CUF kwa nini tumefanya vibaya sana katika uchaguzi mdogo wa Igunga

Mtatiro,wewe ni kiongozi mvumilivu.Tatizo kubwa mlilokuwa nalo ni kuwaandama Chadema kama vile wao ni watawala na kuiacha CCM.Wenzenu Chadema waliepuka mtego wa kuwaponda ninyi.Hilo ndilo lililothibitisha kwamba nyie ni CCM B
 
Umeongea vizuri kaka, kuhusu kukubali matokeo. Lakini kama mwanasiasa mwenye matumaini kwa siku zijazo lazima uangalie kwa nini mmeshindwa. Mimi binafsi nilipoona CUF wako katika muafaka na CCM kwa upande wa Zanzibar nilitambua kwamba itakuwa vigumu kwao kuingia katika uchaguzi (hasa kwa upande wa bara) na kushinda. Kama mngetambua mapema kwamba mmepoteza umaarufu Igunga mngewaunga mkono CDM.Lakini sijui kama hilo linawezekana kwa siasa za sasa maana sie tulio mitaani huwa tunaziona tofauti zenu kuanzia bungeni.
 
hold on bro.....,
you have done your job! im sure mtafanya tathmini na kurekebisha mlipojikwaa.
 
Iweje CUF ifanye vibaya hivyo katika mkoa anakotokea mwenyekiti wake wa kitaifa ndugu Profesa Ibrahimu Lipumba? Yafaa tujitazame upya kama chama maana hii si dalili nzuri kwetu. Tumepoteza mvuto? Kwanini? Nini tufanye ili kurudisha heshima na imani ya wanachama na wanachi kwa chama chetu? Hii ni homework kwako Mtatiro na timu yako!
 
Watanzania waleo nitofauti sana na wa mwaka tisini......

Swala la DC na Bakwata limechangia sana anguko la CUF na hii kwa sababu Hamkuthubutu kukemea CCM walipo ona bora CUF ishinde lakini sio CDM kwa kuwa rubuni Bakwata wawa katae CDM wananchi wakawa soma vizuri

Ndoa yenu na CCM mpaka mkapea Choppa Pia ilisomeka vizuri......

Siasa Zakidini zimechangia Angukola CUF kwani watu wenu waliona bora wa unge mkono CCM ishinde wakawanyima kura na haya wenziowalijadiri Msikitini wewe huna taarifa......

Dhambi yenu ya udini na unafiki wa kisiasa ume waponza CUF kuwa tukana na kuwa ponda CDM ni sawa na kujipaka kinyesi hili hamkulitambua kwa sababu hamna uwezo wa kosoma majira ya Nyakati.....

Sasa ni mda mwafaka kwa CDM kuingia Zanzibar kwa sababu hakuna chama cha upinzani kwa sasa.......
 
Mmevuna mlichopanda mdogo wangu. Wenye akili tulikwisha liona anguko lenu,na bado linaendelea. Itafika muda hata tambo za kejeri wanazo zungumza akina Jussa na Hamad Rashid zitaisha. Kama bado ndani ya chama chenu kuna watu makini,nawashauri mjikite visiwani,Lindi na Mtwara.
 
"Failure is not falling down, its staying down when you fall.."

Vyama vya upinzani lazima vigundue kwamba kuna one common enemy ambae ni CCM, hivyo basi ni kujipanga na kujiunga pamoja kumuondoa CCM...., tofauti na hivyo, kweli kabisa safari bado ni ndefu

Vita hivi vya panzi anaenufaika ni Kunguru...!!!
 
Lazima Niwasifu CUF kwa siasa zao za ustaarabu. Hongereni Sana Kwa Kuelewa Ni Nini Kimewakwamisha Na Kuonesha nia ya kulimaliza hilo tatizo.

Kazi ya CUF Igunga wameimaliza kwa sababu hata wenyewe walijua kabisa kulikuwa hakuna njia yoyote ya mgombea wao kushinda kwa kupitia sanduku la kura halali. Atakayeona aibu zaidi ni Seif S. Hamad, kujifanya kwenda kukagua miradi Tabora kumbe ni kwenda kupiga kampeni Igunga. Hata hivyo bado anakaribishwa kutembelea na si kukagua miradi Tanzania bara hata kama hakuna chaguzi ndogo.

CUF, hiyo dhambi ya kuingia mkenge kwa CCM itawatafuna sana. Kazi yenu iliyobaki ni kuvuruga tu, lolote na liwe.
Kazi kweli.
 
hold on bro.....,
you have done your job! im sure mtafanya tathmini na kurekebisha mlipojikwaa.
kwi kwi kwi kwi kwi nadhani jitayarishe kuendelea kuwapa ujumbe huu wa matumaini kila uchaguzi utakaofanyika.
CCM group mnachekesha sana. Faraja nyingine ni dhihaka. kwi kwi kwi kwi kwi
 
Kaka Mtatiro. Weka maslahi ya wananchi mbele kuliko ya Chama. Nuia kutumikia kwa dhati wananchi hata kuwa tayari kufa kwa ajili yao.

Maamuzi yako yatokane na utashi huu... Utakuwa umewatendea haki wananchi.... na utakuwa umejitendea haki... You'll succeed for sure..
 
1. mlipoipigia ccm kura kwenye uchaguzi wa spika na naibu wake mlitegemea nn?
2. kukumbatia propaganda zenu za udini misikitini mnategemea nn?
3. kujifanya kuwa mmejikita kwenye ngome yenu pemba mnawafundisha nn watu wa bara?

natamani haya yawakute tena kule pemba 2015, ili chama kisambaratike kabisa!!!!!!! maana kwa sasa CUF ni kirusi kinachozuia mageuzi hapa nchini tofauti na kilivyokuwa hapo awali!! CUF ngangari ilikuwa ngangari kweli!!
 
Lazima nikiri kuwa washindani wetu wakubwa CCM na CHADEMA wametushinda katika uchaguzi mdogo wa Igunga.

Kwa matokeo ambayo nimeyashayapokea kutoka kwenye asilimia 88 ya vituo kwa ujumla tumefanya vibaya sana. Japokuwa tumekuwa na mgombea mzuri sana na tumemnadi kwa kutumia uwezo wetu wote ambao kwa hakika kila mtu ameuona, lakini matokeo hatuwezi kuyageuza.

Ninachojifunza zaidi ni kuwa wapiga kura wengi ndani ya Tanzania bado wanaamini zaidi propaganda kuliko hali halisi ya mazingira yanayowakabili na hii ikizidi kushabikiwa ndivyo ambavyo wananchi watakosa fursa bora siku za mbele.
Ikiwa hali hii itaendelea hivi ina maana bado nchi ina safari ndefu ya kufikia demokrasia ya kweli na maendeleo yatakayoonekana kwa macho.

Katika uchaguzi huu wa Igunga CUF tumepambana na changamoto kubwa ya kujibu propaganda zilezile kuwa eti "Sisi ni CCM B", kila tulikoenda tumekutana na kikwazo hiki, tumejaribu kwa dhati kuwaelimisha wananchi bila mafanikio na muda umekuwa ukikimbia kuliko upepo.

Hata hivyo bado naamini kuwa tutapata fursa kubwa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni. Mimi na wenzangu hatutakata tamaa kwani MAFANIKIO KATIKA NYANJA YA SIASA huhitaji mioyo migumu.

Natambua kuwa uongozi ni dhamana nzito inayohitaji kujipanga zaidi na zaidi, Na CUF itazidi kujipanga zaidi na zaidi na kila tutakapoanguka tutanyanyuka na kuanza safari, hakika TUTAFIKA.

Chama changu kinakabiliwa na changamoto kubwa sana mbele ya safari na kwa hakika inahitaji tuzidi kujipanga na kujiimarisha. Kama chama hatutajilaumu kamwe, tumeonesha uwezo mkubwa na kufanya kampeni sahihi tukiwa na mgombea wa kiwango kizuri kwa mpiga kura yeyote anayehitaji kiongozi. Lakini kusimamisha mgombea mzuri na kufanya kampeni nzuri wakati mwingine siyo sababu ya kufanya vizuri. Maamuzi ya nani awe mbunge, ni mzuri au mbaya, anafaa au hafai yako kwa wananchi.

Wananchi wa Igunga tunawashukuru kwa namna walivyotuunga mkono na tunawaomba wawe kitu kimoja katika kuiendeleza Igunga yao kwani mshindi akishatangazwa yeye ni mbunge wa wananchi wote. Vyama vyetu hivi vipo ili kuisaidia jamii kupata kiongozi mzuri tu, nasi kama chama tumetimiza wajibu wetu.

Mimi kama kiongozi wa ngazi ya juu wa CUF - Tanzania Bara(Bila kujali nimekuwa kiongozi wa ngazi ya juu miezi minne tu iliyopita tu) nabeba dhamana kwa matokeo yote tuliyopita, najitwika mzigo wa kusimama imara kuiimarisha CUF. Sitatoka CUF na kukimbilia kwenye
vyama vyenye nguvu Tanzania bara kama CHADEMA n.k. eti kwa sababu tu CUF imefanya vibaya kwenye uchaguzi. Ninaamini katika CUF na nitaisaidia Tanzania yangu nikiwa CUF, ninaamini siku moja wakati CUF imeimarika nitatajwa kati ya watu ambao hawakukata tamaa na hawakuyumbishwa na magumu yaliyowakabili na walisimama kidete kwenda mbele.

Tunawashukuru wale wote waliotuunga mkono katika uchaguzi huu na wale wanaotuunga mkono siku zote na wale watakaotuunga mkono siku zijazo. Kwa hakika wote tunawashukuru sana na CUF itasimama imara.

Mungu awabariki sana.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu,
Chama Cha Wananchi - CUF,
Tanzania Bara,
02 Oktoba 2011,
Igunga - Tabora.

Nakushukuru sana ndugu yangu kwa maelezo yako. Naamini umeandika maelezo haya kukidhi ombi nililotoa katika thread ya 'Baada ya uchaguzi Igunga, CUF itoe maelezo kwa wanachama wake'. Naomba nicomment yafuatayo japo kwa uchache..

1. Umesema kuwa mmepambana na changamoto ya propaganda ileile kuwa ninyi ni CCM-B.. Naamini unajua mnaitwa CCM B kutokana na matendo yenu kadhaa, makubwa ikiwa ni kuungana na CCM katika SMZ, lakini kubwa zaidi katika maamuzi na chaguzi kadhaa bungeni. Je, kwa maoni yako, unadhani sasa umefika wakati wa ninyi kuipinga CCM kwa vitendo zaidi? Je unadhani maamuzi mliyochukua kuungana na CCM huko Zanzibar na bungeni yalikuwa na mapungufu, na kuwa sasa ni wakati wa kuyaangalia upya?

2. CUF kimakuwa moja ya nyama tegemeo kwa wananchi wa TANZANIA nzima. Hatua ya CUF Zanzibar kujiunga na CCM katika SMZ inachukuliwa kama ni kuwasaliti wapenzi wa CUF wa Tz bara ambao bado wanaiona CCM kama adui yao mkubwa kufikia maendeleo. Je, nini maoni yako na unadhani mtafanya nini kurudisha imani mwa wananchi ambao wanaamini CUF Zanzibar na CUF bara sio kitu kimoja tena, kutokana na kuwa na status tofauti?

3. Ndugu Mtatiro unaposema "unaamini" mtapata fursa ya kuwaelimisha wananchi siku za usoni, huoni kuwa kauli yako inaonekana kama mtu asiye na uhakika? Unaweza ukatoa mfano wa fursa mnayoweza kupata hasa ikizingatiwa kuwa pamoja na nguvu, juhudi, na utaalamu wote mliokuwa nao Igunga 'hamkueleweka'?

4. Nimefurahishwa na moyo wako hapo uliposema 'hakika tutafika'. Unadhani matokeo ya igunga yanawapa msg kuwa 'kama mnataka kufika inabidi mbadili muelekeo?

5. Unakiri mwenyewe kuwa CUF kinakabiliwa na changamoto kubwa mbele ya safari. CCM waliliona hilo katika chama chao na wakaamua kujivua gamba. unadhani CUF imefika wakati nanyi mjivue gamba? Je, nikikuambia kuwa gamba lenu ni kuonyesha mrengo unaounga mkono CCM utakataa?

6. Ulipotoa mfano wa vyama vyenye nguvu Tanzania bara (naamini umeweka neno bara ukiwa na sababu maalumu), umekitaja CHADEMA peke yake. Binafsi nachukulia na naelewa kama unatambua kuwa kwa sasa Tanzania chama chenye nguvu ni CDM peke yake, na sishangai hukuitaja CCM, sio?

7. Umesema huwezi kuhama CUF eti kwa sababu TU chama cha CUF kimefanya vibaya katika uchaguzi. Neno 'tu' linanipa moyo kuwa kama litakuwepo tatizo jingine unaweza ukahama. lakini unajua kuwa kufanya vibaya ni zao ambalo limetokana na mbolea za aina tofauti, na kuwa kama sio hizi mbolea basi hili zao lisingekuwepo? Je, utakapogundua kuwa ni vigumu kuondoa hizi mbolea (sababu) zinazofanya CUF ifanye vibaya, utakuwa tayari kuunganisha nguvu na wapambanaji wengine?

8. Je, unafahamu kwamba we una kipaji cha kuwakomboa watanzania dhidi ya udhalimu wa ufisadi? unadhani CUF ni silaha sahihi kwa sasa katika kuwakomboa watanzania?

Ukitoa majibu kwa maswali haya nitakupa ushauri ambao kweli CUF mkiufuta, mtafanikiwa sana katika siasa za Tanzania.
 
Pole sana kijana! Ule mtaji vipi tena! Si mlisema ni 11000? Nadhani mtaji kwa sasa unaweza kubaki 110. Sasa ni muda wa kujikita huko pemba huku bara kwishney! Kwa mantiki hiyo CUF hamna haja ya kuwa na naibu katibu mkuu bara.upo hapo! Teh teh teh teh teh
 
Gordon Brown wa labour chama chake kilipoluzi vibaya alifanyaje? Tanzania tuwe wazalendo kwa nchi yetu katika taasisi tulimo kuna performance appraisal kama hii ya matokeo ya uchaguzi sasa kwa poor performance kama hii lazima uwe responcible, katika taasisi hizi kuna watu wengi hawajapata nafasi kuonesha uwezo wao, hebu tuwe kama Japan ambako prime minister earthquake(natural disaster) tu anajiuzulu sisi matokeo ya sera mbovu tunapongezana? What a shame is this? Hatutaendelea kamwe kama watu kwenye taasisi hatutakuwa responsible na actions zetu.
 
mtatiro kutaka kuinyanyua tena kafu ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kwa sababu kizazi hikihiki kilichowakataa, labda kwa ushauri kidogo, vunjeni ndoa yenu na magamba labda watu wanaweza kuwasikiliza,otherwise unajipotezea mvuto kwani muda haukusubiri,ukistuka utajikuta thamani yako kwiiiiiiiisha afadhali ya mrema, time is money
 
Chukua maamuzi magumu mjomba wake Deo wa UDSM pale... NENDA CHADEMA u will become a great politician... These are the number of the times...! Afterall politicians seek a better future through doing politics... fanyafanya uwakimbie hao wapemba na kuna channel kibao ukiwa CHADEMA.. Don't go to CCM its dying now
 
zilikuwa hesabu rahisi hata mtoto mdogo angelitambua hilo kwa nini walizipata wala cuf hawakuhitaj kujidhalilisha kwenye media
 
Ni maneno ya kiungwana kabisa kukubaliana na ukweli. Hata hiyvo, ndg. Mtatiro bado kazi unayo kama kweli chama chenu kinayo dhamira ya kufanya siasa hapa Tanzania Bara.

Kama ulivyodokeza hapo juu, hakika u-CCM B itakuwa kazi kubwa na ngumu kuuondoa katika fikira za wananchi, hasa ukizingatia namna ambavyo CUF imekuwa ikifanya siasa zake kwenye viwanja vya mapambano. Mathalani, tuliona mvutano mkubwa sana mwanzoni mwa mwaka huu kule Bungeni wakati wana-CHADEMA walipotoka nje wakati Kikwete akihutubia. Tukaona pia jinsi CUF ilivyofanya siasa chafu za kutoka nje na kufanya 'lobbying' ili kuwe na kambi ndoyo ya upinzani Bungeni baada ya mazingira yaliyokuwepo kuwafanya CHADEMA washindwe kuwahusisha kwenye kambi rasmi.

Hakika kutoshirikishwa kwa CUF kwenye kambi rasmi ya upinzani kilikuwa kiashiria kizuri tu kwenu kuweza kujipanga na kuondoa wingu lililokuwa limetinga kiasi cha kuwafanya kuwa mbali na wananchi, hasa linapokuja suala la kuaminiwa kama chama cha siasa chenye nia ya dhati kupingania ukombozi wa wengi. Umetamka mtafanya muwezavyo kuweza kutuelewesha wananchi kuhusiana na ndoa yenu na CCM hadi kupata jina jipya la CCM B, sijajua mtafanyaje hasa ili hatimaye sisi wananchi tuwe na mtazamo tofauti uliochanya kwenu.

Hebu niulize swali kidogo:

Tumeona marais kadhaa barani Afrika wakiwateua wake zao kuwa moja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri kwa nchi wanazoziongoza (mfano, Yoweri Kaguta Museven na Bingu Wamsarika). Kwa kuzingatia mazingira ya siasa ndani ya nchi hizo, hivi, Rais atamwajibishaje Waziri aliyemteua (mke wake) endapo ataenda kinyume na taratibu za utumishi wa umma wakati ni mwanafamilia? Nimeuliza swali hili makusudi nikifananisha na makubaliano yaliyopo kati ya CUF na CCM kule Tanzania Visiwani. Itawezekanaje, CUF kama chama pinzani kikakiwajibisha kwa dhati CCM hata kama kuwajibika kwake kunaihusu Tanzania Bara (kama ingetokea hivyo)? Ni maswali magumu kuyauliza hasa ukizingatia hali ya siasa ilivyokuwa tete kule Visiwani Zanzibar, lakini pia tusisahau umuhimu wa suala la uwajibikaji kwa vile ni muhimu sana na kimsingi, chama chochote pinzani hujinjenga kwa kukikosoa chama kilichopo madarakani. Nyinyi CUF mtawezaje kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha na bado isiathiri ndoa yenu?

Binafsi nakutakia kila la heri wewe na chama chako.
 
Back
Top Bottom