Chupi Yamwumbua Masai

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
Masai mmoja alikuwa anasafiri kwa basi kutoka mkoa fulani kuelekea mkoa mwingine. Siku hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuvaa chupi kitendo kilichomfanya awe anaionyesha onyesha sana kwa watu ndani ya basi! Ghafla alibanwa na haja kubwa hivyo akaomba basi lisimame ili akachimbe dawa!

Eneo walilokuwa wamesimama lilikuwa ni porini kidogo, utingo wa lile basi akamtania kwa kumwambia awe makini eneo hilo lina majambazi sana.

Masai akateremka na kuelekea vichakani kujisaidia. Baada ya dakika kadhaa yule masai alikuja anasikitika sana na kupanda ndani ya basi. Abiria wenzake walipomwuliza anasikitika nini akasema,

“Konda alisema, kweli nimeamini. Hii sehemu iko na majambasi tena majambasi haya yanaiba hadi mafi yangu!”

Abiria wakaangua kicheko kwani wengi walisikia hali ya hewa imebadilika ghafla masai aliporejea wakajua labda hajajisafisha lakini ukweli ni kwamba kwa kuwa alikuwa hajazoea kuvaa chupi, alijikuta akijisaidia bila kuvua chupi na alipomaliza; kutazama chini hakuona mavi akajua kaibiwa kumbe yamebakia kwenye chupi yake!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom