Chuo cha SAUT kinara ufaulu Shule ya Sheria

Udsm Huwa sio wengi sana Kwa sabb hata admission Yao Huwa ni ndogo sana kutokana na kuweka passmark za juu sana kuliko SAUT, unaweza kukuta udsm walikuwa 40 law school yote, Wakati SAUT 200
Kama ni hivyo kuwa UDSM wanaweka pass mark za juu basi ningetegemea hao wachache wanaokwenda Law school ndio. wangefanya vizuri na kuwa katika Kundi la wafaulu!! Unfortunately, sio hivyo!
 
Kama ni hivyo kuwa UDSM wanaweka pass mark za juu basi ningetegemea hao wachache wanaokwenda Law school ndio. wangefanya vizuri na kuwa katika Kundi la wafaulu!! Unfortunately, sio hivyo!
Nikupe mfano kama Udsm walikuwa 20 halafu wakatoka first sitting 4 ni sawa na 20%, halafu SAUT walikuwa 300 halafu halafu wakafaulu 10 ni sawa na 10%? Umeelewa?
 
Chuo gani Jurisprudence wanawafundisha mwaka wa kwanza , hivi mtoto katika zake sekondari ndio unaanza kumkandika jurisprudence? Ataelewa sheria gani? Halafu Wana furushi la masomo ambayo sio ya kisheria comparative religions, mara Kifaransa. Mtu anamaliza na cheti kuonekana kafautu Kifaransa lakini ukimuuliza "comment allez vous" hawezi kukujibu
 
Nikupe mfano kama Udsm walikuwa 20 halafu wakatoka first sitting 4 ni sawa na 20%, halafu SAUT walikuwa 300 halafu halafu wakafaulu 10 ni sawa na 10%? Umeelewa?
Hizo hesabu yako za % mbona hazikubaliki!! Wakifaulu 10 out of 300 ni % ngapi? surely sio 10%!!!
 
Naona mnahalalisha ufelishaji wa wanafunzi unaofanywa na law school of Tanzania, makanjanja ni LST brazaj

"Ni jambo la kushangaza sana kwamba watanzania ni jamii ya watu waliojaa wivu, choyo, husuda, fitna, ujinga, upumbavu na ujuaji uliopitiliza." Hao ndiyo unaowaona humu katika ubora wao.

Kwamba wanafunzi ni vilaza? Kwani huo ulaza unaanzia na kuishia LST tu? Mwanafunzi bora kabisa kutoka Havard University ana uwezekano mkubwa kufeli LST. Huyo naye ni kilaza?

Matokeo yake tatizo linakuwa ni tatizo tu kama yeye binafsi au jamaa zake wameathirika na tatizo hilo moja kwa moja.

Kwamba kwa mtanzania mkuki ni kwa nguruwe tu kwa binadamu mchungu!

Inasikitisha zaidi kuwa wanafunzi LST wanashindwa kuumaliza upuuzi huku wakati uwezo huo hata leo wanao:

Wanafunzi Law School mnayo nafasi ya kujipigania

Bila shaka wanadhani wanaofeli kila mwaka ni wale tu, siyo wao. Yatakapowakuta itakuwa ni vyema wakajiandaa kukaa kimya. Tena kwa kutulia.

FutD12pWIAEjDDU.jpeg


Ukondoo huu hadi lini?

Kwamba wanamsubiri nani kuwapigania? Watanzania hawa wenye kujaa husuda na ujuaji uliopitiliza?
 
Hamna namna unaweza kulinganisha SAUT na UDSM kwenye kada ya sheria mkuu. Nimewahi kutana na wanafunzi wengi wa SAUT mwaka wa 4 hata plaint hajui kuandika, Ukimpa ajibu WSD ndo utacheka, ukitaka vituko mpe kazi aandae Charge, hata ku identify offence hajui.

Sijawahi kukutana na Hali kama hiyo Kwa wanafunzi wa UDSM na Mzumbe.

Hizo story za chuo flani kutoa watu wengi Huwa ni stori za vijiweni na wakufunzi Km mtaalamu Shonga au Don chuwa wakiziskia Huwa wanacheka sana Kwa dharau maana uhalisia ni tofauti.

Sijasoma UDSM lakini Kwa sheria UDSM na MZUMBE bado ni best Kwa nchi yetu Angalia hata wanafunzi wanaochukua, ni wachache na wanaufaulu mzuri hivyo rahisi kufundishika tofauti na SAUT ambao ni zoa zoa mpaka D 2 anaenda kusoma Ll.b

Ll.b3 wa mwaka huu SAUT wapo Karib 1000plus unadhani mazingira ya kujifunza yatakuwa rahisi kulinganisha na chuo kama UDSM wanachukua watu 100 ni wote ni Division one?
SAUT walichokosea ni kujaza wanafunzi wengi kwenye sheria. Huwezi ukawa na wanafunzi 1000 kwenye sheria Hilo ni kosa kubwa.
 
Mkuu bado nasema hizo data za mtoa mada sio sahihi, ni story za vijiweni, japo sikatai kuwa Kuna watu pia kutoka SAUT Huwa wanatoka first sitting pia, mfano Kwa cohort ya 34.

Kuna mtu namjua katoka first Sitting ni mhitimu wa SAUT. Pia najua wengine wanne waliotoka Mzumbe na UDOM.

Hizo story Huwa zipo miaka yote, mwanzo waliokuwaga na tabia ya kueneza huo uongo Ili waonekane wa maana walikuwa UDOM maana college ilikuwa mpya ko walikuwa hawataki waonekane wapo nyuma, lakini Kwa Sasa wamestaarabika.
Hata Mimi nadhani ni hearsay za watu. Sidhani Kama Kuna ukweli wowote hapo. Ni vigumu kujua chuo gani waliofaulu wametokea.
 
Mleta mada (mwandishi) hayuko makini katika uchambuzi wake.
Alipaswa kutuambia hiyo idadi ya wahitimu waliofaulu Law school kutoja SAUT ni kati ya wahitimu wangapi kutoka SAUT ambao walijiunga Law school.
(Note: SAUT ndio chuo kinachodahili wanafunzi wengi zaidi wa shahada ya sheria, na ndio kinachotoa wahitimu wengi zaidi wa sheria, ndio kinachoongoza kuandikisha wanafunzi wengi zaidi kuanza mafunzo pale Law school, itakuwa maajabu kama wengi watakaofaulu Law school hawatatokea SAUT)

Kwa mfano, embu tuwaze tu, labda
Wahitimu wa SAUT waliojiunga Law school walikuwa 500, kati yao waliofaulu ni 10 (hiyo ni sawa na 2%)

Wahitimu wa vyuo vingine (UDSM, Mzumbe, Tumaini nk) waliojiunga Law school walikuwa 321, kati yao waliofaulu ni 14 (sawa na 4.4%).

Ni vipi utaiona SAUT ni bora zaidi ya wengine?
Good analysis mkuu
 
Kule malecturer wanapishana darasani kama wanafundisha seminari kwa kweli warumi kwenye swala la elimu wapo vizuri sana. Waliniudhi tu kutuwekea magrade makubwa ya ufaulu wakati vyuo vingine grade zao zilikuwa chini tulipambana kweli watubadilishie walikataa wakawashushia wale wa nyuma yetu. Nilikwenda pale sijui kiingereza hasa tenses aiseee madam Munga ashukuriwe sana.
Poleni Sana kwa kuwekewa grade kubwa.
 
Udsm Huwa sio wengi sana Kwa sabb hata admission Yao Huwa ni ndogo sana kutokana na kuweka passmark za juu sana kuliko SAUT, unaweza kukuta udsm walikuwa 40 law school yote, Wakati SAUT 200
Huu ndio ukweli kabisa.
 
Kama ni hivyo kuwa UDSM wanaweka pass mark za juu basi ningetegemea hao wachache wanaokwenda Law school ndio. wangefanya vizuri na kuwa katika Kundi la wafaulu!! Unfortunately, sio hivyo!
Duuuuh! Watu mnakaba kila kona.
 
Back
Top Bottom