Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,429
CUF acheni kutunishiana misuli, wenye hekima tushaona mnavyoenda mnaenda kubaya wote na sasa tunaona ipo haja ya kuwashauri kwa hekma ili muweze kunusurika.
Kimsingi kwa mtu yeyote ambaye ni mdau wa demokrasia, hawezi kufurahia kuona migogoro ndani ya vyama vya siasa ambayo inatishia kuviua vyama hivyo. Kwa mantiki hiyo, umefika muda sasa wa wadau wa demokrasia kuwasaidia CUF kupata suluhu ya mgogoro unaowakabili. Aidha, kwa kuwa CUF ni chama cha upinzani, vyama vingine vya upinzani vina jukumu la kuwasaidia CUF kufikia Suluhu kuliko mtu mwingine yeyote.
HATARI ILIYOPO KAMA MGOGORO HUU UTAENDELEA KAMA ULIVYO;
Ikiwa, mgogoro huu utaendelea kama ulivyo bila kusuluhishwa kwa njia za kidiplomasia, madhara ya fuatayo yanatarajiwa kujitokeza.
1. Kuzidi kwa chuki miongoni mwa wana CUF wenyewe kwa wenyewe hasa chuki kati ya wana CUF wa zanzbar/ pemba dhidi ya wale wa Bara.
2. Kuzidi kwa chuki ambayo haiwezi kuwa na faidia kwa yoyote kati ya Prof. Lipumba na Maalim.
3. Kwa upande mmoja CUF ya maalim Seif itakufa kwa kukosa uungwaji mkono wa kitaasisi na kisheria (kutokana na position ya mgogoro kwa sasa) na kwa upande mwingine CUF ya Lipumba itakufa vile vile kwa kukosa uungwaji mkono wa kutosha Zanzibar lakini pia kwa kukosa "Cause and Purpose" bara. CUF itapoteza wabunge wengi toka pande zote. Kwa hiyo wakiendelea hivi matokea yanatarajiwa kuwa "Zero sum game" kwa pande zote.
NINI CHA KUFANYA;
Kwa kuanzia,
1.Tunaziomba pande zote (Maalim na Prof. Lipumba) kwanza waache kutoleana kauli kali na za kuudhi ambazo zitaendelea kuleta uhasama.
2. Maalim aitishe vyombo vya habari akiwa pemba na kueleza wafuasi wake kuwa yuko tayari kufikia maridhiano na prof. Lipumba na Lipumba aitishe Press Dar akieleza utayari wake wa kufikia maridhiano na Maalim.
3. ACT (kwa sababu wanaweza kuaminika na pande zote), wawasaidie CUF kuwatafutia msuluhishi ambaye anaaminika na pande zote ambaye kwa haraka sana ataita wajumbe wa pande zote na kuanza hatua za maridhiano, kwa kuangalia uwezekano wa Lipumba kuendelea kuwa Mwenyekiti na Maalim kuwa Katibu kama ilivyokuwa awali.
MSULUHISHI
Napendekeza Msuluhishi awe ni Shekhe, Maalim Ally Basalleh wa dar es salaam. Hii ni kwa sababu kwa sasa kitu pekee kinachowaunganisha Lipumba na Seif ni dini, wote wanamfahamu vizuri Basalleh na wamekuwa wakiswali nyuma yake mara kwa mara. Aidha Shekhe basalleh ni msomi, mtu mzima, muelewa na mwenye busara kubwa sana.Naamini suluhu itafikiwa.
Nawatakieni suluhu njema.