Chonde chonde nguvu ya umma....

tutanyonywa mpaka lini?watu wanaishi maisha magumu hata mlo mmoja ishu halafu we unaongelea kuogopa vita?au wewe ni kati ya wale wachache walio ktk upande unaobenefit?hapa vyovyote vile na iwe lakini lazima ifike wakati twende sawa.tumechoka kua chini kila siku.tukimbizane heshima irudi ili tusichezewe movie za kijinga kama ilivyo sasa hivi
Hivi hujui kuwa vita vikitokea watakaoathirika ni Mbowe na Ndesambulo? Waulize jama wako tayari. Na tupe orodha ya walioifisadi nchi na uombe wanajf wakuongeze kwenye orodha yako wanaofikiriwa kuwa ndo mafisadi. Utashangaa kwenye yako akitokea mwanajf akataja WAKRISTO ndo wameifisadi nchi hii kwa kuwa wameshikilia nafasi zote za maamuzi. Be careful ndg yangu unachotamani, kikianza huwa hakina dereva.
 
Ni jukumu la serikali ya ccm, kuzuia adha ya machafuko isitokee, rais si tunae, na nahodha mzuri huonekana chombo kinapoenda mrama, sasa ndio tuone umahiri wa JK ktk ku-manage crisis, kama ataamua kukaa kimya kama ilivyo kawaida yake pia sawa. Wahenga walisema 'a good manager is the one with plan b not with the plan'.
 
Amani iko wapi?
1.Watanzania wanashindia mihogo,
2.kinamama wanakufa kwa kukosa huduma bora ya afya,
3.watoto wagonjwa walioko kwenye oksijen wanakufa kwa kukatika kwa umeme,
4.wazee wastaafu waliotumikia taifa hawana thamani ya utu wao,
5.mtoto wa maskini anaishia fom 4 ya shule ya kata akiwa na div zero.
6.muajiriwa wa serikali halipwi kwa kiwango stahiki na pia halipwi stahili zake kwa wakati,

jamani hivi hii amani inayosemwa ni ipi?

Mwizi wa kuku manzese anatiwa kitanzi cha tairi la moto huku lifisadi papa linainuliwa mkono na kusafishiwa tuhuma zake.
Amani na utulivu uko wapi?

Wimbo huu wa amani umefanya watanzania wasiheshimiwe,

tanzania ya leo hata wasio na vinasaba vya ufisadi wamekua mafisadi kwa sababu ya 'amani'

wakati umefika kwa NGUVU YA UMMA kurudishiwa heshima yake,sioni tatizo kwa nguvu ya umma kuonyesha MAKUCHA YAKE ambayo ni makali mno.

"mliwapumbaza mababu zetu kwa miaka 50, hamtaweza kuendelea kutupumbaza kwa miaka iliyobaki".......c..h...a...n...g...e...i...s...c...o...m...i...n...g...
 
schizophrenic mind,
hivi ninyi mlishashindwa kuongelea jingine zaidi ya amani?
Ni amani gani hiyo huku nakufa na njaa??
ni amani gani hiyo huku sina kazi ?
ni amani gani hiyo ninapoona jana naona ni bora ya leo?
ni amani gani hiyo hata psea za chuo hatuna?
je mnayosema amani ni ipi?
 
Mkuu nimekupata vizuri tu, umeangalia madhara ya vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini? Kenya walipojaribu kumtoa Kibaki ili Odinga awe raisi, yalitokea machafuko na waliokufa ni watu wa chini sana kama mimi na wewe. Wengi walichomewa nyumba na hadi leo hii nothing has change na hali imekuwa mbaya x2.

Baada ya fisadi ya Mobutu kuangushwa Congo, kuna lililochange??

Tusifanya masihara kuombea machafuko kupitia nguvu ya umma huku tukipandikizana chuki za kidini.
 
Kwa yanayojiri Libya, nguvu ya umma inaweza kuturudisha kwenye umaskini zaidi ya huu tulio nao. Uharibifu wa mali, uhalifu na kuuana hovyo ni mambo yanayopewa nafasi ya mbele. Kwa mnaopendekeza nguvu ya umma itumike kuondoa mafisadi, chonde chonde tusije ingiza nchi matatizoni kivita na kuwa wakimbizi, sijui tutakimbilia wapi manake kwa majirani zetu karibu kote ni instabilities.
Tanzania kisiwa cha amani nakupenda sana.

Basi tuwe tayari kubakia hapo hapo tulipo kwa sababu tunashindwa hata kusoma alama za nyakati. Leonardo, unaweza kunitajia hata nchi moja ambayo imeweza kuendelea kwa kukiruhusu kikundi kidogo che walafi kula hadi kuvimbiwa huku watu wake walio wengi wakilala njaa. Historia yatufundisha kwamba njia pekee na mwafaka wa kujikwamua kutoka mikononi mwa hawa manyang'au ni ya kutumika kwa nguvu ya umma kuuangusha utawala wao wa kidhalimu. Hao watawala yawezekana waamini hawawezekaniki lakini ni ujinga wao tu unaowapa upofu wa kutoona ukweli kuwa ni swala la muda tu, Mubarak alijaribu sana lakini hiyo tsunami, mmh !

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa hakuna nchi hata moja popote ulimwenguni iliyoweza kufanikiwa kukidhibiti kikundi cha mafisadi kama cha CCM kwa njia ya amani na ututlivu. Hivi sasa tunashuhudia nguvu za dola zinavyotumika Libya kujaribu kunyamazisha sauti ya umma hata ikibidi kulitumia jeshi linalotakiwa kuwalinda wananchi sasa linawageuka na kuanza kuwawinda kama wanyama. Hata hapa Tanzania mwaka jana tulishuhudia msemaji wa JWTZ akiwatisha wananchi kuwa wangekiona cha mtema kuni kama hawaengeikubali CCM. Alichokuwa anasema Shimbo ni kuwa kazi kubwa ya jeshi ni kumlinda Kikwete na wabia wake madarakani.

Juzi juzi tena tumelishuhudia jeshi la polisi likiwashambulia Watanzania kwa risasi na mabomu na leo tumemsikia Jakaya Mrisho Kikwete akitishia kuwashughulikia wananchi kama wataendelea kudai haki. Ndivyo hivyo zilivyo serikali zote dhalimu na zisizotenda haki zinavyokuwa tayari kutumia njia zozote zile ziweze kubaki madarakani kwani ndiyo salama yao. Kwa bahati nzuri tunao watu wachache nchini ambao wako tayari kusimama kuhesabiwa na kuita koleo koleo hata kama kwa kufanya hivyo wanahatarisha maisha yao na ndugu zao. Ukweli utabaki pale pale kwamba nguvu ya umma ni supreme na hata kwa huyo Gaddafi sasa ni swali la muda tu.
 
Leonardo is living in the past, and is a beneficiary of the rotten regime currently operating in the country.
Broda, its time for change, and we do not gonna look back this time...
Better we be in turmoil for some period than continuing being used by some few families!
 
Basi tuwe tayari kubakia hapo hapo tulipo kwa sababu tunashindwa hata kusoma alama za nyakati. Leonardo, unaweza kunitajia hata nchi moja ambayo imeweza kuendelea kwa kukiruhusu kikundi kidogo che walafi kula hadi kuvimbiwa huku watu wake walio wengi wakilala njaa. Historia yatufundisha kwamba njia pekee na mwafaka wa kujikwamua kutoka mikononi mwa hawa manyang'au ni ya kutumika kwa nguvu ya umma kuuangusha utawala wao wa kidhalimu. Hao watawala yawezekana waamini hawawezekaniki lakini ni ujinga wao tu unaowapa upofu wa kutoona ukweli kuwa ni swala la muda tu, Mubarak alijaribu sana lakini hiyo tsunami, mmh !

Kinachosikitisha zaidi ni kuwa hakuna nchi hata moja popote ulimwenguni iliyoweza kufanikiwa kukidhibiti kikundi cha mafisadi kama cha CCM kwa njia ya amani na ututlivu. Hivi sasa tunashuhudia nguvu za dola zinavyotumika Libya kujaribu kunyamazisha sauti ya umma hata ikibidi kulitumia jeshi linalotakiwa kuwalinda wananchi sasa linawageuka na kuanza kuwawinda kama wanyama. Hata hapa Tanzania mwaka jana tulishuhudia msemaji wa JWTZ akiwatisha wananchi kuwa wangekiona cha mtema kuni kama hawaengeikubali CCM. Alichokuwa anasema Shimbo ni kuwa kazi kubwa ya jeshi ni kumlinda Kikwete na wabia wake madarakani.

Juzi juzi tena tumelishuhudia jeshi la polisi likiwashambulia Watanzania kwa risasi na mabomu na leo tumemsikia Jakaya Mrisho Kikwete akitishia kuwashughulikia wananchi kama wataendelea kudai haki. Ndivyo hivyo zilivyo serikali zote dhalimu na zisizotenda haki zinavyokuwa tayari kutumia njia zozote zile ziweze kubaki madarakani kwani ndiyo salama yao. Kwa bahati nzuri tunao watu wachache nchini ambao wako tayari kusimama kuhesabiwa na kuita koleo koleo hata kama kwa kufanya hivyo wanahatarisha maisha yao na ndugu zao. Ukweli utabaki pale pale kwamba nguvu ya umma ni supreme na hata kwa huyo Gaddafi sasa ni swali la muda tu.

Sijapinga nguvu ya umma, ila nimeweka wazi kuwa kama nguvu ya umma italenga uhalifu, kuharibu na mauaji basi umaskini tulio nao utaongezeka mara mbili. Tuombe jeshi na polisi wawe upande wa raia la sivyo nchi itaingia kwenye machafuko.

Polisi na wanajeshi wapewe somo la uraia jinsi ya kudeal na nguvu ya umma kama itatokea hivi punde......
 
Vipi unaogopa kufa kwa njia ya risasi??? au kufa na njaa pamoja na familia yako na kizazi chote cha kwako chote??? lakin ujumbuke kuwa utawaacha wenzako wakila vzr na kuendelea kula gud tym na kuja kujenga maghorofa juu ya kaburi la kwako, mtoto na mkeo. CHAGUA then uangalie, je tuache au tuanzishe noma ya kuwaondoa hao wenzio kabla hawajaja kujenga maghorofa juu ya kaburi lako. Ama kweli unahtaji darasa la Uraia!
 
Kwa yanayojiri Libya, nguvu ya umma inaweza kuturudisha kwenye umaskini zaidi ya huu tulio nao. Uharibifu wa mali, uhalifu na kuuana hovyo ni mambo yanayopewa nafasi ya mbele. Kwa mnaopendekeza nguvu ya umma itumike kuondoa mafisadi, chonde chonde tusije ingiza nchi matatizoni kivita na kuwa wakimbizi, sijui tutakimbilia wapi manake kwa majirani zetu karibu kote ni instabilities.

Tanzania kisiwa cha amani nakupenda sana.

Nchi zote zilizotuzunguuka walianza UPYA na sasa wanaendelea mbele kuliko sisi tunaodai kuwa kisima cha amani wakati Gongo La mboto watu wanalala nje!
 
Back
Top Bottom