Mwamuzi Mwandembwa akae nje angalau mizunguko 5. Makosa yao mechi ya Coastal Union Vs Yanga

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
21,496
37,789
Ukiwa unafuatilia Kwa makini uchezeshaji wa Waamuzi wa soka Tanzania, Mechi atakayochezesha Mwandembwa itakupa mengi ya kuandika. Si Mechi ya Jana pekee (Coastal Union Vs Yanga) ila ni karibu Kila Mechi hata zinapokutana timu za mid-table yeye akashika kipyenga.

Mechi ya Jana yeye na associates wake wote walikuwa ovyo;
1. Kadi ya njano kuonyeshwa Kwa mchezaji wa Coastal ambaye hakuhusika na tukio na alipokuja kuhusika na tukio baada ya dakika 40 Kadi ya awali ikafutwa, akaitwa Gerald Gwalala aliyestahili awali akaonyeshwa Kadi dakika ya 41 Kwa kosa alilotenda dakika ya 11. Je, Gwalala angekuwa amehusika kwenye vurugu za dakika ya 41 angeonyeshwa Kadi 2 za njano mfululizo?

2. Khalid Aucho kuonyeshwa Kadi ya njano Kwa kumpiga Ajibu kiwiko cha uso badala ya Kadi nyekundu huku refa akilazimika Kwanza kuuliza mezani nini kilichotokea wakati yeye ndiye aliyepuliza filimbi ya madhambi faida Kwa Yanga na alipaswa kujua kinachoendelea eneo la tukio Hadi mpira uondoke eneo Hilo (tension area).

3.Kutomuonyesha Ajibu Kadi ya njano Kwa tukio la kupiga mpira mbali wakati ukitengwa na Aucho kitendo kilichosababisha apigwe kiwiko.

4. Waokota mipira kuficha mipira Hadi mchezaji anafuata mpira umbali mrefu kwenye mtaro (Yao) Kwa lengo la kupoteza Muda lakini Mwamuzi hakukemea kitendo hicho wala kuwasiliana na mamlaka kukemea uhuni huo.

Katika hili Kamisaa na Fourth official wasiachwe salama. Kwenye Mechi ya Ahly Vs Simba na Ile ya Raja Vs Mamelod tuliona waamuzi na Maafisa wa Mechi walivyo act kukemea uhuni wa waokota mipira.

Kwenye Mechi Ile ya Taifa stars Vs Uganda Cranes tuliona refa anafukuza waokota mipira baada ya kuanza uhuni wa kurusha mipira uwanjani kupoteza Muda baada ya Stars kuongoza.

5.Waamuzi wasaidizi 1 na 2 wasiachwe salama maana Jana walikuwa na tafsiri binafsi ya kosa la offside.
 
Ngoja mwandembwa Fc waje...
Waje tu nawasubiri. Refa amekuwa na mwendelezo wa ujinga Kila Mechi na siyo Jana tu. Mimi sijasema kampendelea Fulani Ila nahisi uwezo wake ni mdogo Sana. Ukiangalia hayo matukio hapo juu yameumiza timu zote 2 Jana.
 
Back
Top Bottom