kichomiz
JF-Expert Member
- Feb 28, 2011
- 19,013
- 11,949
Wakuu heshima mbele.
Mwenzenu katika mihangaiko yangu ya kusaka mkate wa kila siku,
Leo nimeshangazwa na sheria za wilaya ya Chato au sijui ni Tanzania nzima?na sijui hii sheria Bunge la JMT lilikaa lini na kuipitisha,nimeamka leo asubuhi mida ya saa 2:00 na kuelekea dukani kununua mswaki, nikashangaa kuona maduka yote yamefungwa.
Nilipouliza wenyeji wakaniambia hapa Chato kila alhamisi watu hawatakiwi kufanya shughuli zao mpaka ifike saa nne unusu,
Hali kadharika na usafiri ni hivyo hivyo, nilipouliza kwa nini nikaambiwa eti imeteuliwa kuwa ni siku maalum ya usafi.
Kwa sasa niko hapa halmashauri napo shughuli hazifanyiki, maofisi yamefungwa mpaka ufike muda husika,nilipohoji nikaambiwa hii ni sheria ya mkuu wa wilaya.
Na ukibainika unafanya kazi faini ni tsh 100,000: Na wanasema inamwezi mmoja sasa.
My take.
Je hiii sheria ni kweli ipo kwenye sheria za JMT au ni maamuzi binafsi?
Na je serikali haioni kama inapoteza mapato kwa kwa kupoteza masaa 4 ya kazi?
Je na hawa wafanya wanaosababishiwa hasara ya mapato yao,wanaweza kuwashitaki na kudai fidia?
Elimu ya uraia bado inahitajika sana maeneo kama haya.
Chanzo:
Mimi mwenyewe.