Chuo Kikuu kipya cha Afya kujengwa Dar

Jamani hivi Mwalimu alipopokea nchi mwaka ule wa uhuru alikuwa na walimu (Profs and Drs) wangapi?? wahandisi?? madaktari?? na kadhalika!! sasa sisi badala ya kujipanga na kutafta namna ya kujiendeleza na kupata a "breakthrough" tunabaki kusema walimu wa vyuo vya dar wawe wanafundisha kwenye vyuo vipya..... ile kitu inaitwa uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi nayo tunaiangalia au??

jamani, inabidi tuache kufikiria kutokana na vile tulivyovikuta na kuviona, inabidi tuanze kutumia vipaji vyetu kutafta "any other means necessary" kujiletea maendeleo....
 
Kwa nini wasijenge Tabora? Kuna eneo kubwa tu pale na hospital kubwa ya Mkoa wa Kitete. Walau Tabora nayo itakuwa na income fulani kwani wanafunzi ni purchasing Power. Tabora hamna madini, mgodi, kiwanda wala babu yake nani. Pamejichokea na kukondeana kama kijibwa cha Darfur.....

Mkuu Sikonge,
Umesahau ndugu yangu, Tabora mna migodi miwili ya madini kule. Mmoja wa Resolute (Dhahabu kule Nzega) na wa pili unaitwa Rostam, Rustam, Rastam et. al (Uko kule Igunga- joking). Pia tatizo la nchi yetu ni kwamba tofauti ya maendeleo kati ya Dar na mikoa mingine (ukiacha Arusha na Mwanza) ni kubwa mno. Kwahiyo kwa hali halisi Wahadhiri kwenda kuishi Tabora wanaweza kuona kana kwamba wamepelekwa huko kuteseka. Kilimanjaro, Morogoro na Dodoma access ya Dar ni rahisi ndo maana KCMC, UDOM na SUA hazina shida sana ya kupata wahadhiri. Kwahiyo juhudi zinahitajika kuboresha miundo mbinu na social services katika mikoa mingine ili kuvutia watu kufanya kazi huko.
 
chuo kikuu cha afya ni Muhimu sana kwa mahitaji ya afya ya jamii. Ni wazo zuri ila si kwa Dar es salaam tena. Dar kwa sasa kuna vyuo vikuu vitatu vinatoa madaktari IMTU, Kairuki, na Muhimbili. Vyuo vikuu vya afya huwa ni msaada mkubwa sana kwenye huduma za afya wanafunzi wa afya huwa ni moja ya nguzo za utafiti na utabibu wakati wakiwa masomoni husaidia kuongeza wataalamu kwa kiwango kikubwa wanapokuwa masomoni na kurahisisha kazi za mabingwa wa afya. Kuongeza vyuo hivi Dar ni kutowatendea wananchi wa mikoa mingine haki. Waangalie ni mkoa gani hauna chuo wapeleke chuo. Kuna mikoa mingi ambayo inamahitaji hata ya RMA ambao hawapatikani wakipeleka chuo watasaidia sana hata kupata wanafunzi madaktari na kuboresha huduma za afya na utafiti maeneo hayo, achilia mbali ajira na purchasing power kuongezeka.
 
hii plan ya kujenga chuo kikuu kwembe sio ya leo ni plan tangu wakati wa Nyerere, mara nyingi hawa viongozi wanachukulia advantage ya programz za serikali kwenye mambo yao ya kampeni za umeshawadia tutasikia mengi tu kisiasa naona muda
 
Kwa nini wasijenge Tabora? Kuna eneo kubwa tu pale na hospital kubwa ya Mkoa wa Kitete. Walau Tabora nayo itakuwa na income fulani kwani wanafunzi ni purchasing Power. Tabora hamna madini, mgodi, kiwanda wala babu yake nani. Pamejichokea na kukondeana kama kijibwa cha Darfur.....

Tabora kuna madini yapo Nzega maeneneo ya LUSU na kuna kampuni inayoyachimba inaitwa Tanzania RESOLUTE Mining.
 
Lazima chuo vikuu vingi vijengwe na ushindani utapatikana na hatimaye Elimu bora. Suala la wahadhili/ri si hoja sana ipo Ineternet.

Pia nafikiri chuo cha afya lazima kuwe na hospital nzuri nafikiri nacho ni kigezo.JK kama unaweza tuletee vyuo vingi tena vingi wakufundisha wapo wengi wazungu/waafrika kutoka nje wapo wengi na tena wamebobea nawako tayari kwa mshahara huo huo wa ndani.
 
Sehemu nzuri ya kujenga Vyuo ni Arusha, **** mashamba mengi sana ambayo yako karibu na barabara na yana nafasi, Arusha kuna hali ya hewa nzuri, Arusha ni mji ambao utazidi kukua na kwasababu una eneo kubwa unaweza kuwa mji wa kisasa kama ukipangiliwa.
 
Yeah,
Arusha ni pazuri sana. Kuna mipango ya kujenga sehemu ya Mandela Institute of Science and Technlogy huko Arusha na tayari serikali ilishatoa eneo ambalo limejumuisha na ilimokuwa CARMATEC na walishafukuzwa kwenye eneo hilo tayari na sijui kama sasa serikali imeshawapa eneo lingine maana ilipowafukuza haikuwaambia waende wapi. Chuo hiki ni cha Afrika nzima na makao yake makuu yatakuwa Abuja Nigeria. Sehemu ya Tanzania inakuwa ni kwa ajili ya Biotechnology.
 
Jamani hivi Mwalimu alipopokea nchi mwaka ule wa uhuru alikuwa na walimu (Profs and Drs) wangapi?? wahandisi?? madaktari?? na kadhalika!! sasa sisi badala ya kujipanga na kutafta namna ya kujiendeleza na kupata a "breakthrough" tunabaki kusema walimu wa vyuo vya dar wawe wanafundisha kwenye vyuo vipya..... ile kitu inaitwa uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi nayo tunaiangalia au??

jamani, inabidi tuache kufikiria kutokana na vile tulivyovikuta na kuviona, inabidi tuanze kutumia vipaji vyetu kutafta "any other means necessary" kujiletea maendeleo....

Morani75,
Hayo mawazo yako ndiyo ilitakiwa iwe dira ya kila mtanzania mmoja mmoja. Serikali tayari imekwishatangaza azma yake ya kujenga Chuo Kikuu cha Afya, wajibu wetu ni kutumia fursa hiyo kujiletea maendeleo na wala si vinginevyo. Hatupaswi kuiambia serikali isitishe mpango huo ili kwanza tufanye ukarabati wa vyuo vilivyopo, hii haingii akilini hata kidogo.

Ni vyema watanzania tubadilike na tuwe aggressive badala ya hii mitazamo tunayozidi kuijenga. Kila siku tumekuwa tunashuhudia malalamiko kwamba wageni wakiingia nchi huwa maskini lakini wanatoka wakiwa matajiri, ni kwanini, jibu ni kuwa wako aggressive!!!! Ninatoa onyo kuwa Chuo kutajengwa na tusipochukua nafasi zetu katika hilo watakuja wakenya, waganda nk kuwa wahadhiri na sisi tutakuwa na kazi ya kuuzia soda na chips wanafunzi.

Kazi kubwa ya serikali ni kuweka mazingira ambayo wananchi wataweza kutumia fursa zilizopo kwa maendeleo yao
 
Duh hivi ndio maana nasema kuwa lazima tuwe makini sana na harakati za Kampeni hizi

Mkuu unachosema ni kweli. Ukienda pale mlimani utacheka sana. Hata vyoo vinatisha kwa uchafu, ofisi za maprofesa zinachekesha, hata tiles zake ziko hio, acha maktaba inayoanza kuoza yeynye vitabu toka miaka ya 30. Sasa lengo la kujenga chuo Kikuu kipya ni nini wakti UDSM, UCLAS, MUHIMBILI na SUA vinasuasua? jibu ni kuelekea 2010. Hakuna sababu yoyote ya kimsingi ya kujenga chuo Kikuu kipya, siasa tu. na kama kuna mtu amemshauri rais basi itakuwa ni kwa sababu ya maslahi binafsi.
 
Tilieni mkazo hayo maadishi mekundu

MUHAS comes of age

2009-01-05 11:22:59
By Correspondent

Recently the Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) staged its second graduation ceremony since it was declared a full fledged University from its former status of a Constituent University of the then main Dar es Salaam University in 2006.

MUHAS which started way back in 1963 as a Faculty of Medicine of the defunct University of East Africa with an enrolment capacity of just 10 students all studying same medicine specialty has come of age by knocking 40 years with an increased enrolment to about 700 students studying 71 different health and allied sciences specialties a Correspondent report looks at MUHAS’s proud 40 years…

``We might not have achieved something big and special as an academic institution at local, regional and international levels by having been able to raise Muhimbili University from a mere Faculty of Medicine of the then University of East Africa (UNEA) to a full fledged Health and Allied Sciences University in 2006 at same time scaling up students enrolment from 10 students in 1963 to about 700 last academic year.

But given the circumstances and environment we were shaped in and go on operating, this progress we can, with confidence make us proud hence able to walk majestically as an academic institution with confident feelings MUHAS has served the purpose of its establishment and has given the nation what it deserves``, observed Professor Kisali Palangyo, when giving his speech during the second graduation which was attended by president Jakaya Kikwete.

Professor Palangyo, a MUHAS Vice-Chancellor told the gathering of thousands of people made up of parents, grandaunts, well-wishers, other local Universities Vice-Chancellors and retired Vice-Chancellors as well as members of the public that for MUHAS being able to produce not only high grade and internationally accepted dons, health and allied sciences experts is in itself a remarkable success let alone being able to grow so big during the 40 plus years period.

One of the vivid successes the Vice-Chancellor was so proud of is the Universities fast but justifiable growth of academic programmes/specialties from a single specialty in 1963 to 71 by last academic year. More specialties are in pipe line to meet national demands for health and allied sciences experts.

One of the strategies which enabled MUHAS to increase enrolment is the construction of twin ultra-modern lecture halls able to accommodate 350 students each at a go and provide modern office spaces for 60 dons.

The two ultra-modern lecture halls were built at a cost of 2.3 billion Tanzania shillings (about US Dollars two million).

The money was provided by the government (TZS one billion), loan by the Tanzania Education Authority- TEA (TZS 814,908,600) and MUHAS internal generated revenues (TZS 570m).

Looking at the way MUHAS has managed to realize the scaling up of student enrolment for being able to contribute over 1.3 billion shillings in the construction of the two ultra-modern lecture halls, one might understand and get a true feeling of Professor Palangyo`s words to president Kikwete, `we believe and confidently feel as an academic institution MUHAS has served the purpose of its establishment and has given the nation what it deserves`.

Apart from achievements in student enrolment, MUHAS has for several years conducted meaningful and internationally accepted research in various sectors of health and allied sciences.

These researches according to the Vice Chancellor were conducted through financial support from partner Universities like the Harvard University and Dartmouth Medical School.

Donor agencies which supported research at MUHAS include the Swedish International Development Agency (SIDA/Sarec) and the European Union.

According to Professor Palangyo, research is one of key roles Universities the world over are supposed to undertake if they are to meet their purposes of creation and meet expectations of both the nation and members of the public.

In that sense, the Vice Chancellor expressed his worries in the way the government which is the proprietor of MUHAS has distanced itself from providing funding to research.

``In the last fiscal year MUHAS spent a total of 10 billion Tanzanian shillings which is equivalent to slightly over US Dollars eight million in financing research.

Unfortunately coffers for this important undertaking were filled by donor agencies and partner Universities.

This is not a right move for the government to distance itself from funding research.

The government needs to know that a University without conducting research its credit will be in jeopardy, hence I call upon the state to review its position by releasing funds to cater for research in the coming fiscal year” hinted the Vice Chancellor.

Some of the areas which have benefited from MUHAS conducted research are HIV/AIDS, TuberCulosis (TB), Malaria, children and females ailments.

``Research leads to giving accurate solutions to various ailments and health challenges facing mankind, bring positive thinking towards seeking treatments for complicated health cases and generate new knowledge,`` noted Professor Pallangyo, keeping wondering as to how Tanzania can ignore research yet boldly plans to reduce if not eradicate at all various health and medical challenges the nation is currently facing.

Regarding the buildings and other infrastructure from which the University is operating from, Professor Palangyo said most of the buildings are old and need not only urgent but major repairs to be able to serve their purposes well.

He was happy with the government`s decision to press for MUHAS to be given title deeds for 3,800 acres of land at Mloganzila and Kwembe villages along Morogoro road close to Kibaha township where ultra-modern and huge new MUHAS campus is to be set up in a few years to come.

``With humility and honour, I, on behalf of the MUHAS Council would like to salute your government for its firm support which ensured MUHAS is given the new land title deeds.

With the title deeds MUHAS is confidently owning the 3,800 acres on which it plans to build a new campus plus a modern, referral and teaching hospital worth U$ 40 million,`` said the Vice Chancellor.

MUHAS according to the Vice Chancellor feels the government has taken the right move of seeking a loan of US Dollars 40 million to be used in setting up a well equipped and ultra modern referral and teaching hospital as that will significantly reduce staggering expenditure of foreign currencies for ailing Tanzanians referred to foreign hospitals.

During the second MUHAS graduation a total of 569 graduates were awarded Diplomas, Advanced Diplomas, Bachelor and Master degrees` as well as PhD`s.

Among the graduates was president Kikwete`s daughter Salama Kikwete. The president`s daughter graduated as Doctor of Dental Surgery.

SOURCE: Guardian
 
asante mkuu nyikana.., hivi nami ndivyo ninavyofahamu, kuwa si chuo kipya bali ni campus nyingine ya MUHAS, katika kukipanua na kuendeleza zaidi, nadhani hii ni idea nzuri kabisa, pale muhimbili ni padogo mno, na hapana nafasi ya upanuzi, na sasa muhimbili si college tena ni chuo inahitaji nafasi zaidi,
 
Mkuu unachosema ni kweli. Ukienda pale mlimani utacheka sana. Hata vyoo vinatisha kwa uchafu, ofisi za maprofesa zinachekesha, hata tiles zake ziko hio, acha maktaba inayoanza kuoza yeynye vitabu toka miaka ya 30. Sasa lengo la kujenga chuo Kikuu kipya ni nini wakti UDSM, UCLAS, MUHIMBILI na SUA vinasuasua? jibu ni kuelekea 2010. Hakuna sababu yoyote ya kimsingi ya kujenga chuo Kikuu kipya, siasa tu. na kama kuna mtu amemshauri rais basi itakuwa ni kwa sababu ya maslahi binafsi.

Mkuu upo sahihi ila nadhani maprofessor wenyewe wanatakiwa watafute mbinu ya kuviendeleza hivi vyuo, pana baadhi ya mambo si kuilaumu serikali, hivi jamani kweli serikali ije isimamie usafishaji wa vyoo university? au upatikanaji wa maji? basi pana haja gani akina mukandala kuwepo! tatizo la vyoo ni usafishaji na ugawaji tenda kiholela bila kuangalia muhusika je anaweza kusimamia usafi au la!

kingine ukarabati unafanyika mara nyingi katika vyuo vyetu tatizo lipo palepale ukarabati wa kuripua kwa ajili ya 10%, ni majenereta mangapi yamewekwa UDSM na hayafanyi kazi ipasavyo? ni majengo mangapi yamefanyiwa ukarabati au yamejengwa wakati mfumo mzima wa maji na umeme ndani ya jengo ni tatizo? ni miradi mingapi imekumbatiwa na maprofessor hadi pesa zinarudi kwa wafadhili kwa kuwa hazina cha kufanya wakati hakuna vitendea kazi katika maabara zetu? je bado tunailaumu serikali? Vyuo vyetu tunaviua sisi wenyewe, tuache kuibebesha seerikali mzigo, vyoo vipo UDSM ila havina maji na ni vichafu, nani wakuwasimamia hawa wafanya usafi?
 
Nafahamu wengi nitawakwaza na watanishambulia na nitapenda kusema tena na tena ninayoamini ni ya ukweli.

WAHITIMU /WAFANYAKAZI /WANAFUNZI wengi wa UDSM ni ma conservative sana ningependa kufahamu huwa mnalishwa nini pale.

Sitoshangaa kuona asilimia kubwa karibu 90% ama zaidi wanaopinga kujengwa kwa vyuo vipya wanauhusiano na udsm na wenda watueleze hofu yao huwa imejikita wapi?

Kifupi nielewavyo mimi UDSM imeshuka kielimu kutokana na kukosa ushindani huo ndio ukweli .Huwezi fanya mazoezi tu peke yako harafu ukijiona uko fiti na ukatoka kifua mbele kwamba wewe uko fiti ,ndiyo maana kuna mechi za kirafiki lazima ujipime.

Tanzania imeshuka kielimu kwa sababu ya kung'ang'ania chuo kimoja na kinachoendelea kuonekana kushindwa kudeliver.

Mfano kama unampango wa kujenga nchi ionekane inapendeza nafikiri mwelekeo sahihi si kuendelea kubomoa na kurekebisha vijimiji vilivyolundikana na ku-saturate lazima utafute maeneo mengine huru na yaliyo wazi kuanza kujenga kutokea a-z.

Kunga'ng'ania kuendelea ni vyuo viwili vinavyoelekea ku-saturate ni upotevu wa dira sahihi ktk mapinduzi ya elimu.

JK tuletee vyuo vingi kadri inavyowezekana na tena kama inawezekana kila mkoa lazima iwe na vyuo aghalabu viwili vitatu.
 
Chuo Kikuu kipya cha Afya kujengwa Dar

Na Jackson Odoyo

RAIS Jakaya Kikwete ametangaza azma ya serikali kujenga Chuo Kikuu cha Afya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wananchi jana katika Viwanja vya Ukumbi wa Karimjee wakati wa kuzindua Mpango kabambe wa kuboresha huduma ya afya nchini, alisema Chuo hicho, kitaongeza idadi ya wataalamu wa afya nchini.

Alisema mpango huo, lazima uende sambamba na mikakati thabiti ya kuboresha huduma hiyo nchini.

"Maandalizi ya ujenzi wa Chuo Kikuu katika maeneo ya Mloganzira jijini Dar es Salaam
yamekamilika na kitaanza hivi karibuni ili kuongeza idadi ya Madaktari. "Hivi sasa tunatoa madaktari 200 kwa mwaka, baada ya kuanzishwa kwa chuo hicho tutajitahidi angalu tufikie idadi ya madaktari 1,000 kwa mwaka,"alisema Rais Kikwete

wadau, hii mloganzira iko pande zipi hapa dar
Wazo zuri lakini napinga kila kitu kurundikwa Dar. Je kwa nini wasingelikiweka mikoani? mahali kama kanda ya ziwa au Manyara ingelifaa sana.
Lakini kila kitu Dar.
grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Mtu utakuta eti analalamika ofsi na choo za chuo husika hazifai na lawama zinaelekezwa serikali ,mimi nafikiri Walioshindwa si serikali bali wasomi ,wahadhiri na uongozi wa chuo husika ndio umefeli
 
Mkuu upo sahihi ila nadhani maprofessor wenyewe wanatakiwa watafute mbinu ya kuviendeleza hivi vyuo, pana baadhi ya mambo si kuilaumu serikali, hivi jamani kweli serikali ije isimamie usafishaji wa vyoo university? au upatikanaji wa maji? basi pana haja gani akina mukandala kuwepo! tatizo la vyoo ni usafishaji na ugawaji tenda kiholela bila kuangalia muhusika je anaweza kusimamia usafi au la!

kingine ukarabati unafanyika mara nyingi katika vyuo vyetu tatizo lipo palepale ukarabati wa kuripua kwa ajili ya 10%, ni majenereta mangapi yamewekwa UDSM na hayafanyi kazi ipasavyo? ni majengo mangapi yamefanyiwa ukarabati au yamejengwa wakati mfumo mzima wa maji na umeme ndani ya jengo ni tatizo? ni miradi mingapi imekumbatiwa na maprofessor hadi pesa zinarudi kwa wafadhili kwa kuwa hazina cha kufanya wakati hakuna vitendea kazi katika maabara zetu? je bado tunailaumu serikali? Vyuo vyetu tunaviua sisi wenyewe, tuache kuibebesha seerikali mzigo, vyoo vipo UDSM ila havina maji na ni vichafu, nani wakuwasimamia hawa wafanya usafi?[/QUOTE

Nakubaliana na wewe mkuu 100/100
Wengi wanaopinga na kulalamika sana ni ma conservative tu hawana hoja
 
Tilieni mkazo hayo maadishi mekundu

MUHAS comes of age

2009-01-05 11:22:59
By Correspondent

He was happy with the government`s decision to press for MUHAS to be given title deeds for 3,800 acres of land at Mloganzila and Kwembe villages along Morogoro road close to Kibaha township where ultra-modern and huge new MUHAS campus is to be set up in a few years to come.

SOURCE: Guardian

Jiografia ya Kibaha siifahamu vizuri ila naona kuna uwezekano hayo maeneo yapo Mkoa wa Pwani na sio Dar es salaam kama wengi humu wanavyodhani.

My Take: Chuo kama hiki na vingine vingine vijengwe mikoa ya kati kama Dodoma, Tabora na Singida ili kusaidia kuharakisha maendeleo katika mikoa hiyo.
 
Nafahamu wengi nitawakwaza na watanishambulia na nitapenda kusema tena na tena ninayoamini ni ya ukweli.

WAHITIMU /WAFANYAKAZI /WANAFUNZI wengi wa UDSM ni ma conservative sana ningependa kufahamu huwa mnalishwa nini pale.

Sitoshangaa kuona asilimia kubwa karibu 90% ama zaidi wanaopinga kujengwa kwa vyuo vipya wanauhusiano na udsm na wenda watueleze hofu yao huwa imejikita wapi?

Kifupi nielewavyo mimi UDSM imeshuka kielimu kutokana na kukosa ushindani huo ndio ukweli .Huwezi fanya mazoezi tu peke yako harafu ukijiona uko fiti na ukatoka kifua mbele kwamba wewe uko fiti ,ndiyo maana kuna mechi za kirafiki lazima ujipime.

Tanzania imeshuka kielimu kwa sababu ya kung'ang'ania chuo kimoja na kinachoendelea kuonekana kushindwa kudeliver.

Mfano kama unampango wa kujenga nchi ionekane inapendeza nafikiri mwelekeo sahihi si kuendelea kubomoa na kurekebisha vijimiji vilivyolundikana na ku-saturate lazima utafute maeneo mengine huru na yaliyo wazi kuanza kujenga kutokea a-z.

Kunga'ng'ania kuendelea ni vyuo viwili vinavyoelekea ku-saturate ni upotevu wa dira sahihi ktk mapinduzi ya elimu.

JK tuletee vyuo vingi kadri inavyowezekana na tena kama inawezekana kila mkoa lazima iwe na vyuo aghalabu viwili vitatu.

Mkuu mtazamo wako ni genuine wala hauna matata, ni suala la hoja tu. Ukweli ni kwamba kama huwezi kuendesha chuo kimoja kwenye standard zinazotakiwa, utaweza vipi kuendesha vyuo vingi kwa standard hizo. Jibu ni wazi kabisa kuwa haiwezekani. Lingekuwa jambo la maana sana kama kila mkoa ungekuwa na chuo Kikuu, lakini kwanza tungeangalie jinsi tunavyomanage hivyo vingine tulivyonavyo, tumeshindwa ndio maana hata quality ya elimu inashuka. Maabaara, maktaba, madarasa, vitabu na hata walimu haba. Whatis the point of having a another university? Au ndio yaleyale ya kutekeleza ilani kwa kuwarubuni wananchi? Mkuu hapana tutakuwa tunajidhalilisha wenyewe.

Unajua chuo Kikuu sio sawa na barabara. Barabara unaweza kusema tunatakiwa kujenga nyingine japo hii imeharibika, lakini sio chuo na wala sio hospitali. Inabidi tuwe serious

Toka myahudi ameondoka Chuo Kimekuwa kinadorora tu na knaendelea kudoroa tu. Jana tu nilikuwa pale nimeangalia vyooni mpaka vyoo vya wafanyakazi vinakuwa kama vyoo vya uswahilini, etu kuna ndoo na kopo, hicho ndio choo cha chuo Kikuu karne ya 21. Unaweza ukashangaa hicho kipya ndio kitakuwa na choo cha shimo kabisa, au madawati ya saruji. Hata Mkoloni akirudi anaweza kuchukia kweli.
 
Mkuu
Nafikiri tujaribu kuangalia swala hili kwa nyeti zake, TZ imendelea kung'ang'ania infrustructure zake za elimu kuwa na break point moja ya elimu ,yani ya kwamba hii point ikifeli hakuna mawasiliano tena na hili ni kosa kubwa ambao ma conservative walio wengi wa udsm wanaendelea kulikamatilia.

Na hii naamini ndiyo Technical mistake ambayo Tanzania ililifanya na bado inajaribu kulikumbatia na hii iko very connected na msuo msuo wa uchumi na uongozi legevu wenye utapiamulo na ulio fubaa.

Ukweli tutausema japo unauuma UDSM imefeli na kufeli kwake na kwa kuwa TZ ilijiwekea break point moja ambayo ni udsm nayo TZ imefeli ktk nyanja zote kiuchumi,kisiasa,kiungozi,kiuelewa nk.

Kulingana na maelezo yako uliyotabanaisha hapo juu utaona ukweli kuwa udsm imefeli hata ktk mambo ambayo ni core kwao, sifikiri wala sitaki kuamini swala la tenda ya kusafisha vyoo vya udsm linasimamiwa na serkali na wala sitaki kuamini kwamba udsm hawapati fungu nono kutoka serikalini.Hayo mambo uliyayesema ni vielelezo ambavyo vinazidi kuonyesha kwa jinsi gani udsm imefeli.

Nchi endelevu naamini haiwezi kujitia tai kwa kuwa na break point moja ,tunahitaji vyuo vingi ili tuepukane na hii bottleneck ya udsm na hatimaye ushindani ulio hai ktk nyanja zote na wenye tija upatikane
 
Last edited:
Back
Top Bottom