CONFIDENTIAL: TANESCO, RICHMOND, DOWANS and BoT

Kuna tofauti gani TANESCO kutolipa ikalipa Serikali?. Ikilipa TANESCO ni shirika la umma (Shirika la Watanzania), fedha zake ni za Watanzania.

Serikali inakusanya kodi toka kwa watanzania na kwa niaba ya watanzania wote. Kwa hiyo fedha za serikali ni za watanzania

Hatari pekee kwa TANESCO kulipa ni kufilisika.

Lakini njia zote 2 ni maumivu kwa Watanzania.
 
mmh...kweli Wizara kupitia Karamagi na maswahiba wake walilazimisha mkataba na Richmond na walikiuka masharit ya PPA 2004. Je hiyo kesi Tanesco walikua wapi waieleze ukiukwaji wa sheria hiyo ya manunuzi?
 
Invisible nimefurahi sana.. ukweli uko wazi na tunajua ni kwa nini Wizara iliingilia majukumu ya Bodi ya wakulugenzi wa Tanesco. Walikuwa na maslahi binafsi ndiyo maana wakaita hilo dili liende wizarani. Tanzania ya wadanganyika.
 
Huu ndio ukweli wa mambo.

Wizara walicolude na mafisadi kuua nchi. Hao hao walipe Dowans from their own sources na sio Tanesco. Ngeleja at the centre of this black out should be held responsible at once.

Mkuu Invisible, you rock man...
 
Tunataka WOTE waliopitiwa na hii hela wote WAADHIBIWE kwa kufidia hii hela.

Hela isitoke TANESCO wala HAZINA. Hela yenyewe iko tu katika account za watu hawa hawa.

Naomba kutoka nje ya mada, hivi inakuwaje tunauziwa gesi yetu wenyewe ghali hivi, kwanini tusingechimba wenyewe labda tuweke amangement toka nje?
Mkuu hujatoka nje ya mada; suala la gesi nalo ni suala la kuangalia, linaongeza mzigo mzito kwa TANESCO ilhali inatoka hapahapa kwetu. Inazua shaka kuwa hata tukichimba mafuta bado hali itakuwa mbaya kwa nishati hiyo Tanzania, watakaonufaika ni wachache kwa michezo yao ileile
 
Hapa kuna tatizo, haiwezekana Serikali iingize TANESCO ktk deni ambalo haliihusu, na hii ni kutokana na Serikali kuingilia majukumu ya wahusika waliopewa mamlaka ya kiutendaji, wewe sio TANESCO inakuwaje uingie mkataba kwa niaba ya TANESCO? Sasa yamekushinda unataka Tanesco walipe deni ambalo serikali ndio msababishi wa hilo deni.

Umefika wakati siasa ikae pembeni ktk maswala ya kiutalaamu, wanasiasa tuache kuingilia kazi za wataalamu, matokeo yake ndio haya. Hata sheria ya mikataba hujui leo hii unaenda ingia mkataba na watu ambao wapo kifaida zaidi, hii ni sawa na Chifu Mangungo wa Msovero kuingia mikataba inayotumaliza leo.

Viongozi wa hii nchi punguzeni BLA BLA BLA BLA BLA
 
Namlaumu sana Spika (Mstaafu?) Sitta kwa kutolimaliza hili kama alivyokuwa amelianza. Akalisukumia chini ya busati. Sasa lipatiwe ufumbuzi. Anayetakiwa kuwa jela apelekwe na anayetakiwa kuilipa DOWANS ailipe. Litaitesa CCM vibaya zaidi 2015.
 
Pendekezo lako linaelekea kufanana na la POAC walilotoa; serikali (si TANESCO tena) ndo ilipe gharama hizi!
shuffling from left pocket to the right one....................unless there accountability we are doomed abinitio....................
 
Hapa ndio tunapomkumbuka Sokoine, unakamatwa kwanza, account zako zinafilisiwa, magodown yanafunguliwa, halafu maelezo baadae, ukishapona kisukari huko jela.
 
Hivi Raia kama mimi (kwa niaba ya watanzania milioni 40) siwezi kwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka watu hawa? Naamini ndio walioshurutisha TANESCO kupitia Wizara ya madini na nishati
  1. EDWARD LOWASSA
  2. IBRAHIM MSABAHA
  3. NAZIR KARAMAGI
  4. WILLIAM NGELEJA
  5. ROSTAM AZIZ
Naomba mwongozo wa kisheria
 
Hapa dhamira si kukatishana tamaa, tunataka 'Great Thinkers' tuziangalie kwa umakini hizi nondo na kuja na hoja za kuweza kubadili hali ya nchi. I believe we can, YES we CAN!
Ni kweli Mkuu

Tatizo ni pa kuanzia... waliotuingiza kwenye shida ndio wapo kwenye altare, madhabahuni na kibla!!! na tunatakiwa tuanze na maungamo na kuwapigia magoti ili tusome soma la kwanza, la pili na la tatu


The only solution ni kuwaondoa pale, waje wakae na sisi ndio tuanze hiyo YEs we Can!!
 
Kweli serikali imejaa vilaza, wanasema deni ni la TANESCO na wakati TANESCO ndio waliokataa ku sign mkata wa Richmond (na makampuni mengine 7 yalio bid tender), SERIKALI IKALAZIMISHA TANESCO wa kubali mkataba wa RICHMOND na eventually kuhamishia DOWANS na KULAZIMISHA TENA TANESCO wakubali mkataba na DOWANS.

TANESCO ili fight tangu mwanzo kuepuka haya ma RICHMOND/DOWANS lakini mwenye final say ni BOSS/WIZARA (SERIKALI).....

HAYA; Yote juu hapo ni danganya toto, RA anataka hela YAKE kwa njia yoyote kazi ipo RAIS na wenzake waliowekwa pale na RA kufanikisha madili yake.

Ukiangalia RA anashangilia ,maana mmeingia kwenye mtego wake , wakwamba "NANI ALIPE DOWANS (TANESCO/SERIKALI)" baadala ya "TUSILIPE DOWANS".


RAIS na wenzake wakiamua kuchangisha hela kwa vikombe vya babu, kupandisha bei ya umeme, harambee, minada etc shauri yenu RA anataka hela yake.

SERIKALI ushaidi inao ya wakina nani wamehusika kwa kiasi gani, kuwapeleka mahakamani hawataki/hawawezi. Wananchi wakitaka wawasaidie wanasema wanavuruga amani.

TIME WILL TELL!
 
Mapendekezo ya Ludovick Utouh ni uji mwepesi...

Anabainisha matatizo lakini hapendekezi hatua za kisheria kuchukuliwa wote wale ambao wamehusika katika ufisadi huu. Kama anaweza kujua makosa, yawaje ashindwe kuwataja wahusika jina baada ya jina na kubainisha ni makosa gani ya kuhujumu uchumi wameyafanya na wanapaswa kuchuliwa hatua gani?

Tatizo hapo ni kuwa ofisi ya CAG haiko huru na ndiyo maana Utouh anatoa majibu mepesi ya kumsaidia JK kufunika mashimo makubwa kama haya. This is why we need a new constitutional order to deal with all issues that are weakening our institutions of governance...

Haya mazingira ambayo Utouh kayabaini yatasaidia kwenye kesi ya kukataa kuwalipa DOWANS ya kuwa ile TUZO was fraudulently extracted.........and therefore can not be honoured in light of our own laws.....
 
Jamani ni lini tutampata mkombozi wa nchi hii? Tukiendelea hivi mwisho wa siku hakitaeleweka!
 
Nachelea kumkosoa huyu Ramadhan Khijjah.....haraka sana atapata utetezi....''ati kwa sababu ya dini yake''....lakini hiyo barua yake imeniacha hoi sana...katibu mkuu wa wizara ya fedha ndio huyu kweli anae andika hivi?
 
LUDOVICK Uttouh ameeleza wazi kabisa juu ya jinsi mambo yalivyokuwa, kwahiyo hakuna sababu ya TANESCO kulipa Deni, Wizara ilijifanya inajuwa mambo kwa kulazimisha TANESCO wakubaliane na Wizara itakavyo, wakiwa wanajuwa kabisa kuwa wafanyacho hakiendani na jinsi taratibu, kanuni na sheria zitakavyo na uzuri TANESCO kwa kuwa waelewa walikuwa wakikataa baadhi ya command, lakini mwisho wa siku mambo yameharibika, wizara inataka kujivuwa gamba, heheheheheheh

Wizara lipa deni huna pa kukimbilia
 
Back
Top Bottom