Chumba cha kulala kinatakiwa kiwe na ukubwa gani standard?

Shamkware

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
1,740
2,243
Habari zenu wajenzi na mafundi wa humu Jf,

Naombeni msaada kutoka kwa anaejua shida yangu ni kujua Ukubwa gani unafaa kuwa ukubwa wa Chumba Master na pia chumba bila master kinapaswa kuwa na ukubwa upi kiufundi tafadhali sana
 
Ukubwa utategemea na mahitaji ya chumba chako, unaweza ukasketch plan ya vitu vitakavyokaa kwenye chumba mfano kutakuwa na kitanda kimoja cha 5ft kwa 6f, meza moja ya 2.5ft by 3ft, kabati moja la 1ft by 5ft n.k

Utavipanga hivyo vitu vyako, na kuacha nafasi kati ya item moja na nyingine ili upate access ya kupita, baada ya hapo utakuwa umepata size ya chumba

Common sizes
Chumba cha kawaida 9ft kwa 9ft au chini ya hapo
Chmba cha wastani 10ft kwa 10ft
Chumba kikubwa 12ft kwa 12ft na zaidi

Kwa mahitaji ya ramani, makadirio au ushauri tuwasiliane
 
Shukrani sana mkuu
 
Duuuu... Hlo chumba ni likubwa sanaaaa..... Unamdanganya mwenzako...

Standard ni 3x3m2 au kama master ni 3.5x3.5m2..

Hyo hapo ndio normal standard... Ila kama unataka bangaroo 4x4m2
Yaani master bedroom unaweka 3.5mx3.5m ? Aisee utakuja kuichukia hiyo nyumba. Master bedroom lazima iwe na ukubwa wa kutosha, hata ukitaka kuweka lounge ndani ya master unaweka
 
Cheki hiyo master ina 4.8x4.8
Screenshot_20230903-114812_1.jpg
 
Mimi nimejenga master inaukubwa wa 5.3×3.8M²
Kingine ni 4.2×2.8M²
Cha mwisho ni 3.1×4.2M²
Choo ya public ni 5×1.8M²
Choo iliyokwenye master ni ndogo sana. Yenyewe ni 4×1.2M²
Nakubaliana na wewe kwenye vipimo vya master, lkn hao wanaosema master iwe 3.5x3.5 sikubaliani nao.
Mtoa mada nakusisitiza kama kiwanja kinaruhusu na uwezo kifedha unao hakikisha master yako haipungui sqm 20
 
Master ikiwa kubwa inauzuri wake. Japo mimi bado ipo kwenye level ya boma lakini nqfurahi chumba kinaonekana kitapendeza baada ya kuisha
 
Habari zenu wajenzi na mafundi wa humu Jf,

Naombeni msaada kutoka kwa anaejua shida yangu ni kujua Ukubwa gani unafaa kuwa ukubwa wa Chumba Master na pia chumba bila master kinapaswa kuwa na ukubwa upi kiufundi tafadhali sana
Kwavile hatujui budget yako, we jenga kulingana na pesa yako. Chumba kinaweza kuwa na ukubwa wowote unaotaka wewe. Hakuna standard ya ukubwa wa chumba.
 
Haya mambo yanaendena na mahitaji ya mtu. Kwanza nashangaa sana mtu anauliza swali kama hili. Chumba cha kulala hakina size maalum. Ni uamuzi na mahitaji ya mjengaji.
Upo sahihi sana, lkn mtu mwenye chumba kidogo yupo kwenye hasara tofauti na mwenye chumba kikubwa.

Sasa hivi utasema unajenga kidogo kwa sababu ya mahitaji yako lkn kesho mahitaji yakiongezeka utatamani chumba kikubwa halafu ndo huna.
Au imagine nyumba unaipangisha au unataka kuiuza unaweza ukakosa mteja kwa sababu vyumba umevifanya vidogo sana.

Mwenye uhitaji wa chumba kidogo akipewa kikubwa hana shida lkn mwenye uhitaji wa chumba kikubwa ukimpa kidogo ni tatizo. Hivyo ni bora chumba kiwe kikubwa hata kama uhitaji wako kwa sasa ni wa chumba kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom