na Maalim, pigania haki ya wazalendo hapa wanaoibiwa fedha zao kila siku na majambazi ya CCM. Achana kuikandia Chadema kwa agizo la RA, ungana na Chadema katika kuutokomeza ufisadi ndani ya CCM kwa lengo la kuleta utawala bora. Achana na tamaa ya pesa za wizi, pigania haki ya wazalendo hata bila malipo, kwani siasa za kweli ni kujitolea.
Kama kweli una uchungu wa nchi hii, adui yako inapasa awe CCM, na siyo Chadema. Unapotea sana. Utakimbiwa na wengi.
Yakhe Pemba hakuhitaji hata kampeni wala kiongozi wa CUF kwenda huko ,WaPemba mambo wanayaweza na wala yasikupe shida ,wameshaamka na wanajua nanmna ya kupambana na CCM ,ile viongozi wa CUF kufikia kusema ni wajibu wao tu,(wametimiza wajibu wao kuifahamisha jamii)
Adui sio CCM adui ni wale wote walio na wano ifisidi nchi hii wawemo CUF au Chadema au kwengineko kokote kule ,hao watakuwa maadui ,sasa tusiwe wenye kubabaika katika kuchagua viongozi au Chama kilicho bora kwa kuwa tu baadhi ya viongozi fulani wamekuwa mstari wa mbele katika kulipua mabomu ni lazima ukubali kuwa unaponyoonyeshea wenzio kidole basi kama hukuangalia vizuri vidole vingine tena vinne vitakuwa vinakuelekea mwenyeo , na kama haitoshi mara nyingi wanaolipua mabomu hutokezea mambo yakaenda kombo mabomu yakamlipukia mikononi.
Hivyo tusiwe katika msimamo usiotetereka ,inavyokuwa tunaisimamia haki na kuuchukia ufisadi basi hatuna budi kumuumbua yeyote yule ,ikiwa ni Lipumba au Seif au mwengine yeyote, tusione soo kusema au kukubali kuwa viongozi wa Chadema kumbe nao wamo katika kapu la ufisadi ,tusiwe na gatigati ,ugumu wa kuwaumbua kwa kuwa tu ,tunao au tupo pamoja nao ,hawa kama ni wahusika wa ufisadi kwa kweli watakuwa hawafai na hawatufai ,let us be sensible katika kupambana na wafujaji wa uchumi wa Taifa na Nchi hii ya Tanzania ,haiwezekani ikawa tunapigana na CCM peke yake wakati upnde wetu wapo wanaop fanana nao ,huko kutakuwa ni kutaka kwanza kuwadanganya wananchi na pili kuwaonea choyo CCM ni kwamba tunataka kuwaondoa CCM kwenye ulaji ili tukamate sisi ,CHADEMA imetuhumiwa kuwa hakuna viongozi wenye sifa zinazofaa kuongoza hilo sio jambo dogo ,kwa maana ingine ile kulipua yote ilikuwa ni kutembea na ngozi ya kondoo.
Lazima tuwajibike kwa hili kama hawa waliotuhumiwa na CUF ni wahusika wa ufisadi fulani fulani basi isiwe mbinde kuwachanganya na wale wa CCM na kama Lipumba nae anahusika nae mtajeni ila hadi leo sijaona ni wapi Lipumba amehusika au kuwa upande mmoja na akina Rostam huko itakuwa ni kumzulia au kutaka kumhusisha na mkumbuke tu siku zote ukweli unakuja juu ,sasa mnaweza mkaumbuka ,sijawasikia viongozi wa CHADEMA kulisema hilo kuwa Lipumba anahusika na kuwasaidia akina Rostam ,jamani na wao waseme tusikie kuwa viongozi wa CUF nao ni mafisadi hivi kama kuna ukweli itakuwa shida ,ila naona sasa kama mmebabaika baada ya kuumbuliwa kwa viongozi wa CHADEMA ,msiwe hivyo kubalini ukweli na msiseme Lipumba ameharibu upinzani ,bado hajaharibu kitu.
Naona kama CHADEMA nao wameshikwa pabaya.