DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Clinic ya Marie Stopes iliyoko jijini Mwanza wanajihusisha na vitendo vya utoaji mimba. Mimba zinatolewa sana pale, hasa za wanafunzi wa vyuo vikuu. Mchezo unaofanyika ni kwamba wanawake wanaohitaji hiyo huduma hufika hapo na huulizia huduma ya abortion, au kwa kujifanya mimba imeharibika.
Kinachofuata, mhusika anafanyiwa huduma inaitwa "dilatation and curateage", ambayo kimsingi ni kutanua njia ya shingo ya kizazi, kisha kuharibu mimba kwa kusafisha kizazi.
Sasa, the way wana record hiyo ili kuficha huo uozo ni wana record kama vile mtu alikuja na "miscarriage" tayari au "incomplete abortion" halafu kuwa wao wakasafisha tu kizazi kuondoa mabaki yaliyobaki kwenye kizazi, lakini ukweli ni kwamba wanakua wameharibu mimba na kufanya abortion ila kwenye rekodi zao wanaonyesha kama vile ni incomplete abortion.
Kuna uwezekano pia timu ya usimamizi wa huduma za afya ya halmashauri na hata ya mkoa inajua kabisa mchezo unaoendelea lakini wananyamazishwa kwa bahasha, maana hizi habari ziliwahi kuripotiwa kwao lakini hakukua na hatua zozote ziulizofuata.
Pia, hawa watu kuanzia wakati wa usahili kama unataka kuajiriwa pale kama daktari au muuguzi, wanakuuliza kabisa wewe mtazamo wako kuhusu utoaji mimba ukoje, na wanakupa scenario kuwa ikitokea wakati unatimiza majukumu yako halafu akaja mteja ambae anataka kutoa mimba je utachukua hatua gani? Ukitoa majibu ambayo yanaonyesha kama vile unapinga mambo ya abortion, wanakuchinjia baharini hupati hiyo kazi.
Tukumbuke kuwa kwa nchi yetu, utoaji wa mimba (abortion) ni kinyume cha sheria za nchi.
Nimeona nifichue hili jamani nimechoka vitendo hivi kila siku nashiriki utoaji mimba ila ni kwa sababu ya njaa tu, nimeona nije kutoa ripoti huku, Wizara ya Afya Tanzania fuatilieni hili mchukue hatua. Nendeni pale kagueni records zao muone walivyo na "incomplete abortion" kibao ambazo wanazifanyia dilatation and curatage, hizo zote ni mimba ambazo zimetolewa hakuna cha incomplete abortion wala nini. Fanyeni uchunguzi kwa makini, mtagundua kitu, ila msiende kichwa kichwa.
Asante.
Ilianzishwa kwa ajili ya utoaji Mimba huko UK. Hii ndo kazi yake ya kwanza kabisa kwenye katiba yao
 
Ulivopresent mada kama una wa accuse hao jamaa.
Private institution zinahitaji pesa ili kujiendesha.
Kwa hiyo sitakiwi kuwa accuse hata kama wanafanya mambo ambayo ni kinyume cha sheria? Najua kuwa private facilities zinahitaji pesa kujiendesha, lakini je hiyo inatosha kuzifanya zifanye mambo kinyume cha sheria za nchi?
 
Kwa hiyo sitakiwi kuwa accuse hata kama wanafanya mambo ambayo ni kinyume cha sheria? Najua kuwa private facilities zinahitaji pesa kujiendesha, lakini je hiyo inatosha kuzifanya zifanye mambo kinyume cha sheria za nchi?
Ukienda na siasa zako utajibiwa ki sayansi na utafyata mdomo wako.
Wao wanajua kwamba ni kinyume na Sheria lakini ukiambiwa upeleke evidence ya mimba iliyotoka utaweza? Au unaongea Kwa mihemko.
 
Ukienda na siasa zako utajibiwa ki sayansi na utafyata mdomo wako.
Wao wanajua kwamba ni kinyume na Sheria lakini ukiambiwa upeleke evidence ya mimba iliyotoka utaweza? Au unaongea Kwa mihemko.
Kwa hiyo unashauri nipige kimya tu, nisifanye chochote hata kusema kuhusu hili? Au unashauri nini haswa? Maana unakubali kuwa wanafanya kinyume cha sheria, ila wana loophole ya kujificha na wanaitumia hiyo, so tuache tu?
 
Back
Top Bottom