Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,712
Inafahamika kuwa,inapotokea mtoto akazaliwa "nje ya ndoa",mtoto yule ndo anaadhibiwa kwa kuitwa jina baya sana,eti mtoto haram(silipendi kabisa jina hili).Pia mwanandoa mmoja anapocheat na akagundulika na ndoa kufa bado watoto wanakuja kupata adhabu ya kuishi malezi ya mzazi mmoja na pengine malezi ya hatari kama mzazi mmoja hatakua imara,na pengine mzazi atawatelekeza watoto na watoto kubadilika jina na kuitwa watoto wa mtaani utafikiri mtaa ndo umewazaa,au huitwa "chokoraa" kwa sababu ya starehe ya mtu mmoja.Yapo matatizo mengi yanayosababisha viumbe hawa wateseke usiku kwa baridi kwa sababu hawana pa kulala kisa mama au baba maisha yamemshinda na kuwatelekeza.Hivi dhambi hizi kubwa namna hii ni mwanadam mwenye akili anazifanya kweli?Wengine unakuta ana watoto utafikiri ameahidiwa zawadi kwa kuzaa,watoto wenyewe shule hawaendi kama wanaenda hawana hata viatu na shati la shule halijulikani rangi,hivi umelazimishwa kuzaa?Jamani haya majina sijui mtoto haram,mtoto wa mtaani n.k,nani kayaleta?Kwanini tuwaadhibu watoto kwa makosa yetu?Jamani tunapofanya madudu hebu tukumbuke viumbe visivyo na hatia aidha vitakavyopatikana kutokana na kitendo hicho au kama unacheat na una watoto,hebu fikiri ukijulikana wanao watakua na maisha gani?