Coastal Union 0-2 Yanga | Ligi Kuu Bara | Sheikh Amri Abeid

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,125
Ni weekend tena. NBC Premier League inaendelea ambapo Wagosi wa Kaya, Coastal Union watashuka dimbani kuwaalika Mabingwa watetezi wa taji, Yanga katika dimba la Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika dimba hilo mwezi wa saba mwaka huu katika mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation ambapo Yanga walibuka na ushindi.

Je leo Juma Mgunda ( Guardiola Mnene) ataweza kuwadhibiti tena Yanga? Tukutane hapa saa 10:00 jioni.

Utabiri wangu: 1-1

=======

00' Kipenga kinapulizwa kuashiria mwanzo wa mchezo, Coastal union VS Yanga

01' Aziz Ki anaachia mkwaju wa kwanzo uliolenga goli, mlinda mlango Mahmud anasimama imara. Coastal union 0-0 Yanga

04' ⚽ Benard Morisson anaandika bao la kwanza kuitanguliza Yanga, akiunganisha pasi maridadi kutoka kwa Jesus Moloko. Coastal Union 0-1 Yanga

07' Yanga wanapata nafasi nyingine lakini Moloko anapaisha juuuuuuu. Mpira uliingizwa kwenye box na Benard Morisson.

10' Yannick Bangala yuko chini baada ya kusiginwa na Juma, nahodha wa Coastal Union. Bangala anamsukuma Juma.

11' 🟡Wote wawili wanapewa kadi ya njano

14' Coastal wanaachia mkwaju wa kwanza uliolenga goli kwa shuti la mkwaju wa adhabu ndogo kutoka kwa Betran, Mshery anakamata mpira barabara.

23' Coasta Union wanafika langoni kwa Yanga lakini juhudi zao zinashindwa kuzaa matunda

25' 🔁 Jesus Moloko ambae kaumia anaenda bench na nafasi yake inachukuliwa na Dickson Ambundo

28' Mabadi anajaribu kufika kwenye lango la Yanga, backline ya Yanga inasimama imara na kuzaa kona isiyo na matokeo.

33' 🟡 Morisson anapewa kadi ya njano baada ya 'kujiangusha' ndani ya box

37' Feisal Salum anaachia mkwaju kutoka nje ya 18, unapaa juuuuuu

40' 🚩Coastal wanapata kona ya tatu na Mrundi wa Coastal anaachia mkwaju mkali unaopanguliwa na Mshery, kona pacha inashindwa kuleta athari

42' Ki Aziz anaachia mkwaju wake wa pili golini lakini bado anashindwa kuanza mkeka wa magoli

52' Aucho anapewa kadi ya njano

53' Coastal wanapata kona tatu mfululizo lakini Yanga wanasimama imara. Coastal union 0-0 Yanga

55' 🔁 Fiston Mayele anaingia kuchukua nafasi ya Makambo upande wa Yanga

57' Maabad wa Coastal Union anaipangua beki ya Yanga lakini Mshery anazuia shambulizi

62' 🟡 Kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze anapewa kadi ya njano

64' 🟡 Mubona anapewa kadi ya njano kwa kuvuta jezi ya Morisson

66' 🚩Aziz Ki anaachia mkwaju wa adhabu ndogo, beki anautoa kwenye njia na kuzaa kona

67' ⚽ Fiston Mayeleeee anaiandikia Yanga bao la pili. Kona ya pili ya mchezo kwa Yanga inazaa goli

71' Coastal Union 0-2 Yanga

71' 🔁 Majimengi anaingia kuchukua nafasi ya Hamza

72' 🔁Farid Mussa anaingia kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao la kwanza, Benard Morisson

88' Kila timu inajaribu kufikia lango la mwenzake, Coastal union 0-2 Yanga

89' Yanga wanacheza wenyewe hapa dimba la Sheikh Amri Abeid

90+3 Mpira unatamatika jijini Arusha, Yanga inazoa alama zote tatu na kufikisha alama sita. Coastal union inasalia na alama zake tatu.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ametoa pole kwa mashabiki wa Yanga waliopata ajali pia amewaomba waamuzi kulinda wachezaji kwani ni moja ya jukumu lao akitolea mfano rafu mbaya iliyotokea leo. Pia amekanusha Yanga kuwa na mpango wowote na mchezaji Manzuki.

Kwa upande wa Juma Mgunda, kasema timu yake ina wachezaji wapya wengi na bado wanajenga timu yao na yeye kama kocha anakubali makosa yote yaliyofanyika kwa upande wao.

TAMATI
 
Ni weekend tena. NBC Premier League inaendelea ambapo Wagosi wa Kaya, Coastal Union watashuka dimbani kuwaalika Mabingwa watetezi wa taji, Yanga katika dimba la Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika dimba hilo mwezi wa saba mwaka huu katika mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation ambapo Yanga walibuka na ushindi.

Je leo Juma Mgunda ( Guardiola Mnene) ataweza kuwadhibiti tena Yanga? Tukutane hapa saa 10:00 jioni.

Utabiri wangu: 1-1
Mungu ibariki Coastal union ishinde huu mchezo kelele zipungue mitaani
 
Back
Top Bottom