Chonde chonde mliopo vyuoni!!

Zyamwelele

JF-Expert Member
Aug 5, 2013
405
153
Habari zenu wabunge wa hili jukwaa!!
Kwamda mfupi niliokwepo chuo niliona yafuatayo;

1) Maisha ya wanachuo wengi niyakuigiza (hayana uhalisia)
2) Matarajio ya wanavyuo wengi ni makubwa kama sera ya elim ya sasa yaan (big results now). kitu ambocho ni tofauti na hali halisi ya huku mtaani.
Taanza nahayo mawili kwaleo!
Mawazo hayo yapo hasa kwawanafunzi ambao ni freshers (fresh from school)
kiukweli ukikaa kuwasikiliza mawazo yao kama umeshapitia maisha ya mtaani utawaonea huruma' kwasababu wanayoyafikilia ni tofauti kabisa na hali halisi ilivyo!!
Wengi wao wanafikiria baada ya shule ajira' na baada ya miezi kazaa usafiri.
Chondechonde nduguzanguni huku mtaani kugum hatari' huku kuna sera mpya isemayo 'HAIJARISHI UMESOMEA NINI AU UNAJUA NINI ILA UNAMJUA NANI?'' (IT DOES NOT MATTER WHAT YOU KNOW BUT WHOM YOU KNOW).
Ushauri!! Kama unataka kuajiriwa andaa mazingira kwa kujuana na watu' hasa wale wazee ambao unasoma nao lakini tayari wapo kwenye ajira' wape madesa uwasaidie watakukumbuka mkimaliza, ukijifanya nunda imekula kwako!!

Kingine maisha mazuri sio kukaa ofisin' waliojiajiri wanakula bata na wanamaisha mazuri balaa.

Vinginevyo uwe na bahati ya mtende' maisha yaweza kuwa kama ndoto zako.

Nimemaliza.
 
Umeandika kimazabe ila umeeleweka... ni kweli mtaani pagumu ila ndio inategemea na bahati ya mtu pia, wengine hawamjui mtu na wanapata zali sehem nzuri tu..acha wa-dream tu it comes true sometimes
 
upo sahihi mkuu,nadhani ujumbe umewafikia wahusika

MADENTI HUKO VYUONI

Hakika sisi wazazi,mno mwatufedhehesha,
Madenti wa siku hizi,sana mwatunyong'onyesha,
Kwanza ni hayo mavazi,kweli mwatuaibisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Madenti huko Vyuoni,bure mwajidhalilisha,
Mwazurura mitaani, na usiku "kujirusha",
Mkifeli Mitihani,Mwalimu "kanikomesha"!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Haiba ya Mwanafunzi,siku hizi imekwisha,
Si kama za kwetu enzi,mengi tulijiepusha,
Masomo tuliyaenzi,tulisoma tukakesha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Zimewajaa tamaa, kuharakia maisha,
Chumbani vitu hujaa,wenzenu kuwaringisha,
Usiku ndio balaa,mambo yenu yanatisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.


Zama hizi kuna ndwele,tena zinapukutisha,
Si kwamba naona gele,bali ninawakumbusha,
Malizeni kwanza shule,anasa hazitakwisha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Kaditamati Madenti,maongezi nafupisha,
Wavulana na mabinti,Betord na Mwanaisha,
Msicheze na wakati,jueni mwajipotosha!
Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.

Lambert F. Chialo( Mhadhiri wa Malenga)
Magogoni, Dar es Salaam
0713961860
 
Mkuu kwakuwasaidia.

[FONT=&]MADENTI HUKO VYUONI[/FONT] [FONT=&]Hakika sisi wazazi,mno mwatufedhehesha,[/FONT] [FONT=&]Madenti wa siku hizi,sana mwatunyong'onyesha,[/FONT] [FONT=&]Kwanza ni hayo mavazi,kweli mwatuaibisha![/FONT] [FONT=&]Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.[/FONT] [FONT=&]Madenti huko Vyuoni,bure mwajidhalilisha,[/FONT] [FONT=&]Mwazurura mitaani, na usiku "kujirusha",[/FONT] [FONT=&]Mkifeli Mitihani,Mwalimu "kanikomesha"![/FONT] [FONT=&]Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.[/FONT] [FONT=&]Haiba ya Mwanafunzi,siku hizi imekwisha,[/FONT] [FONT=&]Si kama za kwetu enzi,mengi tulijiepusha,[/FONT] [FONT=&]Masomo tuliyaenzi,tulisoma tukakesha![/FONT] [FONT=&]Kuweni Waadilifu, Madenti huko Vyuoni.[/FONT] [FONT=&]Zimewajaa tamaa, kuharakia maisha,[/FONT] [FONT=&]Chumbani vitu hujaa,wenzenu kuwaringisha,[/FONT] [FONT=&]Usiku ndio balaa,mambo yenu yanatisha![/FONT] [FONT=&]Kuweni Waadilifu, Madenti
 
Wanafunzi kama hamtaki kuamini hili muulizeni Shaurimbaya.

saiz analalama na GPA yake!!

kazi ni kwenu.
 
Mtu kasomea pspa au community development anajipa matumaini eti "mimi bila lakinane sisaini mkataba" kisa tu wamewaona wachache walioajiriwa wanawadanganya kuwa wanalipwa zaidi ya 1 M.
Matokeo yake,siku zinaenda,hata pesa ya kununua gazeti inakosekana,hata soli ya kiatu inapinda kwa matumaini hewa.
 
Ingekua vizuri pia kwa wale wanaojipamba kwa majina ya vyuo wanavosomea wapate ujumbe huu.
 
Ndwele tena ya leo kali vibaya...........vijana hilini somo lenye Adili lifuateni.
 
Tena wengine hata aina ya mjengo na usafiri huwa wanaplan mapema...
Hata MIMI kabla sijarudi uraiani nlichokuwa nakiwaza ni Rav4 L new model na mjengo wa ghorofa moja bt tangia nimeingia uraiani nafikiria ni jinsi gani nitamanage matumizi yangu kusudi niweze ku-save pesa nipate mtaji niwe mjasiriamali!...Ni kweli,nawaonea huruma sana wadogo zetu huko vyuoni.
Mkuu Zyamwelele ulichokiandika ni ukweli 100%
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom