CUF kwa nini tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga

tatizo lenu cuf mmeitwa ccm b kwa sababu ya kukiponda cdm hadharani thus why wananchi wakawa wanawashangaa chama cha upinzani kinampinga mpinzani mwenzie badala ya ccm na ule muafaka umewaathirh sana. But anyway pole sana.
 
Asante Mtatiro kukubali ukweli na huo ndiyo uungwana.

Swala la kuwa ninyi ni CCM B ni kubwa miongoni mwa wananchi. Sina ushahidi wa jambo hilo lakini kuna minong'ono kuwa maalim alinunuliwa Zenji. Aidha itakuwa vigumu sana kwa ninyi kuwa na break through has baada ya kuingia kwenye ndoa ya ajabuajabu na CCM. Angalia usojepoteza mida wako ndani ya cu ukaja juta baadae.

Mimi binafsi nakuamini na nadhani una fursa nzuri za kusaidia kuleta demokrasia nchini ila chama chako na misimamo ya ajabu!
 
Mura Mtatiro umezungumza vizuri na hasa unapokubali kushindwa vibaya na kugundua udhaifu wenu CUF pamoja na uelewa wa wananchi wa igunga.

Kilichowaumiza kwa sehemu kubwa ni kutumia muda wenu mwingi kuishambulia chadema na mkaisahau ccm ambaye ndiye mbaya wetu CUF na vyama vingine vya upinzani.

Mwisho kabisa nikutakie kila la kheri na karibu sana chadema ujumuike na wapiganaji wa ukweli na treni ya ukombozi wa Tanzania kwa sasa inaendeshwa na chadema usipoteze muda wako we panda twende zetu.
 
Afadhali umejifunza na kuyasema haya mwenyewe. Huo ni ujasiri mkubwa. Msingekuwa ccm B katika utendaji wenu wananchi wangewahukumu kadiri ya uwezo wenu. Mlikuwa na mgombea mzuri, lakini kwa vile nyie ni ccm B wale wale mafisadi ambao Rostam alisema wana siasa uchwara. Gharama yake ndiyo hiyo.

Hadi watanzania watakapoona kuwa nyie sio ccm b, hamna lenu huku, labda muambilie huko Pemba na Unguja. Endeleeni ndani ya ndoa yenu na ccm. Msingekuwa ccm B hata chadema isingehitaji kutumia nguvu kubwa kuitoa ccm madarakani, lakini tangu mwaka jana mlifanya jitihada kubwa pamoja na mwenyekiti wenu Taifa kukwamisha safari ya ukombozi wa Tanzania iliyokuwa inafanywa na Chadema. Uccm b wenu ukawa mtaji mzuri kwa magamba.

Igunga tumesikia hadi waliwaletea helkopta. Watawafanyia mengi tu, as long as you remain loyal to them.

Now you may decide if you like, either to remain loyal to them- ccm A and continue losing a lot in the future or you stand on your own as CUF, and become at least recognised by Tanzanians as a genuine political party that struggles for the better life of its People.
 
Hivi sisi tumelogwa na nani?? Ina maana Mtatiro ameyajua haya baada ya kupigwa mweleka na Chadema???

Halafu sijui anajaribu kutueleza nini baada ya kuisadia CCM kuendeleza ufisadi wao Igunga. Hata waombe radhi namna gani, dhambi waliyotenda hawa watu wa CUF kwa kuhujumu harakati za ukombozi huko Igunga itawafuna milele hadi hiki chama kifutike kwenye uso nchi hii....especially huku kwetu!!
 
Mara nyingi huwa mnasema "tuna nguvu katika jimbo fulani, wapinzani wengine watumie ustaarabu kutuachia", lakini mambo yanakuwa tofauti. inafikia mahali inabidi mkubali sasa kwamba chama chenye nguvu katika wapinzani ni CHADEMA, na mkiunge mkono huku bara, mtaonekana wastaarabu.

Hata zile kura 11,000 mlizokuwa mnajivunia zinadhihirisha kuwa mlizipata kwa kuwa CHADEMA hawakuweka mgombea, si kwa kuwa wananchi wanawapenda. Naomba muimarishe nguvu kule visiwani pamoja na maeneo machache ya bara kama vile Lindi, Mtwara, Tunduru na Mafia, hapo nitawaelewa kwani walau mnakubalika, na hata CHADEMA wakiwapinga huko nitaona sio wastaarabu.

Otherwise mkiunge mkono CHADEMA, adui ni CCM si CDM
 
Pole mkuu. Ila jiulize kwa nini CCM B ichukiwe na kushindwa vibaya, lakini CCM yenyewe ipendwe na kushinda uchaguzi?
 
pole mkuuuuu. umesahau ulianza na pingamizi kwa wagombe.a wengine ? hilo pia limekultafuna WAMEKUFANYA HAKUNA AISEE.
 
Lazima Niwasifu CUF kwa siasa zao za ustaarabu. Hongereni Sana Kwa Kuelewa Ni Nini Kimewakwamisha Na Kuonesha nia ya kulimaliza hilo tatizo.
 
Hivi sisi tumelogwa na nani?? Ina maana Mtatiro ameyajua haya baada ya kupigwa mweleka na Chadema???

Halafu sijui anajaribu kutueleza nini baada ya kuisadia CCM kuendeleza ufisadi wao Igunga. Hata waombe radhi namna gani, dhambi waliyotenda hawa watu wa CUF kwa kuhujumu harakati za ukombozi huko Igunga itawafuna milele hadi hiki chama kifutike kwenye uso nchi hii....especially huku kwetu!!

Huyu poti wangu anajua anachokifanya. Niliangalia kampeni zao kupitia tv sibuka, jamaa walikuwa wanaishambulia chadema mwanzo mwisho.

Sasa wananchi wa igunga wameamua kuzungumza nao kivitendo.
 
Mtatiro mlikwenda Igunga mkijua kwa hakika kuwa mtapata matokeo mliyopata.

Ndio sababu mlipofika Igunga vita yenu ikawa ni Chadema na sio CCM. Kwa hiyo usije unalia lia hapa ili kudhani tapata huruma zetu.

Labda nikuhakikishie jambo moja tu kwamba hivi ndivyo itakavyokuwa hata chaguzi zijazo. Wewe baki tu ukijiridhisha kwa maneno mengi yasiyo na maana. Ile dominance ya kafu kwa siasa za upinzani bara na visiwani imekwisha. Nakuahakikishia hata kule Pemba mmekwisha.

Nashangaa kwa nini hukuzungumzia kwa nini wale wapiga kura wenu wengi wa october 2010 wamewapa kisogo!!!! Najua utabaki na story za ndoa yenu na ccm. Sawa kama ndio sababu huoni kwamba mmekwisha? Mmebaki nyie na ccm kuhubiri udini tu.

Hivi ndivyo NCCR walivyokwisha pia, now your the next. Na wewe utakwisha kisiasa na kafu yako.
 
Mtatiro nakufaham sana jinsi ulivyo strong tangu tulivyokuwa kwenye harakati chuo. Pole kwa matokeo ya Igunga, naamini ukitulia utaendelea kujifunza mengi kutokana na matokeo hayo!

Ushauri wangu mdogo kwako, Ikiwa kweli unadhamira ya kuijenga CUF, basi usijaribu kuibomoa kwa kuiponda CDM! Tumia nguvu zako nyingi kupambana na wadhalimu CCM na utashinda. Kuiponda CDM ni kujijengea chuki mbele ya wananchi wengi ambao kwa sasa wanaiona kuwa ni mkombozi wao! Kwa hiyo kupambana na CDM kutapelekea kuiua CUF...
 
ndo basi tena
cuf kwa tz bara msahau
ndoa ya mkeka ina gharama ati
si mliona mko sahihi zaidi
hata mkauza ushindi last year huko zenji
ipo wapi nguvu yenu sasa huko tabora
au mapalala hakuwasaidia????
 
mura,nyamwabho mtatiro,njoo chadema mura,omanyere abharisya bhayo cuf bhasira tanganyika mbareno,taighwa mbe mura,insho chadema mura tokore amang'ana,tabhateghera abhakangi ekafu yabho!
Mura,uighure?
 
Poleni sana CUF, nimependa ulivyojielezea angalieni wapi mmekosea mjipange upya! Hizo ndio faida na hasara za siasa
 
Back
Top Bottom