Conspiracy Theory (MIND SPINNING): Sheikh Ponda Issa Ponda hajapigwa na Polisi

lane

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
897
492
Hello Great Thinkers wa JF,

Kwanza natanguliza samahani kwa yeyote nitakayemkwaza na title yangu pamoja na content ya thread yangu. Niseme tu kwamba hilo sio kusudi langu. Lakini wanajamvi naomba mnivumilie na kunipa nafasi na kusikilizwa japo kidogo kwani nia na maudhui ya mada yangu pamoja na dhamira yangu ni njema kabisa, hasa kwa ajili ya amani ya nchi yangu na pia umoja, mshikamano na upendo kwa watanzania wote.

Sasa katika kutafakari swala zima linalohusu sheikh ponda, nimejikuta nina maswali yasiyo na majibu ambayo naomba niwashirikishe nanyi nyote, na kama kuna mwenye jibu anisaidie:

Kuhusu kupigwa "risasi" kwa sheikh ponda na "polisi", which is what made known to the public hadi sasa, Najiuliza ya kwamba;

1. Kulikuwa na sababu gani ya polisi kumpiga risasi sheikh ponda? je walishindwa kumkamata sehemu nyingine yeyote - mathalani nyumbani kwake, ofisini kwake au hata kumpa taarifa ya kwamba anatafutwa na polisi na hivyo ajisalimishe yeye mwenyewe? Je, ni kweli walikuwa hawajui alipo? Je, kama jibu la hili swali haliko wazi kwa nini tusiamini ya kwamba polisi am serikali kwa ujumla wana agenda nyingine nyuma ya hii? Na je agenda hiyo inaweza kuwa ni ipi?


2. Tukifanya assumption kwamba walikuwa hawajui alipo untill alipojitokeza Morogoro, which by itself ni ngumu kumeza; sasa swali ni kwamba kwanini polisi na maafisa usalama hawakumsubiri mpaka amalize mhadhara wake na pengine kwenda kule msikiti wa mungu moja dini moja huku wakimfuatilia kwa karibu hadi kumkamata kiurahisi pasipo kusababisha taharuki? Kwanini wamkamate mbele ya mashabiki na wafuasi wake? Badala yake waliamua kufanya in a public place tena operation iikiongozwa na afisa mkubwa wa jeshi la polsi kamamda shigolile ambaye naamni anafahamu fika impact ya uamuzi wake, kwa jeshi la polisi na serikali.


3. Toka jana jioni baada ya kupigwa risasi alikuwa wapi? huduma ya kwanza alipata wapi?. Kwa ufahamu wangu mimi a penetrating chest injury hasa ya risasi ina hatari ya kusababisha lung collapse, bleeding na hadi ashindwe kupumua vizuri na kifo kunyemelea fasta. Sasa mbona habari toka itoke kuanzia jana hadi leo ndio wanatuambia yupo muhimbili. And again muhimbili, note that, I said Muhimbili.


4. Inakuwaje mtu ambae anatafutwa na state organs na ambaye usalama wake uko hatarini, he is 'the most wanted' aamue tu kujipeleka muhimbili. Huko si ndo atakamatwa kiurahisi kabisa kama kuku anayesubiriwa arudi jioni baada ya kutwa nzima kuruka ruka na kukataa bosi wake asimle nyama?.


5. Je, hakuna hata mtu mwingine yeyote aliyejeruhiswa japo kiduchu tu au hata kuuwawa na risasi za polisi ambayo bila shaka walipiga risasi randomly ili kuwadhibiti wafuasi wa ponda ambao tunaambiwa na jeshi la polisi walikataa kiongozi wao asikamatwe? mbona hakuna, hakuna taarifa wala tetesi. Hii inawezekana kweli? maanake tunaambiwa kulikuwa na risasi za moto, mabomu ya machozi etc

6. Ndani ya muda mfupi (kumbuka tukio lilitoka mida ya saa kumii na mbili and ushee) vyombo vya habari vya ulaya hasa Uingereza vilipata taarifa ya kupigwa risasi sheikh ponda na to my surprise RPC shigolile alikubali kuhoji haraka na akathibitisha kwamba ni kweli wao polisi ndio waliokuwa wanamtafuta ponda na amepogwa risasi japo kakimbia. Lakini huku nyumbani, polisi kupitia msemaji wao advera wameshakataa hawahusiki. sasa sijui tumwamini advera ambaye yupo ofisini akisubiri taarifa au kamanda shigolile ambae alikuwa frontline.

7. haya mambo yametokea baada ya wale wasichana volunteers wa uingereza kumwagiwa tindikali, je serikali inataka kufanya hiki kiini macho ili kuwaridhisha wakubwa? may be be this is something again, but I dunno

8. Swali la mwisho na la kizushi ni kwamba toka lini seriali imekuwa against na ponda and the like? Je, hawa si wamekuwa wakitoa hate speech na kuhatarisha uvunjivu wa amani lakini serikali imeweka pamba masikioni? matokeo yake watu wamechomewa makanisa, mapadre, wachungaji kuumizwa na wengine kuuwawa at the same time hata pale ambapo evidence isiyo na shaka inaonesha kwamba chuki ya udini inasambaa bado serikali haikuchukua hatua. Sheikh ponda alitajwa moja kwa moja lakini bado yupo na anadunda. Leo imekuwaje tena serikali hiyo hyo ghafla iamuae kumpiga risasi kama jambazi sugu na hatari? mhhh hapa inakataa kuingia akilini


9. Mashuhuda wa tukio hili walionekana kutoa stori ndefu na detailed yenye kuelezea matukio kwa uafasaha tena wakipangilia na kuwasliasha mada vizuri. Katika hali ya panic ya tukio kama hili huwa unapata some sort of amnesia mpaka ukisha-cool off ndio unaanza kukumbuka matukio kidogo kidogo.


In summary maoni yangu ni kwamba Sheikh Ponda Issa Ponda - Hajapigwa risasi bali hii ni mind spinning ya dola ili kuondoa focus kwenye mambo ya msingi yanajitokeza kila uchwao mfano swala la madawa ya kulevya, usalama katika uwanja wetu wa JNIA, tindikali kwa wale binti wa volunteers wa Uingereza etc.

Na kwa kuwa tangia hapo tayari zipo tension ya kidini iliyobuniwa na kuratibiwa na serikali kama namna ya divide and rule machanism ya chama tawala na serikali yake wameona njia mojawapo ya kutuliza munkari upande mmoja wa dini ambao wanaona wanaonewa na serikali na dini nyingine kupendelewa ni kuratibu what I call a pure daytime bluff.

This whole saga is planned kati ya serikali na ponda mwenyewe anaweza akawa anajua kila kitu japo sina uhakika. Haya ni maoni yangu, nakubaliana na wewe kama hautakubaliana na maoni yangu lakini nakaribisha input, crtique na matusi

asanteni
 
nani hajui polisi ni wapiga risasi wakubwa?acha kupoteza uhalisia jipange,polisi wanaoua wanachadema ndo hao hao wanaopiga risasi,usilete hadithi za sungura na fisi
 
nani hajui polisi ni wapiga risasi wakubwa?acha kupoteza uhalisia jipange,polisi wanaoua wanachadema ndo hao hao wanaopiga risasi,usilete hadithi za sungura na fisi

Mkuu Ousofia I get you, napata point yao pia LAKINI jaribu kutafakari zaidi ya hapo, hebu jaribu kupitia hayo maswali yangu hapo juu na tafakari japo kidogo halafu nipe majibu. Usijibu kwa jumla jumla tu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ousofia I get you, napata point yao pia LAKINI jaribu kutafakari zaidi ya hapo, hebu jaribu kupitia hayo maswali yangu hapo juu na tafakari japo kidogo halafu nipe majibu. Usijibu kwa jumla jumla tu.
mazingira yote yanaonyesha polisi ni wahusika
 
kulingana na matukio ya kulipuliwa na mabom kupigwa risasi watu mbele ya polisi, na uchunguzi kuwa wa kisiasa na usio na majibu ya kitaalamu.

100% naamini polis ndio wahusika moja kwa moja.!!
 
Mkuu ficha UPUMBAVU wako sio hekima yako. Ulicho kiandika hapo ni hisia zako za kiudini zilizo wazi huna lolote.
 
Viingereza kibao... Ili utupoteze tu huku ile hali ukweli unaujua,kwahyo ponda fructure aliyopata kajivunja mwenyewe?Acha upumbavu wako kilaza wewe

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
lane,
umeonesha udadisi usio wa kawaida. Umejuaje hii drama? Muasisi mkuu wa udini ni ssm, akamuambukiza cuf, sasa ndio wanaanza kutuchanganya ubongo wetu ili tupotezee. Nasema, msitupoteze, tunajua mnakotupeleka. Kama kamanda Shilogile hajapinga kuwa ni yeye aliyesema kuwa kampiga risasi Ponda, iweje ageuke huyu huyu aseme Polisi hawahusiki? Iweje risasi tena risasi baridi ipenye katikati ya umma imtungue Ponda tu tena begani, jamani, tungeni movie yenye kichwa. Wadanganyika hawapo tena. Tendeni vyema tu. Msituondoe kwenye thread kuu. Sembe imepata mfuniko, mauaji ya padre yamepata myeyusho, sasa baasi huu ni upepo, utapita tuu. Janja ya nyani hiyo. Njii hiii! Kila kukicha, afadhali ya jana. Wiki hii haiishi kabla mitambo ya vituko haijaibua kituko cha kufunika hili. Just mark may word
 
nakubaliana nawe mkuu, tumekuwa watu wa matukio, na serekali yetu sikivu inalijua hilo! kunapokuwa na tension wana tafuta matukio ya kututoa huko! sioni tofauti ya hii ya jana na ya babu wa loliondo!
 
Hello Great Thinkers wa JF,


3. Toka jana jioni baada ya kupigwa risasi alikuwa wapi? huduma ya kwanza alipata wapi?. Kwa ufahamuw wangu mimi penetrating chest injury hasa ya risasi ina hatari ya kusababisha lung collapse, bleeding na ashindwe kupumua na kifo kunyemelea fasta. Sasa mbona habari toka itoke kuanzia jana hadi leo ndio wanatuambia yupo muhimbili kwa sasa.


haya ni maoni yangu, nakubaliana na wewe kama hautakubaliana na maoni yangu lakini nakaribisha input, crtique na matusi

asanteni
lane

Hivi Mjinga akitwa Mjinga anakuwa ametukanwa ?

au pinda alipoitwa --------, je alitukanwa au alisifiwa?

Wewe mimi nakuita MJINGA na ndicho unachostahili.

attachment.php

IMG-20130811-WA0011.jpg IMG-20130811-WA0008.jpg
 
lane, unaweza kuwa na point, hao wanaokupuuza ni wavivu tu wa kufikiri.
Vyombo vya habari vya magharibi vime capture hilo tukio mapema mno na katika hali ambayo inaweza kutafsiriwa kama wamekuwa appeased na hatua ya kupigwa risadi kwa Shehe ponda.

Inawezekana kabisa ikawa ghilba iliyopangwa kiustadi ili kuwapoza wamagharibi kufuatia kumwagiwa tindikali kwa watu wao.
 
Kwa hiyo wewe lane unataka kusema ponda kajipiga mwenyewe risasi au????sijakusoma mtoa mada

Mtoa mada ana hoja.Kutokana na Nchi yetu kuwa Uchi ni rahisi kwa Majasusi wa Nchi zingine kuingia na kufanya hujuma.Mfano wale Mabinti waliomwagiwa Tindikali Zanzibar wana nasaba na Israel;Hujuma za Israel zinajulikana Duniani kote.Vilevile Rwanda ina watu Kibao humu nchini na Generali Kagame alishatoa lugha ya Vitisho kwa hiyo lolote linawezekana.
 
Ponda fiksi tu huyu. Sasa pale alipo Muhimbili kwanini wasiende wakampiga pingu!?
 
Back
Top Bottom