Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Ninamashaka kama hii idadi ya wagonjwa inayotajwa sasa haina uhusiano wowote na tamko la WB la kukopesha nchi zilizoathirika zaidi na corona.
Hata Mimi Nina mashaka na idadi ya waliopona aliyoitaja waziri leo Kama haina uhusiano na tamko la Rais Magufuli kuhusu kuwatangaza wanaopona ya kwamba ni wengi!!!
 
"Dar es Salaam lazima kuwe na wagonjwa wengi na vifo vingi kutokana statistically kuna Population kubwa".Hii kauli ni ya Mamlaka

Ukweli huogopesha lakini bora usemwe,Corona maeneo ya Dar es Salaam inamaliza watu, Hakuna mwandishi au gazeti ambalo linaweza kuhoji familia hizi zinazolia kila siku kwa kutowaona wapendwa wao wanaozikwa kimya kimya na Mamlaka

Kauli za kupeana Morali kuwa watu wachape kazi waongeze pato la Taifa Dar es Salaam litamsaidia nani? Hizi familia ambazo ndugu zao wanazikwa kwa kuugua corona zina mateso makali sana.

Watu maarufu na wenye ushawishi kwenye mamlaka na jamii ndio hao wanazikwa na watu wasiozidi ishirini au kumi, Je wewe kabwela ambae hutambuliki na mamlaka omba yasikukute

Uchunguzi ufanyike nini kinachoendelea maeneo ya makaburi ya huko Bahari Beach eneo la kondo,Buza na Mbweni

Uchunguzi ufanyike ongezeko la kelele za ambulance kwa wingi maeneo ya Dar es salaam kutoka hospital kuelekea maeneo hayo ni wangapi wanazikwa kwa janga hili

Tunakubaliana vita inahitaji umorali na nguvu lakini hili ni gonjwa sio vita linahitaji tiba tahadhari na ukweli

Leo hii kuna malalamiko makubwa watu wakifuatilia ndugu zao hospitali waliolazwa wanajibiwa alishafariki na kuzikwa na mamlaka kimya kimya,

Mamlaka imeamuru wizara ya afya ijibu kuwa sio kila mgonjwa hufa kwa corona ni kweli.Je kwanini wanazikwa na mamlaka bila hata ndugu kuhusishwa bali hujibiwa ndugu yenu alishazikwa amefariki

Wizara ya afya ni bora mkaongea ukweli ili watu wachukue tahadhari kuliko sasa mnapojaribu kuuma na kupuliza,

Paul Makonda alikuwa anapuliza na kufariji watu wachape kazi lakini visa vya watu kupukutika na corona sasa amebadili kauli na kuamua kuwa mkweli kuwa Dar corona inamaliza watu

Mamlaka kila siku inakuja na kauli kinzani kama corona sio ishu kwanini mnafunga shule Tanzania nzima, Ruhusuni baadhi ya mikoa elimu iendelee isipokuwa Dar na Zanzibar

Wanakijiji wasiojielewa na baadhi ya wapiga pambio wao hawachuji kauli za mamlaka, Hii itapelekea watu kuwa na morali na kupukutika zaidi
Sasa huu utumbo si yeyote anaweza andika ni 'hear say' ambazo hazina ushahidi wowote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali pamoja na Makapuni ya Simu na taasisi zingine zinazojihusisha na masuala ya kutuma, kupokea na kufanya miamara ya malipo y fedha. Zingekaa pamoja na kuangalia namna ya kusaidia kupunguza gharama kwenye hiyo miamara ili kupunguza kupokea fedha kutoka mikono ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Tujitahidi sote kwa pamoja kupiga vita hivi ili tuweze kuendelea kuona kesho iliyosalama na yenye watanzania walio na afya njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona Ni Mimi na wewe. Kaa home. Fuata masharti. Kama kuna mtu kachukua Malory kukufunga na kamba Utoke. Usafiri. Usivae mask. Then utakuwa Sawa. Na Pole. Otherwise hata huku ulaya masharti Ni hayo anayowaambia waziri mkuu Toka kwa kuwa una ulazima wa kutoka. Safiri kama una ulazima. Mwisho wa siku Sio kiongozi atakayetuua Bali Ni mtu Kama wewe. Una access na taarifa Zote kuhusu corona Lakini unasubiri uambiwe na kusukumwa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Siku ukiugua Corona ndipo utashangaa ni sharti lipi hukulifuata. Wanasema usitukane mamba hali hujavuka mto.

Unadhani wewe unaweza kuwa bingwa kufuata masharti ya kujikinga na Corona kuliko waziri mkuu wa Uingereza au malkia Elizabeth au Prince Charles au yule mheshimiwa mbunge?

Usisahau kuwa ugonjwa huu ungali mgeni sana. Inabidi uanze kujishangaa mwenyewe kama wewe unataka kutuaminisha kuwa ati wewe unaujua vyema zaidi.

Hujasikia tiba zingine za kujifukiza zinaweza kuwa suluhu. Tafiti bado asubuhi sana mkuu ndiyo maana labda hata mkuu yungali maabara pale Chatto akihakiki zake za kufukiza.
 
Nimesoma hii post yako..
Wakati nasoma nikategemea utasema familia ya fulani wa sehemu fulani, walikuwa na mgonjwa..fulani.. kwenye hospitali fulani. Amefuatiliwa na taarifa zinaonesha amefariki na kuzikwa katika makaburi unakotaja.

Ni post inasema kitu kikubwa lakini ni hisia tu.
Sasa mkichukuliwa mkathibitishe inakuwa shida baadae, shida ya kutosha tu.

Mkuu hukusikia hairuhusiwi kutaja majina ya watu?

Mkumbusheni na Ummy inaweza kuwa wagonjwa wa Corona hamna mbona majina, picha au video zao hazipo?
 
Mtu kuwa maskini anakosa vitu vingi sana...huwa sio mkweli, mbishi hata kama hajui, jeuri kwenye jambo linalomwangamiza, uelewa na elimu ya mambo ni mdogo sana...kila kilicho cha mrengo wake atakisifia hata asipokuwa na ABC zake.

Jamani corona inaua na inaua kweli kweli.....data zinazotolewa na mataifa makubwa sio kiini macho ni za kweli.

Kwa sifa zetu Bongo na mfumo wa utawala usitegemee utaambiwa kila kitu, kuna siasa nyingi na mapambano ya propaganda za kivita utafikiri tunapambana na adui tunayemuona, hivyo tunamtisha tumejiandaa na mavifaa chungu mzima.

Corona is just around there close to you, ready to hug and kiss very softly....hakuna kelele hata tumtungue kwa mabomu.

Ifike mahali tusema ukweli maana utaponya wengi na kuokoa wengi.

Uzuri na ubaya wa corona haibugui mazee, so we are all in the cycle...hata mabingwa wa kuchukulia poa, itakuja tu ndio wataelewa maumivu ya wengine kwa ndugu zao.
 
Serikali pamoja na Makapuni ya Simu na taasisi zingine zinazojihusisha na masuala ya kutuma, kupokea na kufanya miamara ya malipo y fedha. Zingekaa pamoja na kuangalia namna ya kusaidia kupunguza gharama kwenye hiyo miamara ili kupunguza kupokea fedha kutoka mikono ya mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Tujitahidi sote kwa pamoja kupiga vita hivi ili tuweze kuendelea kuona kesho iliyosalama na yenye watanzania walio na afya njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini pesa yetu haiwezi kusambaza virusi vya corona,au BOT wamefuta barua yao
 
Mtu kuwa maskini anakosa vitu vingi sana...huwa sio mkweli, mbishi hata kama hajui, jeuri kwenye jambo linalomwangamiza, uelewa na elimu ya mambo ni mdogo sana...kila kilicho cha mrengo wake atakisifia hata asipokuwa na ABC zake.

Jamani corona inaua na inaua kweli kweli.....data zinazotolewa na mataifa makubwa sio kiini macho ni za kweli.

Kwa sifa zetu Bongo na mfumo wa utawala usitegemee utaambiwa kila kitu, kuna siasa nyingi na mapambano ya propaganda za kivita utafikiri tunapambana na adui tunayemuona, hivyo tunamtisha tumejiandaa na mavifaa chungu mzima.

Corona is just around there close to you, ready to hug and kiss very softly....hakuna kelele hata tumtungue kwa mabomu.

Ifike mahali tusema ukweli maana utaponya wengi na kuokoa wengi.

Uzuri na ubaya wa corona haibugui mazee, so we are all in the cycle...hata mabingwa wa kuchukulia poa, itakuja tu ndio wataelewa maumivu ya wengine kwa ndugu zao.
Umasikini ni mzigo
 
Linakagua makaburi na kuhoji wanaofufuka bila kibali maalum.
Wamekufa kumi tu. Hizo picha na videos mtandaoni mzipuuze, ni za mabeberu wanaotaka nchi isitawalike.

Hata lile lory la manispaa lililoandikwa Dar City Council burial services sio la serikali, hata Kama Lina namba SU.

Mkiliona linaranda randa maeneo ya makaburi mlipuuze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom