Christiano Ronaldo anaacha mzigo mkubwa kwa kizazi kijacho

Encryption

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
996
1,339
Alfredo Di Stefano ni mmoja kati ya watu wanaoheshimika sana katika club ya Real Madrid. Kwa miaka yote 11 aliyodumu akiwa mchezaji wa Real Madrid, Di Stefano alicheza kwa mafanikio makubwa sana. Yeye pamoja na Francisco Gento na José María Zárraga ndio waliobeba mafanikio makubwa waliyoyapata Real Madrid kwenye miaka ya 1950.

Alfredo Di Stefano alikua ni mshambuliaji anayefunga magoli mengi, yeye ndiye aliyekua mfungaji bora wa La Liga kwa miaka mitano mfululizo, kati ya mwaka 1954-1959. Huku pia akiisaidia Real Madrid kutawala soka la Ulaya kwa kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa miaka mitano mfululizo, akifunga goli kwenye kila fainali. Alitwaa pia tuzo ya Ballon d'Or mara mbili mwaka 1957 na 1959.

Kiufupi Di Stefano ni alama ya mafanikio yaliyopo ndani ya club ya Real Madrid. Ni mtu anayeheshimika sana. Mwaka 2000 alitangazwa kama Rais wa heshima wa Real Madrid. Huyu ndiye mchezaji pekee mwenye tuzo ya heshima ya Super Ballon d'Or. Tuzo aliyopewa na chama cha soka nchini Ufaransa mwaka 1989. Hakuna mchezaji mwingine mwenye Super Ballon d'Or.

Alfredo Di Stefano ni mchezaji namba tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Real Madrid, akiwa nyuma ya Cristiano Ronaldo na Raul Gonzalez. Di Stefano ana jumla ya magoli 308 kwenye mashindano yote.

Rekodi yake ya ufungaji bora wa muda muda wote Real Madrid ilidumu kwa zaidi ya miaka 50 kabla ya Raul Gonzalez hajaivunja mwaka 2008. Rekodi yake ilidumu sana. Walikuja washambuliaji wengi Real Madrid wakaondoka, wote hawakuweza kuyafikia magoli yake 308.

Alikuja Ferenc Puskás akashindwa, alikuwepo Pirri akashindwa, alikuja Hugo Sánchez akashindwa, alikuja Carlos Santillana akashindwa, alikuja Emilio Butragueño akashindwa na hata hawa kina Ruud Van Niestrooy na Ronaldo De Lima wote walishindwa. Ni Raul ndiye alikuja kuivunja tena baada ya kuichezea Real Madrid zaidi ya mechi 500.

Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji anayeshikiria rekodi ya ufungaji bora ndani ya club ya Real Madrid akiwa na magoli 439 aliyofunga kwenye mechi 428 Tu. Hii ni sawa na kwamba Ronaldo amefunga kwenye kila mechi aliyocheza na amebakiwa na magoli 11 ya ziada. Ajabu sana Hii. Idadi ya magoli aliyoyafunga ni mengi kuliko idadi ya mechi alizocheza.

Wakati rekodi ya Raul Gonzalez akiivunja rekodi ya ufungaji bora ya Real Madrid iliyodumu kwa zaidi ya 50, Cristiano Ronaldo yeye alitumia miaka sita Tu!! Kuivunja rekodi ya Raul Gonzalez ya magoli 323. Alifanya hivi kwenye mechi dhidi ya Levante October 2015.

Mbali na rekodi hiyo, Cristiano Ronaldo amekua na idadi kubwa rekodi nyingi anazozishikilia hadi sasa. Yeye pia ni anayeongoza kwenye ufungaji bora wa muda wote wa UEFA Champions League akiwa na magoli 117. Ni Cristiano Ronaldo tu anayeshikiria rekodi ya kufunga zaidi ya magoli 50 kwenye misimu saba mfululizo. Huyu pia ana jumla ya tuzo za Ballon d'Or Tano. Kifupi Ronaldo ana rekodi nyingi sana, zaidi ya mia moja.

Cristiano Ronaldo itafika muda ataondoka, anaachana na soka na kufanya mambo mengi, huku nyuma aatacha mambo makubwa sana ambayo itakua ni ngumu sana kwa wachezaji watakaokuja. Rekodi zake zitadumu kwa muda mrefu sana hasa kutokana na kwamba kizazi hiki bado hakina mchezaji anayeonakana kufanya vizuri zaidi yake. Messi na Ronaldo wameendelea kutawala soka la dunia kwa miaka 10 sasa. Ndani ya miaka hii hakuna mchezaji mwingine anayeoneka kuwasogelea.

Hata katika umri wake huu wa miaka 33 bado Ronaldo ameendelea kuwa na Ubora uleule na kasi yake ya ufungaji magoli haijapungua. Bado anendelea kushindana na kizazi hiki cha kina Harry Kane kwenye idadi ya magoli anayoyafunga.

Ronaldo anaendelea kuwa bora kutokana na faida ya ujanja wake anaotumia. Akiwa na umri huu anatambua kabisa hana kasi ile aliyokua nayo akiwa na miaka 23. Anachokifanya sasahivi ni kutumia nafasi zaidi katika ufungaji wa magoli. Anacheza na movements za kina Marcelo, Carvajal, Toni Kroos, Isco na Luka Modric tofauti na mwanzo ambapo alikua na uwezo wa kukimbia kwa kasi kisha kuachia makombora ya hatari.

Si ajabu tukiona anatwaa tena tuzo nyingine nyingi kabla hajastaafu. Huku pia akiendelea kutengeneza rekodi nyingi kwenye maisha yake ya soka. Huku nyuma ataacha mzigo mkubwa sana kwa kizazi kijacho kuweza kufanya kama anavyofanya sasa.
 
Ronaldo is the best goal scorer of all time.

Messi is the best football player of all time!

One is a goal machine, and the other is a team engine!

Nina bahati sana kuwashuhudia hawa jamaa wakicheza katika viwango bora kabisa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom