CONFIDENTIAL: TANESCO, RICHMOND, DOWANS and BoT

Mapendekezo ya Ludovick Utouh ni uji mwepesi...

Anabainisha matatizo lakini hapendekezi hatua za kisheria kuchukuliwa wote wale ambao wamehusika katika ufisadi huu. Kama anaweza kujua makosa, yawaje ashindwe kuwataja wahusika jina baada ya jina na kubainisha ni makosa gani ya kuhujumu uchumi wameyafanya na wanapaswa kuchuliwa hatua gani?

Tatizo hapo ni kuwa ofisi ya CAG haiko huru na ndiyo maana Utouh anatoa majibu mepesi ya kumsaidia JK kufunika mashimo makubwa kama haya. This is why we need a new constitutional order to deal with all issues that are weakening our institutions of governance...

Haya mazingira ambayo Utouh kayabaini yatasaidia kwenye kesi ya kukataa kuwalipa DOWANS ya kuwa ile TUZO was fraudulently extracted.........and therefore can not be honoured in light of our own laws.....

Tatizo ni nani ana jukumu uteuzi wa huyo Utuoh?...ni Rais...na nani kampa Rais urais?....sitajibu hili kwa sasa vile nyote mwajua....mapendekezo na maagizo ya INTOSAAI ambayo husimamia Ma-Utuoh wote duniani ni kuwa CAG anatakiwa ateuliwe na BUNGE na awajibike kwa bunge....Tanzania inakaidi hili...hata hivyo nampongeza Mwalimu wangu Utuoh kwa kuendelea na kazi yake ngumu...alipoanza hakuwa na mvi kama sasa
 
Invisible shukrani zikufikie!

Nimepitia barua zote kwa haraka lakini nimegota kwenye sehemu nne hivi:

1. Barua ya CAG kwenda MoF kipengele (xi) ambapo Tanesco wanasema "...there was no contract with Dowans as those who signed the contract were not known...". Hapa wana maanisha "those from Dowans" au hata aliyesaini kwa niaba ya Tanesco hakuwa na mamlaka hiyo??

2. Commissioning ilitakiwa iwe imefanyika ndani ya siku 150 ambayo ingekuwa Feb 2, 2007. Dowans wakafunga kimtambo kimoja January na mingine mwezi Oktoba 2007. Hii capacity charge (Jan - Oktoba 2007) waliyoenda kudai ICC na wakapewa ilihusikaje wakati mwenye kudai alipaswa kuwa Tanesco??

3. Demurrage ya Usd 2,430,000 kwa miezi 8 wakati huyu Dowans wewe ulitakiwa kumlipa Tzs 152m/day sawa na Usd101,333/day which makes about Usd 24.3 million kwa hiyo miezi 8. Mbona biashara ya ki-chifu Mangungo?? Kweli Dowans ni brain child wa corridor za Magogoni.

4. Barua ya Balali - BOT ya June 2006 inaonyesha kulikuwa na funds kwa Tanesco kuagiza mitambo yao, mbona haijaagizwa mpaka leo?? Wanapotokea kina January Makamba kusema Dowans lazima iwashwe kwa nini wasishinikize pesa hizi zilete Majenereta yetu. If Dowans were to commision the turbines for 150dys kwa hela ya kuunga unga itashindwaje Tanesco wakati mihela ilikuwa pale BOT provided wamefungua Letter of Credit.

Hawa wazalendo walioko serikalini wenye kutuletea hizi taarifa (konfidensho) wanasaidiaje kuzuia haya.
Kwa nini wasifumue mambo kwa wakati ili watanzania tupinge (kama tunavyopinga malipo kwa Dowans) kabla halijafanyika??
 
Mazingira kama haya hapa chini ya kuwaneemesha DOWANS kwa capacity charges wakati mitambo inafungwa kipindi ambacho wahusika wote wanaelewa hakuna uzalishaji ni uthibitisho zaidi ya kuwa wahusika katika usuluhishi walikuwa wanatetea masilahi yao binafsi.

Read this dissection for your considered mulling over.... Utouh alisahau kubainisha jinsi Msuluhishi alivyosigina sheria yetu ya manunuzi jambo ambalo kama likiruhusiwa kuendelea basi tunajenga misingi ya uvunjaji wa sheria hapa nchini......

CAGletertoPMfinance.jpg
 
mweeeeeeeeeeeeeeee jamani njiiiiiiiii hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii........walipe wenyewe serikali
 
Mie naona haya madudu ni ya Karamagi na Msabaha, na ikiwezekana aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara wakati ule, hawa ni wa kukamata wafungiwe Keko na kesi ni ya KUHUJUMU UCHUMI.
 
Mfumo uliopo hauruhusu uwajibikaji kwa watu wanaolitia hasara Taifa,na bahati mbaya watanzania wengi hawana hata interest ya kujua kwa nini tumekwama kwenye huu umaskini,wenye kutaka kujua wanakwamisha na accesibility ya information..

Kama ilivyowahi kushauriwa hapa jamvini ni wakati sasa wa kutengeneza vipeperushi vya kutoa haya "mabomu" ili wajue serikali yao "inavyojitahidi" kupunguza umaskini..,sasa naelewa kwanini walisema CDM inataka "kupindua" nchi kwa jinsi wanavyowajulisha wananchi nini kinasababisha umaskini wao...
 
Asante sana Invisible.

Haya yote tulishayashisi na labda tulikuwa na fununu kidogo. Sasa umetuwekea mtiririko mzima tena uliopangiliwa vizuri na ushahidi wa kimaandishi. Thanks again

Bado suala moja nyeti - tunaona namna wizara ya nishati ilivyojiingiza katika suala hili na ukigeugeu wake. Mara inaagiza mkataba uvunjwe mara inaagiza mkataba usainiwe. Hapa ndipo ilipo harufu ya wizara ya nishati kupokea shinikizo toka kwa mtu ambaye alikuwa na madaraka juu ya wizara hiyo.

Ni nani na kwa maslahi gani? Nadhani Mwakyembe analo jibu; tafadhali invisible tusaidie kumuona Mwakyembe na Sitta.

Inawezekana hivi sasa si wakati muafaka, lakini naamini muda ukifika wakupe hizo docs. Nakumbuka pale Mwakyembe aliposema kuwa kama wangesema yote, serikali inge......! Mpaka tutegue hapo ndipo suala na richmond litapata ufumbuzi.
 
ama kweli..! WHAT GOES BEHIND THE SCENES KWENYE SERIKALI YETU NI AIBU...!

NDIO MAANA RAIS NA WAZIRI MKUU WANASEMA HAWAJUA UMASKINI WA WATZ UNATOKANA NA NINI..? shame on YOU!
 
Something is serious wrong with this country we all call home.. ...yawaje JK amwagize CAG apeleke taarifa zake Bungeni na kuwachulukia hatua wababdhilifu wote na kwenye DOWANS CAG haoni wa kumwajibisha...ila kwenye local governments na parastatals wapo wengi wa kuwachukulia hatua

.....read this missive for your own clarifications


JK: Ripoti ya CAG iwe bungeni Aprili 12

Wednesday, 30 March 2011
Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete ameagiza ripoti za ukaguzi wa hesabu za serikali za mitaa, za serikali kuu, mashirika ya umma na ukaguzi wa ufanisi kwa mwaka 2009/2010 ziwe zimewasilishwa bungeni ifikapo Aprili 12, mwaka huu.

Ameagiza hilo kupitia barua aliyowaandikia Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo.
Rais katika barua hizo, amewataka viongozi hao kuwasilisha bungeni ripoti hizo za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa muda huo, ikiwa ni wajibu wao kikatiba.

CAG, Ludovick Utouh, juzi aliwasilisha ripoti hizo kwa rais, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, iliyorekebishwa mwaka 2005 na kifungu cha 28 cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma namba 11 ya mwaka 2008.

Kwa mujibu wa sheria, ripoti hizo zinatakiwa kuwasilishwa kwa rais kabla ya mwishoni mwa Machi, naye anatakiwa kuwaandikia barua mawaziri husika ili ziwasilishwe kwenye kikao cha Bunge kinachofuata.

Ripoti hizo zinahusu ukaguzi wa fedha za serikali za mitaa, serikali kuu na mashirika ya umma. CAG pia amekagua ufanisi wa utendaji wa Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika kusimamia ujenzi wa barabara nchini.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, ripoti hizo zimeainisha upungufu unaotakiwa kufanyiwa marekebisho.

CAG pia ametoa mapendekezo yanayolenga katika udhibiti na matumizi bora ya fedha na rasilimali za nchi, ambayo Rais Kikwete ameyaafiki.

Rais amemtaka CAG kuwachukulia hatua wote wanaokiuka taratibu za matumizi ya fedha za umma.
 
Hivi yeye hayumo katika hilo?
Asiwemo achekwe?

Na ndiyo maana baada ya kuichakachua taarifa ya mkaguzi mkuu kuhakikisha ......it sees no evil................is unwilling to discuss nor expose the real evildoers and it recommends petty issues which do not address issues of rampant impunity....

JK has definitely embraced the report that recommends DOWANS should rip-off our Treasury under the auspices of CAG... but no criminal investigations recommended against all perpetrators of this heinous crime against humanity ...shame on JK and shame upon Utouh who is doing all this malfeance to cover his own skin; how selfish this guy has turned out to be...
 
hapa for sure jamaa wa dowans walishalamba pesa zamani sana.Tunasubiri copy ra risiti ya malipo ya dowans.Wakuu wenye kuipata tuwekekee ili tujue mjadala umefungwa.
 
Unapoona PM anataja sababu za umasikini ambazo ndiyo maeneo ya kuchochea maendeleo kama ongezeko la idadi ya watu..........huku Uchina idadi ya watu imekuwa kichocheo cha maendeleo..........na PM hayuko tayari kuzungumzia au hata kukiri ufisadi uliokithiri serikalini ndicho chanzo cha umasikini basi ujue hilo taifa ambalo viongozi wake wanakwepa ukweli na kujitumbukiza kwenye uongo kamwe halitaweza kuendelea..................

Waziri Mkuu aelezea ongezeko la umasikini

Wednesday, 30 March 2011
Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amesema kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu, kiwango kikubwa cha ukuaji wa miji na kiwango kidogo cha ukuaji wa sekta ya kilimo ni miongoni mwa sababu zinazochangia kutopungua kwa umasikini nchini.

Aliyasema hayo jana wakati akifungua Mkutano wa 16 wa Mwaka wa Taasisi ya Utafiti kuhusu Kuondoa Umaskini (REPOA) katika hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku mbili ambao ulianza jana, mada yake kuu ni: "Tija, Ajira na Usalama wa Maisha ya Kiuchumi na Kijamii".

Waziri Mkuu alisema umefika wakati wa kujiuliza utafiti unaofanyika nchini umefanya nini kuleta mabadiliko na kwamba matokeo ya utafiti huo unatumikaje kupunguza umasikini wa Mtanzania na nini kifanyike ili kuondoa hali hiyo.

"Jambo ambalo ni changamoto kwetu ni hoja ya kwamba, pamoja na jitihada hizo, taasisi za utafiti hazijaleta matumaini makubwa, hususan upande wa uchumi… miongoni mwa sababu zinazochangia kutopungua kwa umasikini wa wananchi wengi ni pamoja na kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu ambalo haliendani na kiwango cha ukuaji wa uchumi," alisema.

"Kwa sasa kiwango cha ukuaji wa uchumi ni wastani wa asilimia sita, wakati kiwango cha ongezeko la idadi ya watu kinakadiriwa kufikia asilimia tatu. Kwa mfano, mwaka 2009 Pato la Taifa lilikuwa sh. trilioni 28.2, wakati idadi ya watu ilikadiriwa kuwa milioni 40.7 na hivyo kufanya pato la wastani wa kila mwananchi kuwa sh. 693,185, ikilinganishwa na sh. 628,259 mwaka 2008. Hili ni ongezeka kidogo la asilimia 10.3."

"Kwa kiwango hiki tunapaswa kujiuliza utafiti wetu unatusaidiaje katika kuongeza kwa haraka ukuaji wa Pato la Taifa na hivyo kuongeza pato la Mtanzania mmoja mmoja? Vilevile, tujiulize utafiti wetu unatueleza tutumie sera zipi zinazofaa na ambazo ni 'effective' kuwa na idadi ya watu inayoendana na ukuaji wa Pato la Taifa. Sera za idadi ya watu zilizopo je ni 'effective' au tubadili mwelekeo?"

Alisema taarifa zinaonyesha umasikini pia unasababishwa na kiwango kidogo cha ukuaji wa sekta ya kilimo, takriban asilimia 4.5 kwa mwaka licha ya kuwa kinaajiri asilimia kubwa ya Watanzania.

"Kiwango hiki ni juu kidogo ya kiwango cha ukuaji wa idadi ya watu cha asilimia tatu. Kwa kuangalia kiwango cha ukuaji huo ni dhahiri kwamba tija katika kilimo bado ni ndogo. Kwa misingi hiyo, tunajiuliza utafiti wetu unasaidiaje katika kuongeza ukuaji wa mchango wa kilimo katika Pato la Taifa?" alihoji.

Alisema ukuaji wa miji una changamoto nyingi, ikiwamo shughuli chache za uzalishaji wa viwanda, ikilinganishwa na miaka ya nyuma na ambazo kama zingekuwa nyingi zingewezesha kutoa ajira kwa wakazi wengi walioko mijini.

Kwa mujibu wa makadirio ya idadi ya watu yaliyotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu wapatao 43,187,823 mwaka 2010, ambao kati yao watu 31,809,808 sawa na asilimia 73.7 wanaishi vijijini na watu 11,378,015 sawa na asilimia 26.3 wanaishi mijini.

"Kuongezeka kwa watu mijini ambako kunasababishwa na wengi wao kuhama kutoka vijijini, kunaathiri shughuli za uzalishaji za kilimo katika maeneo ya vijijini na hivyo kupunguza kipato na hatimaye kuongeza umasikini kwa wananchi wa vijijini," alisema.

Hali hiyo, Waziri Mkuu alisema inasababisha wananchi wengi, hususan vijana katika miji kujiingiza katika shughuli zisizo rasmi na kuishi katika makazi duni yanayoashiria umasikini.

"Hili nalo ni tatizo ambalo taasisi zetu za utafiti zinatakiwa ziliangalie kama zinasaidiaje nchi katika kuondokana na hali hiyo. Tuangalie taasisi hizi zinachangiaje katika kuongeza ajira na kuwafanya watu, hususan vijana kuendelea kubaki vijijini na kuacha kukimbilia mijini," aliongeza.

Mapema, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya REPOA, Profesa. Esther Mwaikambo alisema wao kama watafiti wanatambua mchango wa Waziri Mkuu katika kuthamini masuala ya utafiti na umuhimu wa watafiti.

Naye Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Dk. Ad Koekkek alisema tija, ajira na usalama wa maisha kiuchumi na kijamii vina mchango mkubwa katika maisha ya Mtanzania pamoja na usalama wake binafsi, lakini ni lazima viendane na matumizi ya teknolojia.

Alisema maendeleo ya kiteknolojia yaweza kubuniwa, yanaweza kufundishwa vyuoni au kuagizwa kutoka nje ya nchi au mawili kati ya hivyo, lakini kikubwa ni kuona yanamsaidiaje mwananchi kuboresha maisha yake.

"Miaka ya hivi karibuni, serikali imeongeza kwa kiwango kikubwa bajeti ya kilimo… lakini je tumefanya utafiti kuona kama ongezeko hilo limesaidia kuongeza uzalishaji mazao ya mkulima? Je, tumechunguza kuona kama wakulima wana uhuru wa kuchagua teknolojia zinazowafaa? Je, tumefanya utafiti kuona kama serikali inatumia njia sahihi katika kutekeleza mpango huu?" alihoji.
 
Yaani haya mapambano inabidi tuingie barabarani... wanatufanya wananchi wapumbavu sana, ahsante sana Invisible nitatoa pesa yangu mfukoni nipige copy elfu moja ili nizisambaze hizi kwa watu vijiweni na wanafunzi mavyuoni.
 
LUDOVICK Uttouh ameeleza wazi kabisa juu ya jinsi mambo yalivyokuwa, kwahiyo hakuna sababu ya TANESCO kulipa Deni, Wizara ilijifanya inajuwa mambo kwa kulazimisha TANESCO wakubaliane na Wizara itakavyo, wakiwa wanajuwa kabisa kuwa wafanyacho hakiendani na jinsi taratibu, kanuni na sheria zitakavyo na uzuri TANESCO kwa kuwa waelewa walikuwa wakikataa baadhi ya command, lakini mwisho wa siku mambo yameharibika, wizara inataka kujivuwa gamba, heheheheheheh

Wizara lipa deni huna pa kukimbilia
walipe wizara ou shirika bado mzigo wa kuzilipa hizo pesautaenda kwa wananchi
 
Suala la Malipo kwa DOWANS Naona pole pole yanatutoa kwenye Point ya Msingi ambayo Wa Tanzania tunapaswa ku stick on.
Suala ni Dowans Kutokulipwa na sio Nani alipe Tanesco or Govt.

POAC inaposema Serikali ilipe Dowans na sio Tanesco huu ni usanii,suala ni Dowans kutokulipwa full stop.

Its high time now Great Thinkers, kuandika tuu hapa JF Haitoshi, sana sana naweza pandisha hasira na Kushindwa kufanya kazi ofisini vizuri.

Its high time now great thinkers kutoka nje ya JF, Ku demostarte yale tunayoyajadili hapa ndani.....

Lets arrange a date where we gonna meet ili tuweze kuyaweka haya tunayoyaandika into action.

Lets propose date and venue.

Rgds
 
Back
Top Bottom