Issue wewe una allergy na dawa zenye sulpher please usinywe dawa hizo ok wengine haiwaletei madhara unawasaidiaje sasaKuna dawa ya kutibu malaria maarufu inayojulikana kwa jina la MALAFIN
View attachment 457836
Hiyo dawa hapo juu ndani ina vidonge viwili na huwa inauzwa kwa bei ya sh 1500, na sehemu nyingine huwa ni sh 2000.
Baada ya kuitumia kwa zaidi ya mara tatu, kila muda ninapoitumia imeniletea madhara ikiwemo uvimbe kama mvilio wa damu kwenye kichwa cha uume na ngozi ya uume kuchubuka. Pia mdomo nao kwenye lips kumetokea mchubuko na mvilio wa damu.
Baada ya kwenda hospitali kuonana na doctor kumuelezea hali yangu ilivyo baada ya kuitumia ile dawa nliyonunua pharmacy. Doctor aliniambia kuwa hizo dawa ni hatari sana na zinaweza kupofua macho na hata kuharibu system ya nguvu za kiume na akanitaka iwe mwanzo na mwisho kuzitumia kwa usalama wangu
USHUHUDA
Baada ya kuelezea hili tatizo kwa watu wengine kuna baadhi nao wamesema limeshawatokea. Zaidi ya watu watatu waliniambia kuwa nao tatizo hili liliwapata.
My take
TFDA kama mnadhani huu uzi ni wa kuchafuliana biashara, chukueni sample ya hizi dawa zilizozagaa nchi nzima na huko kwenye mapharmacy ndio zinauzwa kama njugu na watu wanazinunua sana kwa sababu ni bei rahisi.
Baada ya kuzichukua zifanyieni uchunguzi ikibidi na nyie mnywe kabisa ili muone matokeo yake. Hizi dawa ni feki matokeo yake ndio magonjwa ya cancer yanayotuuwa kila siku.
Chukueni Tadhadhari
ndio ilikua dawa yangu na nilipata matatizo ya nguvu mwaka 2005 sasa sijajua ni hii au kujichuaMie hutumia hiyohiyo na inaniponesha bila tabu
Asante dr. kwa mawazo mazuri. Hata dukani kwangu ninazo japo nazitoa kwa mama mjamzito tu.Ndugu zangu tatizo sio dawa ila tatizo ni watumiaji wanakuwa na mzio (allergy) na dawa hizo, kiufupi wanakuwa allergic to sulphur. Ingawa dawa hizo hazipendekezwi na wizara ya afya ya Tanzania kwa matibabu ya malaria. Ila inaweza kutumika kwa wajawazito kama kinga tu.
Mimi natumia hiyo hiyo ya waja wazito na napona, mseto kwa kweli siwezi kutumia, vidonge vingi hatari!!Pole sana.
Kwanza nikujulishe ya kuwa dawa hiyo imeshaondolewa katika dawa za kutibu malaria na kwa sasa inatumika kama kinga kwa kina mama wajawazito tu (angalia vizuri box lake na utaona for intermittent prevention of malaria in pregnancy).
Kuhusu yaliyokupa ni kuwa umepata reaction ya sulphur na uwe mwangalifu kwa dawa zote zenye sulphur na mueleze daktari wako kabla hajakuandikia dawa.
Dawa ya kutibu malaria isiyo kali ni MSETO au ALU igawa waswahili tunapenda rahisi hata katika manbo magumu na wengi wanaikimbia ALU kwa wingi wa vodonge.
Dawa inapoondolewa kwa ajili ya kushindwa kutibu haina maana kuwa ni asilimia mia.Kuna kiwango ambacho kikifikiwa inabidi iondolewe kwani inahatarisha maisha ya wengi kwa manufaa ya wachache kama wewe.Mimi natumia hiyo hiyo ya waja wazito na napona, mseto kwa kweli siwezi kutumia, vidonge vingi hatari!!
Wataalamu wenyewe nao ni wasanii tu, Mara chloroquine, Mara quinine, Mara fansida, mara SP, mara mseto, muda si mrefu tutaletewa zingine na kuambiwa mseto haifai!Dawa inapoondolewa kwa ajili ya kushindwa kutibu haina maana kuwa ni asilimia mia.Kuna kiwango ambacho kikifikiwa inabidi iondolewe kwani inahatarisha maisha ya wengi kwa manufaa ya wachache kama wewe.
Kitakachotokea ni kuwa ukipata malaria iliyosababishwa na strain (?vinasaba?) ambayo ni sugu kwa SP unayoipenda ina maana ya kuwa utakuwa unasubiria kupona wakati wadudu wa malaria wanaongezeka na hii inaweza kukusababishia kufikishwa hospitali kwa malaria kali ambayo itakuwa inahatarisha maisha yako.
Tujifunze kuwasikiliza wataalamu.
Hakuna usanii ndugu yangu.Kuna mengi ambayo yanafanyika na ni vigumu kwa raia wa kawaida kuelewa.Miaka ya mwanzo ya UKIMWI ilikuwa mwanamke akigundulika na VVU jambo la kwanza ni kuwa asishike mimba lakini leo mama na baba wenye VVU wanapata mto ASIYE NA VVU,tumshukuru Mungu kwa hili kwani watu hawatakufa bila watoto kwa ajili ya kuwa na VVU.Jambo hili halikutokea kwa bahati ni tafiti nyingi na za gharama kubwa zilizofanywa na hao unaowaita WASANII.Mifano ni mingi lakini kumbuka kuwa wakati umelala usiku wa manane kuna watu wako macho wakihangaika kukabiliana na shida za binadamu.Wataalamu wenyewe nao ni wasanii tu, Mara chloroquine, Mara quinine, Mara fansida, mara SP, mara mseto, muda si mrefu tutaletewa zingine na kuambiwa mseto haifai!
Mkuu kunywa bia mbili hapo nitakuja kulipa.Dawa yoyote haiwezi kuondolewa sokoni kwa sababu ya madhara anayoyapata mtumiaji mmoja mmoja bali kwa kuthibitika kuwa dawa husika haina uwezo wa kutibu ugonjwa ambao dawa ilitegemewa ingetibu.
Kwenye kila dawa huwa wanatoa tahadhari kuwa usitumie endapo itakuletea mzio/allerg au hata reaction yoyote sasa wewe baada ya kukuletea mzio ukaendelea kutumia halafu unawataka TFDA wachukue hatua? hapo ni sawa na uvute sigara ikuletee madhara halafu utegemee kulalama kwa mamlaka husika wakati umeona onyo.
Zaidi ya yote MALAFIN ni intermittent preventive therapy of malaria in Pregnant ambayo inatumiwa na wamama wajawazito kuzuia maambukizi ya malaria nimeshangaa kuona wewe mwenzetu bolo lako likaivia damu hayo ndio madhara ya kununua dawa mitaani mkipatwa na madhara mnaanza kulaumu mamlaka
Ina maana mpaka hapo hujaelewa Maelezo ya watalaamu????Hata Mimi ilishawahi kunitokea zaidi ya Mara mbili, hivi sasa nimeacha kabisa kunywa hayo madawa feki.
Nikidhani ni Mimi peke yangu kumbe tupo wengi.
Nipo tayari kutoa ushirikiano wa kuthibitisha madhara ya hizo dawa.!
Wafanyabiashara wa madawa mpo kazini
We naeleza kabisa kuwa zaidi ya watu watatu nnaowafahamu wanasema tatizo wamekutana nalo
Je wengine ambao sijawaho kuwaona?