CRDB yaamuriwa kumlipa Zawadi Bahenge milioni 300 kwa kutumia picha yake kwenye matangazo bila ridhaa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,508
8,128
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiamuru Benki ya CRDB kumlipa fidia ya Sh300 milioni Zawadi Bahenge kwa kutumia picha yenye sura yake kwenye matangazo ya kibiashara bila ridhaa yake.

Pia mahakama imeiamuru benki hiyo kuondoa picha zote za balozi huyo wa Tacaids kwenye mabango yake ya kibiashara yaliyosambazwa nchi nzima.

Mahakama imefikia uamuzi huo katika hukumu iliyotolewa jana Aprili 30, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu, Rahim Mushi, katika kesi ya madai aliyofungua Bahenge dhidi ya benki hiyo akiilalamikia kwa kutumia picha yake kwenye matangazo ya kibiashara katika kampeni ya ‘Tupo kuijenga biashara yako’ bila ridhaa yake.

“Ifahamike kutumia picha ya mlalamikaji kwenye matangazo ya kibiashara umeingilia faragha yake bila ya ridhaa yake,” amesema Hakimu Mushi katika hukumu hiyo na kuamuru.

Zawadi Bahenge_CRDB.png

Wakili wa kujitegemea, Ferdinand Makole akiwa na Zawadi Bahenge baada ya kutolewa hukumu ya kesi ya madai ya CRDB kutumia picha ya mteja wake (Bahenge) bila ridhaa yake.​
 
What if CRDB wakagoma kulipa hicho kiasi cha fedha kwa mlalamikaji? Wanasheria wabobevu majibu?
Anaenda kukazia hukumu na mali za CRDB zenye thamani hiyo zitakamatwa zipigwe mnada.

Ama akaunti mojawapo ya CRDB itazuiwa ili kiwango cha fedha kinachodaiwa kilipwe.

Kuna madalali wa mahakama hao ndo hutumika kutekeleza hukumu za mahakama kwenye kesi za madai.
 
Anaenda kukazia hukumu na mali za CRDB zenye thamani hiyo zitakamatwa zipigwe mnada.

Ama akaunti mojawapo ya CRDB itazuiwa ili kiwango cha fedha kinachodaiwa kilipwe.

Kuna madalali wa mahakama hao ndo hutumika kutekeleza hukumu za mahakama kwenye kesi za madai.
Shukrani...
 
Back
Top Bottom