Kusaga: Clouds FM haina chama! Akanusha Clouds kununuliwa na Rostam Aziz

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Akijibu swali la Gerald Hando kuhusu na clouds kuhusishwa na CCM amesema Clouds haina chama. Katika mwaka huu wa uchaguzi amesema kila chama kitapewa haki sawa kwenye media yake.

Pia Kusaga alisema media yake imekuwa ikisemwa vibaya hasa na mtandao huu wa JF kuwa clouds ni CCM na amekanusha Na kuita kuwa hizo ni propaganda za wapinzani wake wa media.

Clouds fm wamekana kuwa shutuma zinazotolewa kwenye social media hasa jamiiforums kwamba wao CCM sio za kweli.

Akihojiwa CEO wa clouds katika kipindi power breakfast, amesema wao kama radio hawana chama kwa sababu hata sheria TCRA haziruhusu.

Pia kwenye uchaguzi wa mwaka huu wagombea wote watapewa nafasi sawa.

Ameendelea kusema kuwa wafanyakazi wachache kuwa CCM haimaanishi clouds yote ni CCM.

Pia clouds imekanusha habari zilizozagaa kuwa radio imenunuliwa na Rostam Aziz, ameongeza kuwa hizo ni propaganda za kuichafua radio hiyo.

Amesema kama wakiuza radio watatangaza kwasababu radio ni yao,na hawamuogopi mtu.

Wakati wanamuhoji nimesikia wanamuita Joh (labda ndiye Joseph Kusaga) sina uhakika na majina mengine,wanomfahamu watatujuza.

millardayo.png

Habari Wanabodi,

Akizungumza moja kwa moja kutoka Abu Dhabi,CEO wa Clouds Media Ndugu Joseph Kusaga ametamka wazi mtandao wa JF unamuandika vibaya kwamba redio yake ni ya CCM,amesema kwamba radio yake haina chama,anafuata sheria za TCRA,kama kuna mfanyakazi wake anashabikia chama flani basi akirudia tena atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Amesema kama clouds FM ingekuwa ina ushabiki na vyama basi ingekuw ya chadema maana Mbowe ni rafiki yak mkubwa sana wamefahamiana zaidi ya miaka 30.

Nawasilisha.
 
Akijibu swali la Gerald Hando kuhusu na clouds kuhusishwa na CCM amesema Clouds haina chama. Katika mwaka huu wa uchaguzi amesema kila chama kitapewa haki sawa kwenye media yake. Pia G alisema media yake imekuwa ikisemwa vibaya hasa na mtandao huu wa JF kuwa clouds ni CCM na amekanusha Na kuita kuwa hizo ni propaganda za wapinzani wake wa media.
Kwa wale wanaomfahamu kusaga tangu ujana wake wanafahamu fika ni mtu wa namna gani na ukweli usiyo fichika ni kuwa kituo chake cha radio/tv kinazidi kuongeza wasilikizaji/waangaliaji na hivyo kuwa tishio kwa baadhi ya vituo vingine.
CCM inakituo chake cha radio na hata hicho kimekuwa na mvuto fulani hasa kwa wakazi wa dar kutokana na vipindi vyake. Wakati huu soko ndiyo linaamua vitu gani vyende hewani na vituo visivyoendana na hali hiyo vitaendelea kulalamika tuu.
 
Pia amekanusha taarifa kuhusu Rostam Aziz kuinunua clouds media
 
Kuna haja ya watu humu ndani kuwa makini na taarifa zinazoletwa ikiwezekana wafungiwe kabisa Joseph Kusaga kalalamika sana kuhusu kuuzwa kwa Clouds.
 
Kwa wale wanaomfahamu kusaga tangu ujana wake wanafahamu fika ni mtu wa namna gani na ukweli usiyo fichika ni kuwa kituo chake cha radio/tv kinazidi kuongeza wasilikizaji/waangaliaji na hivyo kuwa tishio kwa baadhi ya vituo vingine.
CCM inakituo chake cha radio na hata hicho kimekuwa na mvuto fulani hasa kwa wakazi wa dar kutokana na vipindi vyake. Wakati huu soko ndiyo linaamua vitu gani vyende hewani na vituo visivyoendana na hali hiyo vitaendelea kulalamika tuu.

Inaongelewa kampuni we unaleta ujana wa owner hapo unalenga nini??!!!!
Acha bootlicking . . . . . . . . . .
 
Clouds fm wamekana kuwa shutuma zinazotolewa kwenye social media hasa jamiiforums kwamba wao CCM sio za kweli.

Akihojiwa CEO wa clouds katika kipindi power breakfast, amesema wao kama radio hawana chama kwa sababu hata sheria TCRA haziruhusu.

Pia kwenye uchaguzi wa mwaka huu wagombea wote watapewa nafasi sawa.

Ameendelea kusema kuwa wafanyakazi wachache kuwa CCM haimaanishi clouds yote ni CCM.

Pia clouds imekanusha habari zilizozagaa kuwa radio imenunuliwa na Rostam Aziz, ameongeza kuwa hizo ni propaganda za kuichafua radio hiyo.

Amesema kama wakiuza radio watatangaza kwasababu radio ni yao,na hawamuogopi mtu.

Wakati wanamuhoji nimesikia wanamuita Joh (labda ndiye Joseph Kusaga) sina uhakika na majina mengine,wanomfahamu watatujuza.
 
Kwa wale wanaomfahamu kusaga tangu ujana wake wanafahamu fika ni mtu wa namna gani na ukweli usiyo fichika ni kuwa kituo chake cha radio/tv kinazidi kuongeza wasilikizaji/waangaliaji na hivyo kuwa tishio kwa baadhi ya vituo vingine.
CCM inakituo chake cha radio na hata hicho kimekuwa na mvuto fulani hasa kwa wakazi wa dar kutokana na vipindi vyake. Wakati huu soko ndiyo linaamua vitu gani vyende hewani na vituo visivyoendana na hali hiyo vitaendelea kulalamika tuu.
crappy post
 
toleo la MAWIO la jana,limeripoti kikamilifu clouds kutumika na CCM kisiasa na kipropaganda!!

clouds fm wameshiriki kuandaa na kuomba zaidi ya 2.5 bln kutoka Ikulu kwa ajili ya propaganda ya kuhimiza kura ya ndio ya kura ya katiba ya CCM,mchanganuo huo umeandikwa na RUGE MUTAHABA ukihusisha pia wanamziki wa clouds kwa wingi walio chini ya THT!!!

Kusaga wala RUGE hawawezi kukili waziwazi ila watambuzi wa mambo wanajua na wao pia unafiki wao wanaujua,wao kwao ni pesa tu kwanza!!!!
 
Back
Top Bottom