platozoom
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 9,372
- 11,176
Ni mod anayependa sana kujibu kwa kizungu hata kama umemuuliza kwa Kiswahili. Tulimwajiri miaka 5 iliyopita na tukampa "Terms and condition", na alituvutia kwa sababu alituambia yeye ni msomi wa kiwango cha shahada ya uzamivu, (Kwa wapenda kizungu hiyo ni P.H.D yaani Pure Head Damage).......
Na zaidi ya hapo akatwambia yeye ni shombeshombe au Suriama yaani kachanganya damu: Baba Mmarekani na mama Mgiriki, na pia amerudi DAR na kuishi Masaki. Haikutupa kazi sana kumkubalia kwa sababu alikuwa anatema ngeli si mchezo.
Sasa tatizo liko hapa, tumegundua kwamba alitudanganya........Kwanza si shombeshombe wala mboshemboshe pili hana hiyo PHD tatu haishi Masaki
Kifupi ni mzaramo wa Maneromango, mama yake alizaliwa Kimanzichana na kwamba anaishi Mwananyamala kwa Kopa na kuwa elimu yake ni Darasa la saba alilomaliza kwa taabu sana mwaka 1989.
Mtaanza kusema kiingereza kajulia wapi........Kifupi tumegundua alishawahi kufanya kazi kwa Mzungu mmoja maeneo ya Mbezi miaka kadhaa iliyopita, na huko ndipo alipojulia Ung'eng'e.
Kwa hiyo msione kila mkimuuliza kwa Kiswahili anawajibu Kiingereza ni kwa sababu kama mnavyofahamu "Mswahili akipata................"
Wasalaam platozoom
Note: Comment at your own risk terms & condition applied