Chuo cha uhasibu arusha chafungwa.

R-CHUGA

Member
Mar 23, 2012
77
8
Ni baada ya machafuko yaliyotokea leo hatimaye chuo cha uhasibu Arusha kimefungwa kwa muda usiojulikana mpaka hapo bodi itakapokaa na kufanya maamuzi.
 
kwahiyo hawataweza muaga mwanafunzi mwenzao au itakua vipi sasa.
 
Sasa ni wazi watu waliopewa uongozi sehemu husika kama ya RC Malongo ni hasara tupu kwa Taifa letu!

Hakika panapovuka moshi kuna moto!
 
Sijajua itakuwaje kuhusu kumuaga mwenzetu ila nadhani kesho asubuhi ntakuwa huko ntapata taarifa zaidi.
 
kama ndugu watachukua mwili kesho na watu hawapo chuo hawaoni itakua ni kuongezea hasira watu
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ni janga kwa Taifa. Huyu jamaa anaendesha Mkoa kwa maslahi ya CCM. Ujinga mtupu.
 
nimeona kwenye news**** kinachonishangaza ni kwanini Lema atafutwe na polisi?....kwanini wameita Breakdown iondoke na gari lake,bila idhini yake?
 
Sina hakika kwa wanazuoni kutukana na kukosa uvumilivu inatoa picha gani kwa wananchi wa kawaida. Na mh Lema kama Mbunge analionaje hili la Amani ya Arusha kutoweka Kila kukicha. kwa sasa hata tu wanafunzi wetu wakifanya vibaya mitihani yao wamekuwa madai mengi ikiwemo ya kutafuta njia hata ya kuandamana kumshawishi mwal alegeze kamba hivi tunakwenda wapi?
 
kama ndugu watachukua mwili kesho na watu hawapo chuo hawaoni itakua ni kuongezea hasira watu

Ulitaka naye agome??? pili tatizo lake nini? mwanafunzi kachomwa kisu wanafunzi wsi waachie polisi? na kama cdm wanajua namna mkuu wa mkoa alipaswa kufanya kwanini mh Lema asitoe ushauri wake? acheni kuwahadaa watoto wa wakulima na kuwafanya wao ni ngazi ya kupandia juu.
 
chuo kimefungwa muda usiojulikana waliokua wanategemea ku graduate?
 
Jamani wacheni tu hicho chuo kifungwe manake watu wamechoka muda mrefu sana huyo mkuu wa chuo ndio mwenye matatizo makubwa na ndio chanzo cha yote. Vita kubwa sana hapo hata kwa wafanyakazi wa chuo wananyanyasika sana bila msaada wowote hata bodi ya chuo imeshindwa kazi wanakula pesa ya taasisi tu wamegeuza chuo shamba la bibi wala haya siyo maswala ya kisiasa hapa kuna uchafu wa kutisha hata ikulu inajua na sijui wanasubiri nini wasimkamate huyo mkuu. Hebu nendeni takukuru mkapewe file lake muone tuhuma zake na kwa DPP bado anahonga eti asikamatwe mpaka sasa hivi file lake lipo kwa DPP MEZANIA linasubiriwa kufanyiwa kazi kumbe anahonga na anawatumia wajumbe wa bodi kumuwekea mambo sawa asipandishwe kizimbani. Ukweli ni kwamba huyu mkuu mpaka sasa inashangaza kwamba analindwa na nani hadi muda huu kwani haistahili kabisa kuwa pale alitakiwa awe ameshafikishwa mahakamani kitambo lakini serikali yetu hii ya CCM imejishushia heshima kwasababu ya kule ujinga na uchafu wa majambazi sugu wanaohujumu nchi. lema hausiki wala mkuu wa mkoa hana shida. wanafunzi wa chuo hawajaanza kuandamana leo jamani ni miaka mingi sasa kwani mmesahau tuhuma ya bodi ya mikopo kwamba fedha za wanafunzi zililiwa? na kuna michango mingi wanafunzi wanachanga kumbe ni michango hewa mkuu huyo ni fisadi wa nguvu na anatuhumiwa kwa ufisadi na ushahidi umekamilika na takukuru wanatakiwa wamkamate haraka sana lakini ukweli ni kwamba mkurugenzi wa takukuru ambaye ni Eliezer Feleshi amekalia file lake bila sababu zozote. Takukuru wameshindwa kumpeleka mahakamani kwasababu huyo mkuu analindwa na bodi ya chuo cha uhasibu akiwepo mwenyekiti wa bodi mwanaidi mtanda. Hivyo bodi hiyo nzima na mkuu huyo wa chuo wanatakiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za chuo hicho na waziri wa fedha anatakiwa sasa kutoka tamko kwani inaonyesha waziri naye ana lakujibu kwani chuo hicho kipo chini ya wizara ya fedha. lakini tuhuma za pale ni nzito mno na zinatisha hata kuliko za kina chenge na mramba. Mkuu huyo kwa sasa yupo india kwa madai ya kikazi lakini ni njia ya kula pesa za taasisi na katika tuhuma za kujibu safari za india ni mojawapo kama hamuamini mkamateni lema ndio mtajua hapo pamekaaje kwani mambo yote sasa yanakwenda kuwekwa hadharani Kwa maelezo zadi soma gazeti la raia mwema mtandaoni kichwa cha habari “KASHFA ZAIDI ZALIPUKA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA. Utaona mambo mazito na bado serikali imekaa kimya bila aibu inalea mafisadi na wakati tuhuma zote zina ushahidi wa kutosha tena wa nguvu sio zile za kusuasua wala sio ushahidi wa kubabaisha kwa mtindo huu CCM haitakubalika huko tuendako wanajiangusha wenyewe chadema watajishindia kwa sababu ya ujinga wa CCM.
 
Back
Top Bottom