Clouds Media Group siku nyingine mkitaka kuzileta Bendi za Kongo muwe mnatuuliza wenye mziki wetu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,130
Nimesikitishwa sana na kwa kiasi kikubwa mno mara baada ya kusikia ya kwamba Mwanamuziki wa Ngiama Makanda Werrason na Bendi yake ya ' Maison Mere ' wanakuja ' Kutumbuiza ' nchini Tanzania kwa mualiko wa Clouds Media Group.

Sababu kubwa tu iliyopelekea Mimi kusikitika ni kutokana ya kwamba hata ' Tajiri ' Joseph Kusaga na ' Tajiri Mwenza ' Ruge Mutahaba wanajua fika kuwa ukitaka ujaze ukumbi hadi wengine ' wakanyagane ' katika ' Show ' basi walete Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana.

Werrason anapiga ila JB Mpiana anajua mziki na hakuna Mwanamuziki wa Kongo kwa sasa ambaye anaweza kuujaza Uwanja kama ule wa Taifa kama JB Mpiana na Bendi yake ' iliyobarikiwa ' kabisa ya Wenge Musica BCBG.

Clouds Media Group siku zingine kabla ya ' Kukurupuka ' kuleta hizi Bendi za Kongo muwe Kwanza mnatuuliza wenye mziki wetu na tuliobobea nao ili msije mkajikuta mnaingia hasara na mkaja kujuta bure! Hakuna kama Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana iwe hapa duniani au mbinguni na Wenge Musica BCBG ya JB Mpiana ni Bendi ambayo hata ikiwa inapiga ' Malaika ' wa Mbinguni huwa wanacheza na ' Maualana ' mwenyewe anafurahi huku akiwa anaendelea na Uumbaji wake.

Mmenikera kama siyo kuniudhi sana kutoileta Wenge Musica BCBG yake JB Mpiana nchini Tanzania. Ulaya kote huko hadi Latin America achilia mbali America kwenyewe, South Africa na nchi nyingi tu za Afrika wanaigombania hii Bendi nyie mnaenda kutuletea Ngiama Makanda Werrason na Wenge Musica ' Maison Mere ' yake!

Nawasilisha.
 
Mpaka sasa likiwekwa lile sebene la Werason halina mpinzani.

Werason yuko vizuri kwenye live show on stage labda kama wewe umezowea kusikiliza audio huwezi kulijuwa hili.

Labda nungeona unajuwa muziki kama ungeshauri aletwe Fere gola ndio hajawahi kufanya show Bongo.
 
Hapa mimi na wewe tunakwenda Sawa kabisa.Sijawahi penda nyimbo ya Werrason na fally ipupa zaidi ya JB mpiana
 
alikula za uso huyo jamaa yako Jb mpiana aliyefanya uchawi wa kumeza chura,muulize mama sakina trans kilichomtokea pale leaders club na mwanza hadi akazimia
 
Mpaka sasa likiwekwa lile sebene la Werason halina mpinzani.

Werason yuko vizuri kwenye live show on stage labda kama wewe umezowea kusikiliza audio huwezi kulijuwa hili.

Labda nungeona unajuwa muziki kama ungeshauri aletwe Fere gola ndio hajawahi kufanya show Bongo.

Siku nyingine ukikutana na Watu wenye mziki wetu wa Kongo na tunaoujua vyema usije ukaandika ' upuuzi ' wako huu tafadhali. Nenda kokote pale uliza Kongo nzima nani ni Bingwa wa kupiga ' Live ' na ambaye hujaza Ukumbi kila aendapo na mpaka sasa ameshasababisha Watu wengi kupoteza maisha kwa Kugombania kuimbia Ukumbini utaambiwa ni JB Mpiana na Kundi lake zima la Wenge Musica BCBG. Umeshajiuliza ni kwanini Bendi yake ( ya BCBG ) inaitwa ' L'equipe Nationale ' yaani Timu ya Taifa? Je umeshajiuliza ni kwanini Quarter Latin yake Koffi na Wenge Maison Mere yake Werrason hawajaziita hivyo?

Cc: Shunie
 
Babe endelea basi
 
alikula za uso huyo jamaa yako Jb mpiana aliyefanya uchawi wa kumeza chura,muulize mama sakina trans kilichomtokea pale leaders club na mwanza hadi akazimia

Sijakuelewa na nakuomba urudie tena kuandika. Na bahati nzuri ' Shows ' zake ( JB Mpiana ) za mwaka 2012 hasa ile ya Leaders Club Dar es Salaam nilikuwepo na nakumbuka nilikuwa ' nikiserebuka ' jirani kabisa na Haji Londa na huyu huyu Steve Nyerere bila kumsahau Mtangazaji anayempenda JB Mpiana kupita maelezo Ben Kinyaiya. Onyesho lake la Mwanza sikuenda japo nililifuatilia kiumakini kabisa na unaambiwa alifanya ' balaa ' huko hadi leo ' Wasukuma ' wanatamani JB Mpiana arudi ila tatizo tu ni kwamba ili kumleta hapa Tanzania unatakiwa uwe na kama Tsh 300 Milioni wakati kuwaleta akina Koffi Olomide na Werrason hata ukiwa na Tsh 15 Milioni unaweza.

Na kwa kukusaidia tu ni kwamba katika ile ' Show ' ya Leaders Club huyo Mama Sakina mmiliki wa Bendi ya Mashujaa alipigwa ' Kipapai / Ulozi / Uchawi ' na yule adui yake mkubwa wa Twanga Pepeta hadi nakumbuka ' akazimia ' na akina Steve Nyerere wakambeba pale Ukumbini na kumkimbiza Kwake lakini wakati wanataka kumuondoa pale baadhi ya Wanamuziki wa Wenge Musica wakiongozwa na L'echostre Director wao ambaye pia ni Mwimbaji Jules Kibens Molongeshi a.k.a Le Professeur aliwaambia wampake ' dawa ' fulani ambapo alipakwa kweli na Mama ' akazinduka ' pale pale ila akashauriwa tu akapumzishwe.

Katika suala la Uchawi / Ndumba / Ulozi / Ola Ola cheza na Watu wote duniani ila siyo Wakongo ( Wazaire ) Mkuu.
 
Back
Top Bottom